Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Tusidanganyane bwana hakuna raha kama kukaa kwako kuondokana na makodi na kero za mwenye nyumba! unakuta unapanga nyumba huruhusiwi chochote mfano hata kufuga kuku wala mbwa zaidi ya kupanda maua tu na unatoa kodi ndefu wakati ukiishi kwako una uhuru na husumbuliwi kwa kodi ya mwezi wala mwaka. Kodi yoyote sikuzote inaumiza
 
"Verry caluculating"
Nimependa sana huo msemo wako mama watoto, iko hivi..
Biashara zina changamoto ni kweli, unachopaswa kufanya ni kujifunza kuzizoea na kucheza nazo wakati wote na kujifunza namna bora ya kuzitatua.
Kama kuwa na nyumba yangu kutanifanya nirelax hiyo kwangu sio relief ni shida nyingine sihitaji kurelax kwasasa, huo muda utafika ila sio sasa.
Why relaxing at this age?

Inawezekana tunatofautiana kidogo lakini nikiona kuna gape fulani kwenye biashara yangu na naweza kupata pesa hata kama nalipa kodi kesho nitachukua hiyo pesa na nitawekeza, mwenye nyumba tutaongea tu si ni binadamu? halafu ukishakuwa MWAMINIFU kwenye maisha si rahisi kukwama. Naweza nikamkopa fulani nikamlipa fulani wakati nasubiri chazo fulani kitoe pesa nirudishe kwa mtu A. Lakini siwezi kukubali pesa inipite hivi hivi na nina WATU

Concept ya biashara ni pana sana.. yani ukiwa mfanyabiashara hata maisha yako binafsi unavyoongea, unavyowasiliana na watu, Mipango yako, matumizi yako, familia yako vinatakiwa viwe kibishara.

1.Jenga mahusiano mazuri na watu (marafiki wa faida) achana na kuambatana na watu wanaokata tamaa haraka.
2.Kuwa mwaminifu
3.Fanya utafiti kila mara.
4.Soma/ Jisomee ( Ongeza maarifa ya kitu unachofanya /kusudia kufanya kila upatapo fursa)
5.USIOGOPE.
Unasema hutaki kurelax sasahivi utarelax baadae je unaijua kesho yako? ndugu maisha ni leo hayo ya kesho ni majaliwa! yaleyaleee nimevuna mazao mengi nimeweka ghalani sasa acha nafsi ifurahi kwa kula na kunywa akasikia sauti mpumbavu wewe usiku huu naitaka roho yako. ISHI VIZURI SASA
 
Baishara huwa ni salama kwa mtu mwenye mtaji mkubwa na aliye diversify vyanzo vyake tofauti na hapo mtu utarudi kule kule ulikokuwa .

Ndio maana wanaojiita Wana biashara eti nzuri vimtaji vyao wengi ni 5-10 mln sasa hapo si waganga njaa tuu hao kuna pesa hata ya kwenda vacation mwisho wa mwaka?
Kama nakuelewa kwa mbaaali. Japo ml. 5-10 ni mtaji mkubwa au mdogo kutegemea na nature ya biashara.
 
Biashara ni Risk takers.
Nyumba hakuna risk.

Kule kuogopa kuingiza 20m kwenye biashara zikaharibika zote .

Mtu anaona Bora ajenge awe na kijumba chake na maisha simple for the rest.

Marisk takers ndo wanajitungua liwalo na liwe wanaingia kwenye biashara muda mfupi wanafanikiwa.

Wakati nyumba ya 20m inaingiza 100,000/= kwa mwezi .
Mfanyabiashara anaingiza 2ml kwa mwezi.

Vikao vya kuitana freemason,na kupeana makafara ambayo hatuyajui vifungwe kuanzia Leo.

Overall wote hatuwezi kuwa wafanyabiashara na wote hatuwezi kumiliki nyumba.

So Kila mtu afanye anachokiweza.
 
Biashara utakayoanzisha baada ya kujenge nyumba mara nyingi ni ya kuganga njaa tu si kwa ajili ya mafanikio makubwa.
Nikiwa naishi kwangu na nikaweza kuokoa 300k ya kulipa kodi kwa baba mwenye nyumba itakua nimeokoa kias kikubwa Cha pesa
Unavyosema nikijenga siwez kuwa na biashara kubwa nitakua na biashara ya kugangaa njaa tu huo ni uoga wako mwenyewe, maana hata hyo biashara unayo anzisha unaweza kuanzisha na isifanikiwe ikaishia kugangaa njaa na kumtafutia baba mwenye nyumba kodi tu.
Bora niwe na kwangu na nianzishe biashara kwa kujiripua bila kuwa na presha kuwa biashara ikianguka nitakosa hata sehem ya kuish na itabidi nianzie 0 kabisa.
 
Unasema hutaki kurelax sasahivi utarelax baadae je unaijua kesho yako? ndugu maisha ni leo hayo ya kesho ni majaliwa! yaleyaleee nimevuna mazao mengi nimeweka ghalani sasa acha nafsi ifurahi kwa kula na kunywa akasikia sauti mpumbavu wewe usiku huu naitaka roho yako. ISHI VIZURI SASA
Mkuu, Nikisema siwezi kurelax kiuchumi haimaanishi siishi vizuri, ninaishi vizuri ila kuna malengo napambana yatimie na kuishi vizuri sio lazima uwe kwenye nyumba yako.
Labda nikuulize..

Ukipata nafasi na ukaambiwa upande miti hekari 100 na kukomaa kwake mpaka kuvuna ni miaka 20 hautapanda?

Je hauna malengo ya miaka 20 ijayo kwakuwa unaogopa kufa?
Kama ndivyo, huo ni ubinafsi mkubwa sana

Sio kila uwekezaji utakunufaisha wewe. Tunawekeza kwaajili yetu na vizazi vyetu
Kama kifo kikija its okay, siwezi kuwa na mashaka na kitu beyond my control.

Mipango yangu itaendelea, Mungu akisema inatosha, wataendelea wengine mimi nitakuwa nimepigana vita na imani nimeilinda haswa.
 
Biashara ni Risk takers.
Nyumba hakuna risk.

Kule kuogopa kuingiza 20m kwenye biashara zikaharibika zote .

Mtu anaona Bora ajenge awe na kijumba chake na maisha simple for the rest.

Marisk takers ndo wanajitungua liwalo na liwe wanaingia kwenye biashara muda mfupi wanafanikiwa.

Wakati nyumba ya 20m inaingiza 100,000/= kwa mwezi .
Mfanyabiashara anaingiza 2ml kwa mwezi.

Vikao vya kuitana freemason,na kupeana makafara ambayo hatuyajui vifungwe kuanzia Leo.

Overall wote hatuwezi kuwa wafanyabiashara na wote hatuwezi kumiliki nyumba.

So Kila mtu afanye anachokiweza.
Bado mchanga sana kwenye haya maisha
 
Chonde chonde haya mawazo yatoke mioyoni mwenu

Yasiwe yamenukuliwa kutoka kwa vitabu na makala mbalimbali
 
"Verry caluculating"
Nimependa sana huo msemo wako mama watoto, iko hivi..
Biashara zina changamoto ni kweli, unachopaswa kufanya ni kujifunza kuzizoea na kucheza nazo wakati wote na kujifunza namna bora ya kuzitatua.
Kama kuwa na nyumba yangu kutanifanya nirelax hiyo kwangu sio relief ni shida nyingine sihitaji kurelax kwasasa, huo muda utafika ila sio sasa.
Why relaxing at this age?

Inawezekana tunatofautiana kidogo lakini nikiona kuna gape fulani kwenye biashara yangu na naweza kupata pesa hata kama nalipa kodi kesho nitachukua hiyo pesa na nitawekeza, mwenye nyumba tutaongea tu si ni binadamu? halafu ukishakuwa MWAMINIFU kwenye maisha si rahisi kukwama. Naweza nikamkopa fulani nikamlipa fulani wakati nasubiri chazo fulani kitoe pesa nirudishe kwa mtu A. Lakini siwezi kukubali pesa inipite hivi hivi na nina WATU

Concept ya biashara ni pana sana.. yani ukiwa mfanyabiashara hata maisha yako binafsi unavyoongea, unavyowasiliana na watu, Mipango yako, matumizi yako, familia yako vinatakiwa viwe kibishara.

1.Jenga mahusiano mazuri na watu (marafiki wa faida) achana na kuambatana na watu wanaokata tamaa haraka.
2.Kuwa mwaminifu
3.Fanya utafiti kila mara.
4.Soma/ Jisomee ( Ongeza maarifa ya kitu unachofanya /kusudia kufanya kila upatapo fursa)
5.USIOGOPE.
Hahaha kama nimekosea unanichana tu sio unanisifia uongo hapa. Upo sahihi kamesa na maelezo yako yana-make alot of sense ila mimi kipaumbele changu ni makazi kwa kweli maana nikiangalia kodi inavyonipaga stress hapana kwa kweli. Unapata kadili kadogo unapata kahela badala ufikirie vitu vya maana unamfikiria mwenye nyumba, kodi huwa inaniuma mimi utadhani nampa ya bure
 
Hahaha wala sikukusudia kukukosoa baby nimependa tu ukokotozi wako
Nakuelewa sana sana
kuwa na vipaumbele ni muhimu sana kwenye maisha ni jambo jema na linaonyesha kiwango chako cha ukomavu kuliko kufanya mambo kiholela.

Unaweza kunidokeza makadirio ya budget yako ya kujenga nyumba unayoitaka?
labda naweza kutia neno.
 
Watanzania wengi wanaokaa kwao haimaanishi wana raha, wengi bado ni omba omba na tegemezi kwenye hizo nyumba zao.
Ni baba na mama wenye nyumba ambao ni mafukara!
Pia jifunze tofauti ya rent na tax.
Tusidanganyane bwana hakuna raha kama kukaa kwako kuondokana na makodi na kero za mwenye nyumba! unakuta unapanga nyumba huruhusiwi chochote mfano hata kufuga kuku wala mbwa zaidi ya kupanda maua tu na unatoa kodi ndefu wakati ukiishi kwako una uhuru na husumbuliwi kwa kodi ya mwezi wala mwaka. Kodi yoyote sikuzote inaumiza
 
A home is your base, it's your empire, kupanga ni utumwa flan
Utumwa kwa nani?
Wewe ndio boss, unamlipa mwenye nyumba unakuwaje mtumwa?

Inawezekana unazungumzia nyumba za kupanga za kushare vyoo wapangaji kumi
kweli hizo zinakera maana utaambiwa sijui zamu usafi, mara kuchanga umeme nk

Lakini mtu anayeishi kwenye apartment yake kero inatoka wapi?
Ndio maana nasisitiza TAFUTA PESA.
Ukiwa na pesa utachagua wapi uishi nani umuepuke.
 
Sababu umetoa pesa kuijenga and still utakua unato pesa kuihudumia.
Kitu chochote ambacho pesa unayotoa ni nyingi kuliko kinavyokuingizia ni liability
Watu wanajenga nyumba kusevu cost za rent halafu wewe unasema ni liability kwa sababu unaihudumia, niambie hizo gharama za kuihudumia nyumba ni kiasi gani kwa mwaka hadi iizidi rent unayolipa kwa landlord? Mfano mimi landlord wangu namlipa 3,600,000 kwa mwaka lkn ukiniuliza mara ya mwisho kuja kuihudumia hiyo nyumba sikumbuki, na hata akija hawezi kumaliza hata laki 5
 
Utumwa kwa nani?
Wewe ndio boss, unamlipa mwenye nyumba unakuwaje mtumwa?

Inawezekana unazungumzia nyumba za kupanga za kushare vyoo wapangaji kumi
kweli hizo zinakera maana utaambiwa sijui zamu usafi, mara kuchanga umeme nk

Lakini mtu anayeishi kwenye apartment yake kero inatoka wapi?
Ndio maana nasisitiza TAFUTA PESA.
Ukiwa na pesa utachagua wapi uishi nani umuepuke.
Sasa ukiwa na Hela kwanini upange
 
Back
Top Bottom