Kujiita wa mjini halafu huna vitu hivi au moja ya hivi vitu ni dalili ya ubwege

Kujiita wa mjini halafu huna vitu hivi au moja ya hivi vitu ni dalili ya ubwege

Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Ni fahari kuzaliwa mjini na kuwa mtu wa mjini kama una yale yanayopatikana mjini.

Mfano, mjini kuna karibu huduma zote za kijamii mathalani shule, vyuo, na miundombinu yote muhimu ya wewe kuipata elimu.

Sasa itashangaza umezaliwa mjini, umekulia mjini, halafu ati usiwe na elimu. Halafu kutwa kuchwa kutambia wajinga wenzako kuwa wewe ni mtu wa mjini. Unajichoresha kwa Watu lakini wewe hilo hulijui.

Umezaliwa mjini kwenye fursa nyingi sana lakini huna kazi wanakuja wale wa vijijini wanakupiku wanakuajiri wewe unakalia mimi born town, unajichoresha. Ni kwamba upeo wako mdogo.

Umezaliwa mjini, kuna vyombo vya habari na upatikanaji wa elimu ya kijamii na kiraia lakini unaúlizwa mambo madogo ya nchi au kijamii unajiumauma. Huna unalojua la maana zaidi ya vitu vya kitoto toto. Upeo mdogo, unatambia Watu kuzaliwa mjini Watu wanakuchora tuu.

Wewe ni mtoto wa mjini lakini unamawazo ya kichawi na kishirkina. Yaani unaamini hakuna linalowezekana bila uchawi au ushirikina. Kitu kidogo unaenda kwa waganga. Hivi uliona Watu wa mjini wakawa na mawazo ya namna hiyo. Vijijini huko ndio Watu huwaza kwa namna hiyo.
Watu wanakuchora tuu.

Mwili wa mjini akili ya shamba. Sasa umezaliwa mjini alafu unaamini katika uwezo wa uganga na ushirikina. Hivi ungezaliwa kijijini si ndio ungekuwa mchawi au mganga mwenyewe. Watu wanakuchora.

Sifa moja ya wapo ya Watu wa mjini hasa majiji makubwa kimataifa ni kutoamini mambo ya kishirikina na kichawi. Ukiona bado upo kwenye jamii inayoamini mambo hayo kwa wingi ujue hicho ni kijiji tuu.

Umezaliwa mjini lakini unamawazo ya ukabila. Wewe kila kitu kuulizia ukabila. Watu wanakuchora tuu.

Unatamba wewe ni Born town lakini unatumia Jiko la mkaa na kuni. Hauna mashine na majiko ya kurahisisha maisha bado unatamba wewe ni WAMJINI. Unajichoresha. Kama upo mjini na bado unatumia Jiko la kuni vipi ungekuwa kijijini

Wewe ni Born town lakini hata kutumia kompyuta au kutumia mitandao ya kijamii, sijui mambo ya email hujui. Bado unajiita mtu wa mjini. Watu wanakuchora. Kazi kupiga piga kelele.

Unajiita born town lakini hujui hata lugha moja nyingi ya kimataifa ili kuwasiliana na dunia. Hivi unajua maana ya mjini. Born town ni lazima ajue lugha hata moja ya kimataifa kuachana na ile ya taifa lake. Watu wanakuchora.

Unatamba wewe ni Born town alafu hata huna mpango wa kwenda hata nchi jirani, huna hata passport. Ajabu hata kitambulisho cha taifa hauna. Hivi neno mjini unalichukuliaje? Watu wanakuchora tuu.

Kifupi wewe ni Bwege tuu. Upeo mdogo unakufanya usumbue mabwege wenzako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umepiga mulemule
 
Born hia hia 😁😁

Hata hivyo kila mji una zone. Kuna mtu amezaliwa mwanza au arusha city centre na mwingine kazaliwa na kukulia Dar uswazini. Kwa hiyo usishangae mtu akatoka mkoa na kuingia kwenye system za mji kuliko yule aliyekuwepo miaka yote daslam kutokana na connections au lifestyle analoishi.

Kwa hiyo exposure hutokana na pahali unapokulia na jamii inayokuzunguka. Kwa hiyo Kama umezaliwa na kukulia sehemu ambazo ndugu zako hawana contacts za wanasiasa au wafanyabiashara wakubwa na wala hakuna majirani wenye ajira zinazoeleweka zaidi ya madeiwaka na walinzi wa kariakoo. Mkuu ni ngumu mno kufikia hizo standards za mjini ulizonazo kichwani
 
Na kwa nini watu ambao hawana standards za mjini ndio hupendelea kutamba nd kujigamba wao ni Born hiahia.
Je ni kutokujiamini?
 
Wanaojiita watoto wa mjini sahv wako tofauti kabisa... hata mentality zao pia
Wao kwenda kidimbwi, wavuvi kamp element ndy wanasema wao watoto wa mjini
Wakati wetu watoto wa mjini unawakuta salamanda au azam pale unakutana na mabosi mbalimbali wanawapa michakato
Mnapeana mambo yanasonga
Ndomana mwisho wa siku unakuta watu vichwa vimebeba mambo kibao baada ya kukutana na watu wa kila aina

Ova
 
Wanaojiita watoto wa mjini sahv wako tofauti kabisa...hata mentality zao pia
Wao kwenda kidimbwi,wavuvi kamp element ndy wanasema wao watoto wa mjini
Wakati wetu watoto wa mjini unawakuta salamanda au azam pale unakutana na mabosi mbalimbali wanawapa michakato
Mnapeana mambo yanasonga
Ndomana mwisho wa siku unakuta watu vichwa vimebeba mambo kibao baada ya kukutana na watu wa kila aina

Ova

Kizazi cha nyuma yetu 80's kurudi nyuma mtoto wa mjini ni WAMJINI kweli.
Kuanzia mipango ya kuzamia nchi zingine, masuala ya uchumi n.k
 
Kizazi cha nyuma yetu 80's kurudi nyuma mtoto wa mjini ni WAMJINI kweli.
Kuanzia mipango ya kuzamia nchi zingine, masuala ya uchumi n.k
Miaka ya nyuma enzi za kupiga simu kimazabe line zile za TTCL international call, wakati ule dili kweli, ahh tulipigisha sana watu.

Hawa matajiri wa kihindi sijui nani ambaye nilikuwa sijamuungisha.

Wao wanaongea UK na India Canada alafu ni michakato tu mwanzo mwisho.

Nilijuwana nao matajiri wengi sana kupitia line hiyo.

Kesho wewe ni kupitia tu pesa zako makwao 😄.

Nilikuja kamatwaga juu gorofani kitega uchumi nikapewaga kesi uhujumu uchumi ngoma mpaka Kisutu lakini nikaimaliza, sema huko nilichomwa na watoto wa Sinza nakumbuka 😄.

Ova.
 
Sio Poa Bro.
Kwa sasa vijana wengi ni waoga
 
Ikajagaa dili za viza enzi zile bandika bandua 😄
Aise maisha haya ngoja siku nkituliaa ntaandika bonge la uzi
Maana maisha kama sinema

Ova

Andika vijana wengi tujifunze.

Kwa sasa vijana kuongea tuu na Mhindi au muarabu au mzungu hawawezi. Hawajiamini.

Mbaya zaidi wanakasumba mbaya
 
Sisi wa shambani acha tubaki kusoma comments za waliozaliwa mijini
 
Andika vijana wengi tujifunze.

Kwa sasa vijana kuongea tuu na Mhindi au muarabu au mzungu hawawezi. Hawajiamini.

Mbaya zaidi wanakasumba mbaya
Wakat ule unawangunisha wahindi waonge International call
Aise matajiri, wana maviwanda nk
Ndio maana waliposikia nimepata matt ahh faster tu nilichomolewa
😄
Ila nlikuja juta sana kuwashirikisha wale watoto wa Sinza na wakati ule kesi uhujumu uchumi ulikuwa hauna nguvu sana, sema tu kesi ni kesi

Ova
 
Back
Top Bottom