Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Halina ubishi hata kiduchu kwa miaka yote tangu mwaka 1995 hayati JPM amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha barabara za Tanzania zinaunganika. Na kweli sasa hivi nchi imepiga hatua kwa kuwa na miundo mbinu mizuri. Pia alipokuwa rais wa JMT aliwakingia kifua wamachinga wasiwekewe kiwingu na kufanya biashara kwa uhuru wao.
Lakini hii pekee ndio inakuwa sababu ya kusema hakuna madoa yaliyowekwa na uongozi wake au utawala wake?
Muamar Ghadafi alitengeneza taifa lililokuwa na miundo mbinu mizuri tena ya kisasa kuliko hata nchi za ulaya. Alihakikisha watu wanapata elimu bure,ndoa bure na chakula bure, lakini doa pekee lilimfanya mpaka akauliwa kwa fedheha ni ukatili dhidi ya binadamu, tena alioufanya kwenye gereza maarufu la Abu salim. Maana alikuwa hataki kukosolewa.
Ni kweli kabisa hayati JPM alikuwa mfuatiliaji na msimamizi mzuri ndio maana alifanikisha nchi ikawa na miundo mbinu mizuri, ndio kusema alitawala bila dosari?