Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Hakika!! Tena saa nyingine labda pesa iwe ya kupita ila kama ni endelevu huwa hakuna kuwaza hiyo.
Najua ile ndoto yako umeshaitimiza kwahiyo hata utakapokua bibi hapao baadae roho yako ilishapata kile ulichotamani.

Ila Shadeeya hujatimiza ahadi ya kunitumia ile ramani ujue, au hutaki saresare maua🤪🤪🤪, imenikonga roho sana ile aisee
 
Nimeongelea vyumba 12 vya kulala kama una studio inamaana una matumizi nayo
 
Hii picha ni kwenye mauzo ya nyumba ya vyumba 12 vya kulala
 
Kuna watu nature yao wanapenda ligi,kwahiyo anataka kuonyesha watu kuwa yeye ni nani badala ya kufikiria idadi ya watoto wake na maisha yake ya uzeeni ambapo watoto hawatakuwepo tena hapo nyumbani,ingawa kama una pesa ya kutosha kujenga hiyo nyumba siyo shida,ila kama hela yako ni ya kuunga unga sishauri...
 
Hata kama una pesa ndefu uzeeni huwo uwezo wa kufanya ma party hutakuwa nao si kwa pesa bali kwa nguvu kukuishia. Nyumba itabaki kama gofu wewe unatumua chumba kimoja jiko na sebule
 
inatakiwa kujenga nyumba kuendana na kipato chako, watanzania wengi kipato kidogo anataka kujenga lijumba likubwa , mara bati la msouth, matokeo yake linachukua miaka kukamilika, jenga nyumba kuendana na kipato chako,
Wewe umemwelewa mtoa mada. Nilivyoelewa mimi hawazungumzii matajiri wakubwa kama kina Bakhesa. Anazungumzia kina sisi. Mtu unakuta kipato chake ni kidogo lakini anang'ang'ana kujenga mjumba mkubwaa. Watu wa aina hii wako wengi sana.
 
100
 
Weweee!
EPA imekupitia, RADAR iko mfukoni, OGL ilipitia kwako,mzee wa milioni saba kwa Dakika ndo rafiki kipenzi, makontena yaliyovurumishwa bandarini robo ni ya kwako!

Sasa ukajenge nyumba kajamba nani ?

Utakuwa huitendei haki fuko lako!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…