Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

Hivi kweli mtu anaweza kujenga nyumba moja na kuishi humo humo hadi anazeeka? Mimi naona nyumba 4-5 ndo zinanitosha
Kuna watu wanazeeka hawana hata nyumba moja wewe unauliza kuzeeka kwenye nyumba yako moja? Wewe ushajenga ngapi hadi sasa hivi? Ingekuwa unaamua tu wengi tungekuwa na nyumba nyingi sana
 
Nyumbani kwetu kulikua na nyumba tatu za vyumba 3 aisee wageni walikua hawakauki harafu wanakuja na familia zao , me mwenyewe nlivyo anza maisha nikapanga nyumba nzima ya vyumba 3 washikaji zangu wakafanya guest house bahati mbaya mimi ni muoga kumchama mtu nikawa naumia ndani kwa ndani, nyumba kubwa zina majaribu sana hasa kwa maisha ya mjini atatoka mtu ushagoo huko anadai amekuja kutafta maisha akikuta chumba kipo hatoki mpk ujitoe akili
 
Kuna watu wanazeeka hawana hata nyumba moja wewe unauliza kuzeeka kwenye nyumba yako moja? Wewe ushajenga ngapi hadi sasa hivi? Ingekuwa unaamua tu wengi tungekuwa na nyumba nyingi sana
Nyumba ya kwanza nitaanza kuijenga mwakani..Mungu akijaalia
 
...ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

vipi kama ni watoto wanne wasio na mafanikio?

tuna tatizo kubwa sana la ujengaji hoja na uchambuzi wa vitu hata vidogo vidogo... hasa hasa watu wa third world niliokutana nao duniani... hatufundishwi critical thinking tokea wadogo...
 
Kuna tofauti kati ya nyumba kubwa na nyumba yenye vyumba vingi.
Mimi nafikiri kuna tofauti kati ya nyumba kubwa na nyumba nzuri. Inaelekea watu wengi humu wanapenda nyumba kubwa.. yaani yenye vyumba vingi. Mimi napenda nyumba nzuri hata kama ina vyumba vichache. Binafsi sipendi ghorofa.
 
Ukubwa wa nyumba sio vyumba mfano wa nyumba kubwa kama ya Reg Mengi unazani inavyumba vingi ile.

Nyumba kubwa ni kitu muhimu maana ni nyumba inayokuwa na service mbalimbali mfano mimi napenda Gym, Library, Swimming hivi vyote nikiviweka kwenye nyumbayangu lazima uone kubwa ila sio eti kubwa kwaajili ya idadi ya vyumba.

Then kwenye idadi ya vyumba nyumba standard inaanzia vyumba 4 mpaka 5.
 
Watu tuliotokea kwenye umaskini (hasa wa africa) huwa tuna shida sana......mara nyingi huwa tunadhamini sana mali kuliko kitu kingine lakini pia tunapenda vitu vitakavyotuonyesha kwenye jamii.......yaani kujenga nyumba ya vyumba vitatu mtu anawaza hivi na uprofesa wangu wote watu wataniona je?........wakati huo huo wazazi ama jamaa zake wa karibu wanaishi kwenye nyumba za udongo kijijini hata kama hawaishi kwenye nyumba za udongo lakin maisha yao unakuta ni duni mno..... there are so many things we could do kwenye investments zikasaidia vizazi na vizazi.....tatizo letu ni exposure na umaskini
Huu ni mtazamo wako.. unaheshimiwa. Exposure.. Umasikini.. kusaidia ndugu na vizazi na vizazi.
Nani amesema ukijenga ghorofa unasimamisha huduma zingine?
Kwa kukusaidia tu: Watu waliojenga ghorofaz wana nyumba zingine ambazo ndugu zao wanazitumia.
Wana biashara zao zinazosaidia ndugu na vizazi.
Wamewekeza kwenye miradi itakayosaidia vizazi na vizazi.
Na pia wanaojenga maghorofa huku Africa wengi wao wanapambana kutafuta mkate huko overseas. Meaning exposure siyo tatizo.

Yote huanzia kichwani kwa mpangaji. Anahitaji nini ktk maisha yake.

Wengi wenye limited pocket kama wewe ndo mna mawazo mbano.. kuwa kujenga nyumba kubwa kumepitwa na wakati.. Its not true.
 
View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,
Ni ushamba mkubwa kwa sababu hata ukipangisha bei haitalingana na ukubwa wa nyumba,pia ukiishi mwenyewe baada ya watoto kuondoka nani atafanya usafi jumba lote hilo? Bi mkubwa atakuwa kachoka
 
View attachment 1273865

Una familia ya watoto wanne, umefanikiwa kimaisha watoto wanasoma na unajenga nyumba ya ghorofa vyumba 12 vya kulala.

Kwanza gharama za ujenzi ni kubwa, baada ya ujenzi kutunza nyumba ya vyumba 12 ni gharama kubwa sana. Hata ukiwa na mawazo ya familia kukutana watoto wanne wenye mafanikio si mara nyingi watakuwa nyumbani.

Nyumba ya vyumba vinne mpaka sita inatosha, pembeni unaweza kuweka houseboy quarter na guest wing.

Ukiwa mzee wewe na mke wako au mume wako kuishi kwenye nyumba ya vyumba 12 wakati watoto wote wana miji yao nayo ni gharama,

Ni wazo zuri japo kuna kitu umesahau, hizi nyumba si kwa ajiri ya kulala pekee.

Utakuwa unawatenga wanaokabidhi hati zao za nyumba benki.

Vyumba vitatu hapati mpunga sawa na wa mjengo kama huo.
 
Mleta mada acha kupiga chenga...hasara kuu ya nyumba kubwa ndugu yangu ni....WAGENI WATAFANYA KWAO..WATAHAMIA...hakuna asiejua kashkash za kuwa na familia kubwa hapa jijini....
watu wakiona jumba kubwa wanahamia...sasa wahamie watu 5..na wewe na mke na watoto na beki 3..labda watano..mnakua kumi (10)...lazima upaki gari..na bado hawajaanza tabia zao halisi...utahama kwako
 
Mijumba mikubwaaa unakaa na mume wako tu..... Watoto Wana miji yao. Matokeo yake mapepo na Mashetani yanahamia nyumbani kwenu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna tofauti kati ya nyumba kubwa na nyumba yenye vyumba vingi.

Sasa nyumba kubwa itakosaje vyumba vingi? Tatizo tukisikia chumba tunajua ni chakulala. Gym ni chumba, library ni chumba,chumba cha cinema,utility room. Hapo tayari vyumba vinne. Ongezea vyumba vya kulala vitatu tu. Sitting room, dining room, kitchen. Bado Choo cha jumuia.

Sasa hii ni 3-bedroom house ila ina vyumba vingine karibu 10! Hizi ndio nyumba za wenye hela.

Akina sisi ni 3-bedroom yenye jiko,sitting room na toilet. Ndio nyumba ya wastani. Ila ukichukulia juu juu kila mmoja atasemekana ana 3-bedroom house.
 
Back
Top Bottom