Culture Me
JF-Expert Member
- May 24, 2017
- 10,490
- 21,398
Wanajamvi, ninafahamu humu jamvini Kuna magwiji wa kila idara from miti shamba hadi PhD za MD.
Hivi kujifukiza ni kinga au ni tiba ya corona? Najua watanzania kutokana na umasikini wetu wa kipato na akili tunapenda sana mteremuko.
Hapa Tanzania ni kawaida sana kumsikia abiria akimpigia kelele dereva wa Basi apunguze mwendo wakati kuvunga tu mkanda kumemshinda, same applies to corona, kila Kona sasa ni kujifukiza kujifukiza, wengine wanatuambia tujifukize usiku na mchana na yawezekana kabisa tukaacha kuchukua tahadhari kisafukizia, je kujifukiza ni kinga ya corona au ni tiba?
Je kujifukiza huku kila siku unagombania daladala na mwendokasi au kila siku upo Kariakoo kupiga kazi haiwezi kuwa gharama kubwa kuliko kushinda nyumbani? Watu wa economic benefits analysis nisaidie pia katika hili. Je kweli mvuke unatoka kwenye maji yenye centigrade Mia moja hayawezi kusababisha chemical changes kwenye sura zetu?
Mwisho.
Je kujifukiza kwa mitishamba kumekuja baada ya Mungu kuonekana ameshindwa au ni back up?
Sijijui,
Kuna video moja ya TV moja India mtangazaji anahojiana na Professor ambaye ni Daktari wa magonjwa ya binadamu ni bingwa wa tafiti mbalimbali. Kifupi ametoa mawazo yake nikalinganisha na kauli za Mh Rais nikaona kuna mantiki.
Yeye anasema virus wakishangilia mwilini kuna dalili kama uchovu kuishiwa nguvu utajisikia, kisha mwili uta detect kwamba kuna stranger hivyo utafanya attack kwa kupandisha joto la mwili l.
Anasema ukishajisikia joto la mwili liko juu unachotakiwa kufanya CHEMSHA MAJI WEKA KWENYE CHUPA YA CHAI HALAFU KILA BAADA YA MUDA FULANI KUNYWA YALE MAJI YAKIWA YA MOTO HADI UHAKIKISHE UNATOA JASHO LA KUTOSHA FANYA HIVYO MARA KWA MARA KWA SIKU MBILI MFULULIZO. Anasema kufanya hivyo linapandisha joto la mwili hivyo kuvunja vunja virus mwilini mwako kwani joto la mwili likipanda kwa degree celsius 1°c ni joto tosha kuharibu virus.
Linganisha mantiki ya Mh Rais na huyu Mtabibu toka India.
Kujifukiza ni tiba au kinga?Hii ni mbinu mbadala ya kujifukizia
View attachment 1429209
😀😆😀Huyo mwenyewe aliesema hivo, amehama mjengoni" analala juu ya mawe!
Mbona hajatulia tu mjengoni na aendelee kujifukiza!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiondoka jichemshe, ukirudi jichemshe. Hakuna haja ya kufunika sura mkuu.Kwa hiyo ukishajifukizia asubuhi unaendavtu kwenye mishe bila shida na wala huhitaji mask na kunawa nawa kwa kuwa unakinga tayari.
Sasa huyu mwanasayansi wetu ujasiri wa kutuambia Mambo ya kujifukizia kwa nafasi yake ameupata wapi?Mkuu, hakuna uthibitisho wa kisayansi kuwa hizi steam inhalation therapy kwamba ni tiba au kinga ya COVID-19.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka niungue ee?Ukiondoka jichemshe, ukirudi jichemshe. Hakuna haja ya kufunika sura mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Chagua 1 kati ya haya ma2. Kufa kwa corona au kujitibu corona kwa kujifukiza.Unataka niungue ee?