Kujiita wa mjini halafu huna vitu hivi au moja ya hivi vitu ni dalili ya ubwege

Kujiita wa mjini halafu huna vitu hivi au moja ya hivi vitu ni dalili ya ubwege

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Ni fahari kuzaliwa mjini na kuwa mtu wa mjini kama una yale yanayopatikana mjini.

Mfano, mjini kuna karibu huduma zote za kijamii mathalani shule, vyuo, na miundombinu yote muhimu ya wewe kuipata elimu.

Sasa itashangaza umezaliwa mjini, umekulia mjini, halafu ati usiwe na elimu. Halafu kutwa kuchwa kutambia wajinga wenzako kuwa wewe ni mtu wa mjini. Unajichoresha kwa Watu lakini wewe hilo hulijui.

Umezaliwa mjini kwenye fursa nyingi sana lakini huna kazi wanakuja wale wa vijijini wanakupiku wanakuajiri wewe unakalia mimi born town, unajichoresha. Ni kwamba upeo wako mdogo.

Umezaliwa mjini, kuna vyombo vya habari na upatikanaji wa elimu ya kijamii na kiraia lakini unaúlizwa mambo madogo ya nchi au kijamii unajiumauma. Huna unalojua la maana zaidi ya vitu vya kitoto toto. Upeo mdogo, unatambia Watu kuzaliwa mjini Watu wanakuchora tuu.

Wewe ni mtoto wa mjini lakini unamawazo ya kichawi na kishirkina. Yaani unaamini hakuna linalowezekana bila uchawi au ushirikina. Kitu kidogo unaenda kwa waganga. Hivi uliona Watu wa mjini wakawa na mawazo ya namna hiyo. Vijijini huko ndio Watu huwaza kwa namna hiyo.
Watu wanakuchora tuu.

Mwili wa mjini akili ya shamba. Sasa umezaliwa mjini alafu unaamini katika uwezo wa uganga na ushirikina. Hivi ungezaliwa kijijini si ndio ungekuwa mchawi au mganga mwenyewe. Watu wanakuchora.

Sifa moja ya wapo ya Watu wa mjini hasa majiji makubwa kimataifa ni kutoamini mambo ya kishirikina na kichawi. Ukiona bado upo kwenye jamii inayoamini mambo hayo kwa wingi ujue hicho ni kijiji tuu.

Umezaliwa mjini lakini unamawazo ya ukabila. Wewe kila kitu kuulizia ukabila. Watu wanakuchora tuu.

Unatamba wewe ni Born town lakini unatumia Jiko la mkaa na kuni. Hauna mashine na majiko ya kurahisisha maisha bado unatamba wewe ni WAMJINI. Unajichoresha. Kama upo mjini na bado unatumia Jiko la kuni vipi ungekuwa kijijini

Wewe ni Born town lakini hata kutumia kompyuta au kutumia mitandao ya kijamii, sijui mambo ya email hujui. Bado unajiita mtu wa mjini. Watu wanakuchora. Kazi kupiga piga kelele.

Unajiita born town lakini hujui hata lugha moja nyingi ya kimataifa ili kuwasiliana na dunia. Hivi unajua maana ya mjini. Born town ni lazima ajue lugha hata moja ya kimataifa kuachana na ile ya taifa lake. Watu wanakuchora.

Unatamba wewe ni Born town alafu hata huna mpango wa kwenda hata nchi jirani, huna hata passport. Ajabu hata kitambulisho cha taifa hauna. Hivi neno mjini unalichukuliaje? Watu wanakuchora tuu.

Kifupi wewe ni Bwege tuu. Upeo mdogo unakufanya usumbue mabwege wenzako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ni kama Machadema yaani wanaemtegemea kwenye propaganda hajua kwamba TRA ni ya Muungano anaanza kushangaa Kamishna wa ZRA kuteuliwa Kamishna wa TRA 😃😃

Mabwege ni wengi sana upande ule.
 
Umjini ni ujinga mwingi, ukitaka kuna kwa utafiti kidogo tu, angalia hata maraisi waliomtangulia huyu wa Sasa, wote ni kutoka vijijini. Fursa za mjini ni mbanano tuu na mbwembwe nyingi.
 
Ni kama Machadema yaani wanaemtegemea kwenye propaganda hajua kwmaba TRA ni ya Muungano anaanza kushangaa Kamishna wa ZRA kuteuliwa Kamishna wa TRA 😃😃

Mabwege ni wengi sana upande ule.
Ukizaliwa mjini halafu unakuwa na mawazo mgando ya kijima kila mda kuiwaza Chadema na kushabikia ccm ya wachawi wewe huna tofauti na Zinjanthropus
 
Waliotoboa maisha wengi machimbuko yao ni vijijini.
 
Umeniwezea kwenye passport tu ndo Sina vingine kote Nina vigezo vya kuwa born town
 
Hiyo ni misemo tuu.

Huku mtaani mambo ni tofauti kabisa.
Sio ajabu kuna kijana yupo kijijini na hajawahi kufika mjini lakini ni Mjanja kuliko vijana wengi wa Mjini
Ni hivi mkuu, unaweza ukamtoa mtu kijijini lakini ukashindwa kutoa kijiji ndani ya kichwa chake.

Exposure and accumulated experience ndiyo kila kitu kwenye maisha.

Ni kweli, kukaa mjini siyo guarantee ya kufanikiwa ila, mtu wa mjini ni wa-mjini ata akiwa hana hela
 
Ni hivi mkuu, unaweza ukamtoa mtu kijijini lakini ukashindwa kutoa kijiji ndani ya kichwa chake.

Exposure and accumulated experience ndiyo kila kitu kwenye maisha.

Ni kweli, kukaa mjini siyo guarantee ya kufanikiwa ila, mtu wa mjini ni wa-mjini ata akiwa hana hela

Lakini wapo Watu wengi wamezaliwa mjini na hawajawahi kuishi wala kufika kijijini lakini wana mambo ya kijijini. Na hawa hapa mjiji ni wengi mno

Na wapo waliozaliwa kijijini na hawajawahi kufika mjini na wanamambo ya mjini. Hawa unawazungumziaje
 
Kwenye msafara wa mamba pia kenge wapo

Na ñdio hao wanaowanyanyasa wengine ilhali wao hawana tofauti yoyote na hao wa kijijini.

Ni sawa na wale wanaotamba nimesoma UDSM wakati na kunyanyasa waliosoma vyuo vingine. Wengi wa hivyo kichwani wana bar ndogo.
 
Back
Top Bottom