Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,

Kweli, kabisa wenzetu wahindu wanapangisha NHC lakini hizo biashara zake zinamwingizia mpunga mrefu, heri uwe na nyumba ya kawaida na biashara ya maana
 
Kwangu mimi nyumba standard at least iwe.na 5 bedrooms ( Master ya baba na mama, girls room ,boys room, Guest room na dada wa kazi room) nje unaweza kuweka servant quarter kwa ajili wa kazi .. huo mtazamo wangu naweza kusahihishwa
Mkuu chumba cha house girl cha nini. Si alale na watoto wa kike wenzake?
 
Three bed rooms ni nyumba ya kimaskini sana.
Umeongea vyema kabisa.

Wengi wenye mijumba mikubwa wana zaidi ya vyumba huko ndani.

Kuna swimming pool, garage, movie theatre, sports arcade, bathrooms za kutosha, studio ya kurekodia, ofisi, library, walk in closets, kitchens za kutosha, living rooms za kutosha.

Sio kila mtu anapenda kujibana kwenye 3 bedrooms.
 
Mimi nimejenga vinne, lakini kuna nyumba ya wageni nje. Vitatu viko juu kimoja ensuite kiko chini. Hiki nitahamia uzeeni nitakaposhindwa kupanda ngazi.
Mimi nimejenga viine lakini ndani kuna kila kitu ofisi jiko stoo public toilet . Vyumba vyote seilf contained Master bed room ni kubwa sana yenye madiridha manne. Halafu nje nyuma kuna jiko na public toilet na car parking na nina watoti watatu tu. Lakini bado naiona ndogo.
 
Kwangu juu kuna master bedroom ambayo ni en suite na viwili vinashare toilet na bathroom ambayo ndiyo family toilet. Chini kuna choo cha wageni na chumba kimoja,
 
Umeongea ukweli mkuu
Mimi nyumba yangu ya kuishi kule kilimanjaro Ni ya vyumba 6 tu full stop
Nyumba zingine nimejenga za biashara nikakodisha mbeya,dar,mwanza siwezi kujenga jumba kuubwa Bila faida
 
Umeongea ukweli mkuu
Mimi nyumba yangu ya kuishi kule kilimanjaro Ni ya vyumba 6 tu full stop
Nyumba zingine nimejenga za biashara nikakodisha mbeya,dar,mwanza siwezi kujenga jumba kuubwa Bila faida
 
Back
Top Bottom