Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,558
- 7,935
Hayo maneno ya siri ndio hayo shabahabahababa ahaba sindiyo ? watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Ndugu yangu, ukisikia mtu ananena: "shakakakakakakkaka" hayo sio maneno ya kipuuzi, bali ni lugha za rohoni ambazo Biblia imethibitisha. Imeandikwa: ‘Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho.’ (1 Wakorintho 14:2). Hapa Paulo anaonyesha wazi kwamba kuna kunena lugha ambazo akili ya mwanadamu haielewi, kwa sababu ni siri za kiroho mbele ya Mungu.
Ndiyo maana pia akaongeza: ‘Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda. (1 Wakorintho 14:14). Hii inamaanisha kwamba sauti au maneno yanayosikika yanaweza kuonekana kama hayana mpangilio kwa masikio ya kawaida, lakini kwa Mungu ni maombi ya rohoni yaliyo safi kabisa.
Najua kuna baadhi ya watu huwa wanaigiza kunena kwa lugha. Hata hivyo, wanaojazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha bila kuigiza, wapo wengi.
Huu uzi unawahusu pia ninyi. Si mnakiri kwamba mnamwamini Yesu? Sasa Yesu ndiye aliyeahidi kwamba atatuletea msaidizi(Roho Mtakatifu) na ahadi yake ilitimia siku ya Pentekoste. Petro na wanafunzi wa Yesu walijazwa Roho Mtakatifu. Na ujazo huo unaendelea hadi leo kwa kila aliyetubu dhambi na kumwamini Yesu.Huu uzi mpambane wnyewe makafiri kwa makafiri, kobaz tukiusishwa hapa alietutaja atajuta hiyo mitus yake
Hili fungu bado linazungumzia mbinguni pia ukimuamini yesu atakupa uzima wa milele na utastarehe naye kwenye ufalme lakini ni hadi siku za mwisho baada ya masumbuko na mateso ya dunia hakuna raha duniani tangu dhambi ilipoingia.Kama unaamini hivyo vifungu vinazungumzia watakaofika mbinguni; na kifungu hiki je: Mt 11:28-30
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini
Kama wewe unasubiri uingie mbinguni ndo upate raha, nakupa pole, mimi nina raha nafsi mwangu hapa hapa duniani kabla sijaenda mbinguni. Ndio sababu niliandika uzi hapa kwamba kuokoka ni kutamu - ni rahaHili fungu bado linazungumzia mbinguni pia ukimuamini yesu atakupa uzima wa milele na utastarehe naye kwenye ufalme lakini ni hadi siku za mwisho baada ya masumbuko na mateso ya dunia hakuna raha duniani tangu dhambi ilipoingia.
Nani aliongea kama hivi kipindi cha mitume na manabii au hii ni ya hivi leo tu ?Hiyo shabahabahababa ni mfano tu. Mtu anayenena kwa lugha anafanya hivyo kwa kujaliwa na Roho Mtakatifu mwenyewe. Hajitamkii tu shabahabahababa
Mimi sina raha duniani na nimeamua kumfuata mungu sio kwa sababu ya raha au ahadi zake za majumba na fahari bali kwasababu amestahuli sifa.Kama wewe unasubiri uingie mbinguni ndo upate raha, nakupa pole, mimi nina raha nafsi mwangu hapa hapa duniani kabla sijaenda mbinguni. Ndio sababu niliandika uzi hapa kwamba kuokoka ni kutamu - ni raha
Jamani asiwadanganye mtu — kuokoka ni kutamu!
Hii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu: Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu...www.jamiiforums.com
Lakini watu wasio mjua mungu wanasema wamekwisha okolewa wakati hukumu bado ? je unaweza kuokolewa kabla ya ukumu kwamba ulithi Jerusalem au jehanamu?Ni kweli kabisa! Hiyo ni Ahadi ya Mungu kwa kila aliyeokolewa.
Hapo hakuna raha kama mnavyoijua bali utopia. Ukisinzia, huwa hujitambui. Hivyo, matatizo yako huahirishwa hadi utakapoamka. Sasa huko mbinguni (kaburini) unalala bila kuamka wala kuwa na chembe hata ya kujijua. Unakuwa umekufa. Ndiyo maana yesu alisema huko hakuna kuoa au kuolewa tofauti na mohamed aliyewahadaa kuwa watakwenda kule kufanya ngono na wanawake kwa makumi. Hakuna kitu kama hicho. Hizo ndude zenyewe zitakuwa zimeishaoza kaburini.Hivyo vifungu vya raha vinazungumzia watu watakao fika mbinguni sio duniani
- Ana amani na furaha ya kweli kama ilivyoandika katika Warumi 14:17: “Maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu”
Hakuna raha ukiwa na roho mtakatifu huku duniani bali majuto, yesu mwenyewe alilia msalabani alibeba mzigo
Mitume wali uwawa kwa ukatili sana hatuwezi kusema walikuwa na raha wakati wengine walichunwa ngozi, huu ni mfano harisi ni kwa namna gani roho mtakatifu anafanya kazi ndani ya mtu.
Mitume hawakuongea lugha zisizo eleweka mfano shabakabsjakam, malaika hawakuwai kuongea, yesu hakuwai kuongea, manabii pia waliandika biblia kwa kuongozwa na roho mtakatifu kwa jumla ya vitabu 66 na hatuoni sehemu ya iliyoandikwa shabansnajsnsnjs, hakuna vitu kama hivi kwenye maandiko.
Lakini watu wasio mjua mungu husema wanasikia raha wanaroho mtakatifu na wanaongea kama machizi lakini nakwambia mungu hayupo ndani yao
Kama siku ile mungu atawachukua watu na kuwafanya madondocha wasiojitambua, je angemtoa mwanae wa pekee afe ili wanadamu wa mwamini ili iweje, ?Hapo hakuna raha kama mnavyoijua bali utopia. Ukisinzia, huwa hujitambui. Hivyo, matatizo yako huahirishwa hadi utakapoamka. Sasa huko mbinguni (kaburini) unalala bila kuamka wala kuwa na chembe hata ya kujijua. Unakuwa umekufa. Ndiyo maana yesu alisema huko hakuna kuoa au kuolewa tofauti na mohamed aliyewahadaa kuwa watakwenda kule kufanya ngono na wanawake kwa makumi. Hakuna kitu kama hicho. Hizo ndude zenyewe zitakuwa zimeishaoza kaburini.
Mkuu tunaokolewa na Kuhesabiwa Haki kwa IMANI SI kwa Matendo ya Sheria!Lakini watu wasio mjua mungu wanasema wamekwisha okolewa wakati hukumu bado ? je unaweza kuokolewa kabla ya ukumu kwamba ulithi Jerusalem au jehanamu?
Yesu alikufa ili kuwafanya muwe makuhani mtubu yeye amekwenda zake kwa baba kuandaa makao tazama atarudi tena na mawingu kuhukumu endapo siku hiyo utarithi nchi mpya basi ndipo na useme umeokolewa na hukumu na hasira yake.
Olewake anayejihesabia amekwisha okolewa akijua kuwa siku ya hukumu bado na siku ile ifike haukumiwe je huku kujidai umeokolewa kuna maana gani ?
Lakini Usikalili elewa maandiko kwa maana watakao okolewa sio wale waliojitakasa na kujifanya weupe na kusikaMkuu tunaokolewa na Kuhesabiwa Haki kwa IMANI SI kwa Matendo ya Sheria!
(Marko16:16-17)-Aaminiye na Kubatizwa ATAOKOKA,asiyeamini ATAHUKUMIWA.
Watakaohukumiwa ni Wale wasioamini.
(Wagalatia2:15-16)
Mungu mwenyewe ndiye anatupa Neema ya Kushinda Dhambi,na tena ndiye atufanyaye Watakatifu kama Yeye(1Petro1:15-16),ili tusitahili kwenda Mbinguni kukaa naye,(Wafilipi3:14) na (1Wathesalonike5:23-25)
Tena msijisumbue kwa lo lote bali kwa kuomba! Kama anavyoshuhudia huyu ndugu ni Kuomba Mungu azidi kutujaza Roho wake atupe kuyashinda Majaribu.
Mifano ya watu walioamini wakahesabiwa wameokolewa na walishuhudia wakiwa hai! Watu wa nyakati za Kanisa la Kwanza!
(Matendo2:46-47)-wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA.
(Tito3:3-4)-Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, ALITUOKOA.
Vipi kwa Maandiko waliokolewa wakiwa hapa hapa duniani (na wameshakufa) au Walipoingia mbingu mpya na nchi mpya?
Mpendwa ni kushauri usisikilize haya Mafundisho Manyonge yanayopotosha kuwa tutaokolewa tukishafika Mbinguni au Sijui Mbingu mpya na Nchi mpya!
Hayo yameandaliwa kwa ajili ya Watoto wa Mungu waliookolewa wakiwa hapa hapa duniani,WATAKATIFU WALIOKO DUNIANI!
(Zaburi16:3)
Kama umemwamini Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliyekuja kuuokoa ulimwengu na dhambi,tayari umeokolewa.
“Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafishwa; bali waovu watafanya maovu; wala hapana mtu mwovu atakayefahamu; bali wenye hekima ndio watakao okolewa.”
Soma uzi huu utajua nini maana ya kuokoka au kwanini watu wanasema wameokolewa kabla ya siku ya hukumuLakini watu wasio mjua mungu wanasema wamekwisha okolewa wakati hukumu bado ? je unaweza kuokolewa kabla ya ukumu kwamba ulithi Jerusalem au jehanamu?
Yesu alikufa ili kuwafanya muwe makuhani mtubu yeye amekwenda zake kwa baba kuandaa makao tazama atarudi tena na mawingu kuhukumu endapo siku hiyo utarithi nchi mpya basi ndipo na useme umeokolewa na hukumu na hasira yake.
Olewake anayejihesabia amekwisha okolewa akijua kuwa siku ya hukumu bado na siku ile ifike haukumiwe je huku kujidai umeokolewa kuna maana gani ?
Mafundisho mazur, kama una whatsup link tuunge tuendelee kujifunzaNi raha isiyoelezeka kwa urahisi, Roho Mtakatifu anapokujaza. Moyo unakuwa na amani na furaha ambayo dunia haiwezi kukupa. Unahisi uwepo mkubwa wa Mungu ndani yako. Unaanza kunena kwa lugha mpya, na kujiunga na ulimwengu wa rohoni. Unaanza kuwasiliana na Mungu directly.
Kama bado hujajazwa Roho Mtakatifu, anza kuomba ujazwe. Ila ngoja kwanza nikuelezee zaidi faida za kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, ili uwe na kiu ya kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ukijazwa, unapata nguvu ya kushinda dhambi na majaribu. Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa kuishi maisha matakatifu na kumshinda shetani.
Utapata nguvu ya kushuhudia. Unapojazwa Roho Mtakatifu, unakuwa na ujasiri wa kutangaza habari njema za Yesu Kristo ulimwenguni, na kushuhudia utukufu wa Mungu maishani mwako.
Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu. Ukijazwa, utaanza kuomba maombi yenye kina. Kunena kwa lugha kutakuwezesha kuomba mambo ambayo akili yako haiwezi kuyafikiria, kwa kuwa Roho mwenyewe ataomba kupitia kwako.
Kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha sio hadithi, ni experience halisi ya kiroho, inayoambatana na raha isiyoelezeka. Ni zawadi ambayo Mungu anatupatia sisi watoto wake, ili tuishi kwa ushindi, furaha na ushirika wa karibu naye.
Wakristo wa kwanza walijazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Wakanena kwa lugha mpya na kupata nguvu ya kuwa mashahidi wa Yesu (Mdo 2:4)
View attachment 3464355
Kuokoka ni lugha ya kiswahili inayomaanisha maana yake ni kuokolewa au unamaana nyengine ? sijausoma huo uzi kwasababu ninajua ndani yake pengine kuna pumba pumba tuSoma uzi huu utajua nini maana ya kuokoka au kwanini watu wanasema wameokolewa kabla ya siku ya hukumu
Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?
Kama umekuwa ukijiuliza maswali kama hayo, leo ni siku yako ya kujua maana ya kuokoka na pengine ndiyo siku yako na wewe ya kuokoka. Kuokoka ni neno tu la kawaida la Kiswahili lenye maana ya kusalimika au kunusurika kutoka katika janga, maafa makubwa au hatari yoyote inayokuijia. Mfano mzuri ni...www.jamiiforums.com
Nanena kama Roho anavyonijalia.
Siku ya Pentekoste, walipojazwa Roho Mtakatifu, Maandiko yanasema "wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kunena" (Matendo 2:4). Wenyewe hawakusema wanaongea lugha gani, bali waliokuwa wakiwasikiliza ndio walioshuhudia kwamba wananena lugha zao (Matendo 2:6-8). Vivyo hivyo leo, kunena kunaweza kuwa kwa lugha za wanadamu au lugha za rohoni ambazo hazieleweki kwa akili ya kawaida ila ni mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu (1 Wakorintho 14:2). Umenipata?
Muulize hivi hii style ya kunena kwa lugha sizisoeleweka nani aliyeifanya au imeanza hivi karibuni kipjndi hiki, kama manabii waliandika vitabu vingi hatujaona lugha kama za ahabakdbsjaknshana, wala malaika hawakuwa wakiongea lugha za hivi bali waliongea lugha zinazo eleweka japo hawakuwa wayahudi wala waebrania lakini waliongea na manabii na kuelewana.Lugha za rohoni ni lugha gani?
Ukichaa unasema ni Raha?!Ni raha isiyoelezeka kwa urahisi, Roho Mtakatifu anapokujaza. Moyo unakuwa na amani na furaha ambayo dunia haiwezi kukupa. Unahisi uwepo mkubwa wa Mungu ndani yako. Unaanza kunena kwa lugha mpya, na kujiunga na ulimwengu wa rohoni. Unaanza kuwasiliana na Mungu directly.
Kama bado hujajazwa Roho Mtakatifu, anza kuomba ujazwe. Ila ngoja kwanza nikuelezee zaidi faida za kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, ili uwe na kiu ya kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ukijazwa, unapata nguvu ya kushinda dhambi na majaribu. Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa kuishi maisha matakatifu na kumshinda shetani.
Utapata nguvu ya kushuhudia. Unapojazwa Roho Mtakatifu, unakuwa na ujasiri wa kutangaza habari njema za Yesu Kristo ulimwenguni, na kushuhudia utukufu wa Mungu maishani mwako.
Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu. Ukijazwa, utaanza kuomba maombi yenye kina. Kunena kwa lugha kutakuwezesha kuomba mambo ambayo akili yako haiwezi kuyafikiria, kwa kuwa Roho mwenyewe ataomba kupitia kwako.
Kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha sio hadithi, ni experience halisi ya kiroho, inayoambatana na raha isiyoelezeka. Ni zawadi ambayo Mungu anatupatia sisi watoto wake, ili tuishi kwa ushindi, furaha na ushirika wa karibu naye.
Wakristo wa kwanza walijazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Wakanena kwa lugha mpya na kupata nguvu ya kuwa mashahidi wa Yesu (Mdo 2:4)
View attachment 3464355