Kujifariji sana ni tatizo, utajifariji mpaka uongo

Kujifariji sana ni tatizo, utajifariji mpaka uongo

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
WATU WANAOJIFARIJI SANA WANA HATARI YA KUBAKI WALIPO MAISHA YOTE.

#Wale ambao kila kitu ni mpango wa Mungu hata kama ni uzembeo wao.
#Wale ambao wanajipa matumaini ya kufanikiwa ilihali hawana juhudi zozote
#Wale ambao wanajidanganya uongo wenye matumaini na kukwepa ukweli wenye uhalisia
# Wale ambao wapo radhi wadanganywe kuliko kuupokea ukweli.

UKIJIONA NI MTU WA KUJIFARIJI SANA JUA KUNA UKWELI UNAUKWEPA

Kuna ukweli huutaki kuusikia na ambao ungekupa hatua mpya ndio maana kila kitu unasema nj mpango wa Mungu ilihali mengine ni matokeo ya uzembe wako tu sasa kwa sababu hutaki kukubali kuwa wewe ni MZEMBE basi unaendelea kujifariji kuwa hata hayo yametokea kwa mpango wa Mungu.


JIAMBIE UKWELI TU


Jiambie kuwa kuna sehemu unakosea kisha badili namna ya ufanyaji ili upate matokeo tofauti la sivyo utaendelea kujifariji mpaka uzeeni na matokeo yanabaki kuwa yale yale.

Mwanasayansi Saul kalivubha


Mitandaoni
#fikia ndoto zako
 
Kuna umri fulani ukifika unajua kabisa huwezi kubadilisha mambo inabidi tu kujifariji

1000011128.jpg
 
Back
Top Bottom