Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Mkuu vipi nimuite yule rafiki yako anayependa nyumba aje kukupinga
Yupi huyo? Kujenga ni woga tu. Hata ukisoma humu sababu za watu utasikia mara unaweza kupoteza kazi ukakosa kodi,mara biashara itakufa utakosa kodi,ada. Ukiangalia deep unaona ni woga tu. Muhimu tafuta hela, jenga kwa starehe sio hadi unajibana hela ya kula kisa woga utalala nje!
 
Nakubaliana na wewe kujenga nyumba sio vita. Hata real estate naipinga kama unavyoipinga wewe
 
Mimi kujenga na biashara naona zote ni hobby.
Japo kujenga kuna faida zaidi kama itakuwa first priority maanajengo huongezeka thamani kila siku--na safari ya ujenzi huanzisha nyingine,ni kama addiction.Ukijenga kwanza(hata kama ni kwa mkopo)--utatumia gharama za kukodisha nyumba kulipia nyumba yako na utakapomaliza--hiyo pesa utaiwekeza kwenye jambo jingine.Ukiwa na nyumba assurance ya umiliki ipo.
Biashara nayo ni njema,kwa wale walioamua kupita njia hiyo--ukiwekeza kwenye mtajii hadi biashara itakapokuwa kubwa--nalo ni wazo.
We all have priorities---na sio lazima tufanane.
Usafiri,Nyumba,Pesa mfukoni,Chakula mezani--na kufurahia maisha inatosha--huwezi fanya kila kitu.
 
Biashara kabla ya ujenzi unatakiwa uwe makini sana, biashara ina sayansi yake. Nashauri jenga kwanza huku unafikiria hiyo sayansi ya biashara. Kumbuka katika mahitaji makuu ya binadamu, nyumba ipo ila biashara haipo, tafakari.
Hiyo pesa ya mshahara na mikopo unayotumia kujenga miaka 5 au 7 saba nyumba ya vyumba 4 si bora ungeiingiza kwenye biashara miaka 5 upate pesa za kutosha kukuwezesha kujenga ndani ya mwaka 1 au 2 na umalize kabisa huku ukiendelea kujipatia kipato kwenye uwekezaji wa pembeni ?
 
Hii inaweza kuwa sababu ya msingi watu kukimbilia kujenga nyumba zao hata kwa mikopo yenye riba kubwa huku baadaye wakiishi maisha ya omba omba.
 
Mimi naona kuwa na nyumba ni muhimu sana kama huna kipato cha uhakika. Ila kama una uwekezaji wenye uhakika sidhani kama kuna haja ya kukimbilia kujenga
Kama huna kipato cha uhakika inabidi ukazane na ujitihadi kupata kipato cha uhakika na sio kukumbilia kuzika pesa kwenye kiwanja na nyumba ambayo haitakusaidia kupata hicho kipato cha uhakika.
 
Njoo na haya mawazo ukiwa na umri wa miaka 50
 
Kama huna kipato cha uhakika inabidi ukazane na ujitihadi kupata kipato cha uhakika na sio kukumbilia kuzika pesa kwenye kiwanja na nyumba ambayo haitakusaidia kupata hicho kipato cha uhakika.
Njoo na haya mawazo ukiwa na umri wa miaka 50 na kuendelea
 
Binadamu Tuna vipao mbele vinavyo tofautiana.
Na Kuna watu wamekuja Duniani kufanikisha maisha ya watu wengine.
Hatuwezi fanya Biashara wote au kuajiriwa wote au kujenga wote.
Na chochote tufanyacho kinafaida kama sio kwangu basi kwa mwingine
Thread closed
 
Nimefanikiwa kujenga nyumba Moja ya kuishi Arusha, ambacho nimeona ni kwamba sitokuja jenga tena nyumba ya kuishi popote Tanzania instead nikifanikiwa kujenga ni za biashara tu na ni frames au mfano wa hv.

Nyumba za kuishi kwa kipato chetu ni Headache, nyumba unahaingaika nayo haiishi miaka mitano. Hapana huo upuuzi sifanyi tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…