Sijijui,
Kuna video moja ya TV moja India mtangazaji anahojiana na Professor ambaye ni Daktari wa magonjwa ya binadamu ni bingwa wa tafiti mbalimbali. Kifupi ametoa mawazo yake nikalinganisha na kauli za Mh Rais nikaona kuna mantiki.
Yeye anasema virus wakishangilia mwilini kuna dalili kama uchovu kuishiwa nguvu utajisikia, kisha mwili uta detect kwamba kuna stranger hivyo utafanya attack kwa kupandisha joto la mwili l.
Anasema ukishajisikia joto la mwili liko juu unachotakiwa kufanya CHEMSHA MAJI WEKA KWENYE CHUPA YA CHAI HALAFU KILA BAADA YA MUDA FULANI KUNYWA YALE MAJI YAKIWA YA MOTO HADI UHAKIKISHE UNATOA JASHO LA KUTOSHA FANYA HIVYO MARA KWA MARA KWA SIKU MBILI MFULULIZO. Anasema kufanya hivyo linapandisha joto la mwili hivyo kuvunja vunja virus mwilini mwako kwani joto la mwili likipanda kwa degree celsius 1°c ni joto tosha kuharibu virus.
Linganisha mantiki ya Mh Rais na huyu Mtabibu toka India.