"Verry caluculating"
Nimependa sana huo msemo wako mama watoto, iko hivi..
Biashara zina changamoto ni kweli, unachopaswa kufanya ni kujifunza kuzizoea na kucheza nazo wakati wote na kujifunza namna bora ya kuzitatua.
Kama kuwa na nyumba yangu kutanifanya nirelax hiyo kwangu sio relief ni shida nyingine sihitaji kurelax kwasasa, huo muda utafika ila sio sasa.
Why relaxing at this age?
Inawezekana tunatofautiana kidogo lakini nikiona kuna gape fulani kwenye biashara yangu na naweza kupata pesa hata kama nalipa kodi kesho nitachukua hiyo pesa na nitawekeza, mwenye nyumba tutaongea tu si ni binadamu? halafu ukishakuwa MWAMINIFU kwenye maisha si rahisi kukwama. Naweza nikamkopa fulani nikamlipa fulani wakati nasubiri chazo fulani kitoe pesa nirudishe kwa mtu A. Lakini siwezi kukubali pesa inipite hivi hivi na nina WATU
Concept ya biashara ni pana sana.. yani ukiwa mfanyabiashara hata maisha yako binafsi unavyoongea, unavyowasiliana na watu, Mipango yako, matumizi yako, familia yako vinatakiwa viwe kibishara.
1.Jenga mahusiano mazuri na watu (marafiki wa faida) achana na kuambatana na watu wanaokata tamaa haraka.
2.Kuwa mwaminifu
3.Fanya utafiti kila mara.
4.Soma/ Jisomee ( Ongeza maarifa ya kitu unachofanya /kusudia kufanya kila upatapo fursa)
5.USIOGOPE.