MBINU ZA KUKUSAIDIA USIFE NA BIASHARA YAKO /ZUIA KAMPUNI NA BIASHARA YAKO KUTOKUFA.
Kumhusu Mwandishi.
Kim Hvidkjaer, ni msomi wa masomo ya usimamizi wa biashara MBA kutoka chuo kikuu cha Copenhagen Business vilevile ni mwanzilishi wa kampuni ya kimasoko ambayo baadaye alikuja kuiuza, lakini pia yeye ni mwekezaji kwenye masoko ya hisa na majengo (Real Estate). Kim kwenye
maisha yake aliwahi kuwa milionea akiwa na umri wa miaka 31 lakini pia akaja akafirisika na kuanza upya tena na kuibuka tena akiwa mwenye mafanikio makubwa .
Leo anatupitisha kuangalia mambo ambayo hupaswi kuyafanya ili kuihami biashara yako kutokufa na iwe biashara yenyekujiendesha kwa faida na Mafanikio.
Tuzame Ndani kuyaona mengi;-
1.Ukiangalia takwimu za uanzishaji wa biashara waweza kuvutiwa sana nawe kuanzisha biashara ama kujitosa kwenye biashara, takwimu zinaonesha nchini marekani kila siku huanzishwa biashara Elfu kumi na mbili 12000na hii ni kusema kwamba kwa kila mwaka ni biashara millioni 4,400,000 huanzishwa lakini hali ya kusikitisha ni kuwa Asilimia 80 mpaka 90 ya biashara hizo hufa kabla ya kufikia kumbukizi la siku za Kuanzishwa kwake Ndani ya miaka mitano.
Ingia kwenye biashara lakini usijiambiekuwa itafanikiwa kwa Asilimia zote kusema hivyo ni kujidanganya wewe mwenyewe maana kuwa na tumaini sio Mkakati wa kukuhami na biashara yako.
2.Uamuzi wako wa kuanzisha biashara ni uamuzi uliouchukua wenye kukutaka wewe utumie wingi wa akili ili kuijenga biashara hiyo na hapoutahitaji kuwa na afya bora, fedha za kugharamia, familia yenye kuukunga mkono na kuwa na dhamiri ya kutaka kufanikisha.
3.Mambo pekee unayohitaji ili uweze kujenga biashara humilivu ni pamoja na;-
i)Tabia za mafanikio
ii)Muundo Bora wa biashara
iv)Utafiti wa sokov)Upatinaji wa mtaji
vi)Uundaji wa bidhaa unayotaka kuiuza.
vii) Uendeshaji wa kampuni
viii)Mauzo
ix)Ukuaji
Haya ndiyo tutakwenda kuhangalia kwa upana wake kwenye uchambuzi wa kitabu hiki.
[emoji3544]TAHADHARI[emoji3544]
Kuanzisha kampuni na biashara si kwa ajili ya watu wenye mioyo mepesi,weka akili jambo hilo.
Uchambuzi wa mambo yenye kukufanya Usife na biashara yako.
1.TABIA
Epuka kuwa na tabia zifuatazo ili kuwa na biashara humilivu na yenye kustawi kwa haraka na yenye mafanikio makubwa.
Moja;-Kuwa na tabia ya kutokuanza jambo /Biashara
Huwezi kushindambio bila ya kuanza kukimbia,usiruhusu biashara yako ifie kichwani mwako bila ya kuanza jitahidi vuta pumzi anza,kimbia.
Kamwe usijipatie sababu na visingizio vya wewe kutokuanza wengine hujipa visingizio vya umri ya kwamba umri wao ni mdogo ama mkubwa.
Uchunguzi unaonesha yakuwa kuna watu walianzisha ujasiriamali wao katika umri waliokuwa nao walipopata hamasa ya kuanza na kuanzisha.
Elon Musk alianza akiwa na miaka 24
Bill gate alianza akiwa na miaka 21
Steve Jobs alianza ana miaka 21
Mark Zuckerberg alianza na miaka 19
Mark Pincus alianzana miaka 41
Evan Williaum alianzisha Twitter akiwa na 34
Kanali Harland David Sanders Alianzisha akiwa na miaka 62
Wewe unagonja nini kuanza anza weka uoga pembeni na anza.
Mbili;- Epuka tabia ya kujiona na kujihisi u mjinga /Hautoshe.
Ukiwa na kujiona ya kuwa huna vigezona hutoshei kuanzisha jambo hapo utakuwa unasumbuliwa na tabia ya kujiona na kujihisi u mjinga (Imposter Syndrome)na hii hukufanya uanze kujiaminisha ya kuwa wewe huwezi na moja kwa moja utaishia na kutokujiweza.
Ili kushinda tabia hii
✓Jisemee ya kuwa unaweza
✓Chukua hatuakwa udogo
✓Sherekea ushindi wa nyuma
✓Andika uliyowahi fanikisha
✓Andika uimara wako
✓Andika udhaifu wako
Kisha anza.
Tatu;- Tabia ya kutaka kufanya tu unachopenda kukifanya basi.
Pana ukweli kuwa ni muhimu kufuata shauku zako (Ur Passion) lakini maisha ya biashara yenyemafanikio haitoshei tu kufanya unachokipenda wahitaji kwenda zaidi ya hapo. Palilia kulipenda unalolifanya hata kama halikuwa sehemu ya yale unayoyapenda sana maana si kila unachokipenda wewe kinaweza kuwa biashara.
Nne;- Tabia ya kutaka kufanya mambo mengi mengi kwa wakatimmoja (Plate Spinning).
Epuka tabia hii ya kutawanya nguvu zako kwa mambo mengi mengi yasiyo kuwa na tija za moja kwa moja na biashara yako kwa mfano unaanzisha biashara haijakomaa hata umeanza kusoma PhD , huku unaendelea kusoma umeamua kuoa wakati unamaliza kuoa unakwendahoneymoon saa ngapi utatimiza Jambo la maana lenye tija. Ondoa hali hiyo itazamisha biashara yako na wewe.
Tano;-Kutaka kufanya mambo yote wewe.
Jambo hili linaongeza hatari zaidi ya biashara yako kufa kwakua kuna maeneo utakuwa huna uwezo na hivyo wahitaji watu wengine wenyeuwezo nayo using'ang'anie.
Badili tabia hizo na eneo la tabia kwenye biashara yako utaanza kuliweka kwa uzuri.
2.MUUNDO WA BIASHARA.
Usijaribu kumfundisha nguluwe namba ya kuimba utakuwa unapoteza muda wako tu na utamkera nguluwe. Kuwa na muundo mbovu wa biashara ni sawa nakumfundisha nguluwe kuimba. Kuwa na wazo Bora na ukakosea namna bora ya kuingiza mapato , mpango wa kupata wateja na kuwa na mpango wa kuwalinda itakuwa kazi bure kuendesha biashara ya namna hiyo.
Kuwa na mpango bora wa biashara kuna faida kuliko kutokuwa nao kabisa.Tumia mfumohuu rahisi wa kuandika mpango wa biashara kwa kutumia mifumo wa Business Canvas ulio undwa na akina Alexander Osterwalder ukiwa na mtiririko huu ukiwa unatengeneza mpango wa biashara.
åWahusika wa biashara/Key partners.
ii)Shughuli rasmi za kufanywa/Key activities.iii) Rasilimali/Resource
iv)Thamani pendekezwa/Value Propositions
v)Kipengere cha wateja/Customer Segment
vi) Uhusiano wa wateja/Customer Relationship
vii)Namna ya kufikia wateja/Channels
viii) Gharama /Cost structure
ix)Mapato /Revenue StreamLa mwisho kwenye Muundo wa biashara hakikisha pia unaingia kwenye sekta bora inayokua kwa mfano tafiti zinaonesha kuwa asilimia 54% za kampuni zinazoanzishwa kwenye sekta ya Kilimo,mistu na uvuvi hufa. Na kwenye sekta ya majengo ya upangishaji kwa asilimia 41% hufa. Kwahiyo ingiakwenye sekta bora hata kama una ujinga mwingi utashinda kuliko kuingia kwenye sekta mbovu ukiwa na akili nyingi utaanguka tu.
Ili kuingia kwenye sekta bora angalia mambo haya matano muhimu;-
Moja;- Angalia takwimu za ukuaji
Mbili;-Angalia washindani wako
Tatu;-Angalia mwelekeowa soko /uwezo wa wateja wako wa kununua.
Nne;-Nguvu ya wasambazaji wako.
Tano;-Hatari za vipingamizi kwa maana ya masharti na vigezo vikiwa rahisi sana huwaruhusu wengi kufanya jambo hilo hivyo kupunguza faida.
Chagua kwa usahihi sekta ya kuingia wewe na wekea muundo Bora wabiashara.
3.UTAFITI WA SOKO.
Kwenye mchakato wa utafiti wa soko unapaswa kujiuliza maswali ya nani watakuwa wateja wangu, Nani washindani wangu, Upi uimara na udhaifu wa washindani wangu na mwisho epuka kufanya mambo haya wakati ukiwa kwenye utafiti wa soko;-
Mosi;- Kuigakila kitu kutoka kwa wengine.
Mbili;- Kutokukata Kuiga kabisa yale bora.
Tatu;-Kutokugeuza udhaifu wako kuwa nguvu.
Nne;-Kutokuamini ya kuwa mteja ndiye Boss wa maboss wote na kwamba aweza kufuta kazi watu wote kwenye biashara.
Tano;-Kutokuwa na bidhaa ya mfano na kuwa nawazo tu kichwani.
Sita;-Kutaka sana kuwa na takwimu zote za mambo ndipo uanze ama uingie sokoni.
Saba;- Kudanganya kwa kughushi /kutokufuata taratibu za kisheria kuhalalisha biashara au kampuni yako.
Yaepuke mambo hayo ukiwa kwenye mchakato wa utafiti wa biashara yako.4.KUPATA MTAJI WA BIASHARA.
Biashara nyingi hufa kwasababu ya ;-
✓•Kwenda kinyume na matumizi ya fedha za mtaji
✓•Kutokuwa na fedha za kutosha za mtaji
✓•Kutokuwa na uwekezaji wa kutosha
✓•Kushindwa kukusanya mtaji
✓•Bidhaa isiyofaa kwa sokoKushinda tatizo la mtaji usikaze sana kupata mtaji wa biashara badala ya kukazana na kufahamu soko linataka nini na linaweza kulipia kitu gani na usipange kupata fedha nyingi ndipo uanze anza na kidogo lijaribu soko na kisha endelea kukuza mtaji siku hadi siku na waweza tumianjia za;-
✓•Kundunduliza
✓•Kupata mtaji jumuia yaani Crowd Funding
✓•Wawekezaji malaika
✓•Tumia akiba zako
✓•Uza sehemu ya hisa
✓•Punguza matumizi yako
✓•Pata kazi ya pembeni
Mwisho unapoomba mtaji wa kifedha usiombe kama omba omba Bali omba kama mfalme kwakuwaambia wawekezaji utakavyokwenda kutengenezea fedha zaidi. Pangia na hakikisha unazungumza na wawekezaji zaidi ya 20 mpaka 50.
Maonyo ya kuzingatia unapotumia fedha za mtaji ama kuomba mtaji;-
Moja:-Weka BAJETI zako vizuri
Mbili;-Fahamu kwa bayana Nani kawekeza nini naatapata nini ama fedha zake zimetengeneza faida kiasi gani.
Tatu;-Epuka kugawa madaraka na mamlaka yote kwa wawekezaji kwenye mgawanyo wa hisa walau gawa kwa asilimia hizi Asilimia 33% wape wawekezaji, Asilimia 25% kwa mwanzilishi mwenza /Wafanyakazi, Asilimia 42% wewemwanzilishi mwisho vumilia mpaka hisa za kampuni zizae matunda ya jasho na uvumilivu wako.
Nne;-Tafuta na ajiri mtaalamu wa uhasibu ni uamuzi mbaya kama huna ufahamu wa mambo ya kifedha umeshikilia nafasi hiyo ajiri mtaalamu wa fedha akuundie muundo wa kifedha na anaweza kuwawa muda na si mwajiriwa wa kudumu awe Chief Financial Officer CFO wako.
Tano;-Usipuuze kutokupata faida mapema /anza kupata faida mapema. Kwakua faida kwenye biashara ni ya muhimu.
Sita;- Usitake kupata mtaji mwingi kupita kiasi waweza kuwa anguko lako.
5.KUUNDA BIDHAA.Akili kwako weka wazo la kwamba kuunda bidhaa ni kama kuchora mchoro ya kwamba mpaka uwe na mchoro bora unapaswa kupitia mchakato wa kuchora michoro mingi na mwisho utapata mchoro bora. Kisha kuipeleka biadhaa hiyo kwa wateja kwa lengo ya kuijaribu na wateja wakupe mrejesho wamaeneo ya kuboresha na wewe uyaboreshe.
6.KUONGOZA KAMPUNI YENYE MAFANIKIO.
Kuwa na timu Bora ya watu wako kwenye biashara ndiyo msingi wa Kwanza wa kuwa na uongozaji wa kampuni bora.Hakikisha timu ya watu wako inakuwa na mchanganyiko wa watu wazoefu hawa wengi huwa wazee ambaokuwa nao huwa pana gharama na vijana wenye damu changa na wasio na majukumu makubwa ya kimaisha ukiwa na timu ya aina hii ni kuwa na Timu ya Kijani (Green Team).
Masharti na maonyo ya kuzingatia unapoongoza kampuni yako;-
i. Hakikisha kila mtu anafanya kulielekea lengo na maonoya kampuni na si vinginevyo.
ii.Ainisha majukumu ya kila mmoja na wapatie kila mmoja kwa usahihi.
iii.Wapatie majukumu na waruhusu kukosea kwenye kukosea pana kujifunza.
iv.Itengenezee mazingira timu yako kufanya kazi kwa juhudi kwakua hakuna mafanikio bila juhudi.v.Jenga nguvu ya mashirikiano kwa kila kitengo.
vi.Zungumza lengo na maono ya kampuni mara kwa mara bila kuchoka.
vii.Furahia na timu yako panapokuwepo ushindi usichukue wewe sifa peke yako.
viii.Nyumbulika kwa kila Hali inapojitokeza ikitaka kunyumbulika.
ix.Usiache kuwa namwanzilishi mwenza badala ya kuwa pekee yako na mwanzilishi mwenza awe na sifa za;-
✓•Azibe sehemu ya udhaifu wako ulionao
✓•Afahamu majukumu yake
✓•Jichanganye na watu ili umpate aliye sahihi
✓• Unamfahamu vilivyo.
x.Usichelewe sana kuajiri ama kuwahi sana kuajiri.xi.Usiogope kumfuta kazi mtu na ukitaka kumfuta kazi mtu ziwepo sababu mbili muhimu;- moja;- sababu ni kuwa sio mtu sahihi mbili;- Huwezi gharama zake.
xii.Weka mpango wa kuwajibika kila mmoja.
xiii.Usipangie kuwa CEO wa kudumu bali jifute kazi pale mambo ya kampuniyanapokwenda vizuri mwachie mwingine maana si wakati wote wewe unaweza kuwa bora.
Fanyia kazi mambo hayo na utaingoza kampuni yako kwa ustawi.
7.MAUZO
Ukiona mambo yanakwenda vizuri kwenye kampuni Fahamu ya kuwa kitengo cha mauzo ya kampuni kipo kazini na kinafanya kazi nzurina ya kupendeza. Kama hauna kitengo cha mauzo hakikisha unakuwa nacho kitengo cha mauzo.
Mambo yanayosababisha kupunguza mauzo;-
i.Kutokuwa na kitengo cha mauzo.
ii.Kutokuwa na mafunzo ya mauzo/wafundishe watu wako.
iii.Kutokuwa na mfumo bora wa mauzo.
iv.Kukosa bidhaa mbadalaya kuuza wakati ambapo bidhaa mama sio muda wake wa mauzo.
v.Kukosa upimaji wa mauzo.
vi.Kufanya mauzo kwa wateja wasio sahihi na kutokuuza kinachohitajiwa.
vii.Kupangia bei vibaya.
viii.Kuahidi kupita kiasi na kutimiza kwa udogo.Kuangalie kwa jicho la wivu kitengo chako cha mauzo na utakuwa na kampuni himilivu.
8.KUKUZA KAMPUNI.
Kukuza kampuni kunataka sana ujifahamu namna ya wewe kujiongoza kila siku iendayo kwa Mungu wakati ukitimiza majukumu yako ya kila siku.
CEO unawajibika kujiamini, kujali afyayako ya akili, kupokea mawazo mapya, kujiafanyia tathimini ya ukuaji mara kwa mara, Kutokukata tamaa , kuwa na mpango B pale mpango A unaposhindwa, na kujiuliza maswali ya je hiki ninachofanya ni maamuzi sahihi au lah ? Hii inakusaidia kupunguza kufanya maamuzi mabayayanayoweza kukugharimu.
Mwisho hakikisha pia unafahamu wakati wa kuachana na hicho unachokifanya kama hakitoi matokeo unayolenga na kuyahitaji, wapo CEO wengi ambao wanaendelea kufanya kisicho leta mabadiliko kwakua tu wana msemo akilini mwao ya kwamba “Don't quit”, ama ule wa“Winners don't Quit”
Ukiyamanya mambo hayo kwa utuo na kwa kujifunza mara kwa mara kwa hakika utakuwa na msingi wa kuendesha kampuni na biashara himilivu na yenye kushinda vikwazo vingi.
Kila la kheri ndugu CEO.