Kujifukiza ni kinga au ni tiba?

Kujifukiza ni kinga au ni tiba?

Sijijui

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
7,877
Reaction score
8,804
Wanajamvi, ninafahamu humu jamvini Kuna magwiji wa kila idara from miti shamba hadi PhD za MD.

Hivi kujifukiza ni kinga au ni tiba ya corona? Najua watanzania kutokana na umasikini wetu wa kipato na akili tunapenda sana mteremuko.

Hapa Tanzania ni kawaida sana kumsikia abiria akimpigia kelele dereva wa Basi apunguze mwendo wakati kuvunga tu mkanda kumemshinda, same applies to corona, kila Kona sasa ni kujifukiza kujifukiza, wengine wanatuambia tujifukize usiku na mchana na yawezekana kabisa tukaacha kuchukua tahadhari kisafukizia, je kujifukiza ni kinga ya corona au ni tiba?

Je kujifukiza huku kila siku unagombania daladala na mwendokasi au kila siku upo Kariakoo kupiga kazi haiwezi kuwa gharama kubwa kuliko kushinda nyumbani? Watu wa economic benefits analysis nisaidie pia katika hili. Je kweli mvuke unatoka kwenye maji yenye centigrade Mia moja hayawezi kusababisha chemical changes kwenye sura zetu?

Mwisho.
Je kujifukiza kwa mitishamba kumekuja baada ya Mungu kuonekana ameshindwa au ni back up?
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza hivi huo mvuke unaua virusi vya corona vilivyokwisha ingia viko kwenye mapafu tayari, au vilivyo usoni au kwenye koo au usoni, siajelewa kwa kweli!!
 
Kujifukiza ni kinga, kwa mategemeo kwamba kirusi bado kipo katika maeneo ya ndani ya pua, kikikumbana na mvuke ni lazima kife.

Kama kimeshatoka maeneo ya pua na kushuka kuelekea kwenye mapafu kufukizia hakuna faida yoyote.
 
Kujifukiza ni kinga, kwa mategemea kwamba kirusi bado kipo katika maeneo ya ndani ya pua, kikikumbana na mvuke ni lazima kife.

Kama kimeshatoka maeneo ya pua na kushuka kuelekea kwenye mapafu kufukizia hakuna faida yoyote.
Toa mechanism ipi inaweza kuua kirusi kwa kutumia mvuke, yaani fafanua vizuri kama mtaalamu
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza hivi huo mvuke unaua virusi vya corona vilivyokwisha ingia viko kwenye mapafu tayari, au vilivyo usoni,au kwenye koo,au usoni, siajelewa kwakeli!!
Maana yake hujaanza kujifukizia
 
Kujifukiza ni kinga, kwa mategemea kwamba kirusi bado kipo katika maeneo ya ndani ya pua, kikikumbana na mvuke ni lazima kife.

Kama kimeshatoka maeneo ya pua na kushuka kuelekea kwenye mapafu kufukizia hakuna faida yoyote.
Asante mkuu.sasa kutoka kwenye maeneo ya pua hadi kwenye mapafu kinatumia siku ngapi toka siku ulipokipata?
 
Toa mechanism ipi inaweza kuua kirusi kwa kutumia mvuke , yaaani fafanua vizuri Kama mtaalamu
Wataalam wapo mahospitalini wakitibu watu. Mvuke unaua virusi, joto kali linaua virusi. Kuna viwango vya joto vikifikiwa hakuna virus mwenye kuweza kuendelea kuwa hai.
 
Siku nne au tano kinaweza kuwa maeneo ya puani, baada ya hapo ndio kinashuka mapafuni.
Oooh kumbe tujifukize aise,sasa gharama za kuchemsha maji every day maana yake si mkaa wa book tatu kila siku au umeme wa kutosha?
 
Wataalam wapo mahospitalini wakitibu watu. Mvuke unaua virusi, joto kali linaua virusi. Kuna viwango vya joto vikifikiwa hakuna virus mwenye kuweza kuendelea kuwa hai.
Nyuzi joto Mia hakuna anayeweza himili, otherwise tusingekuwa tunapoza chai na maji ya kuoga
 
Back
Top Bottom