Kujiita wa mjini halafu huna vitu hivi au moja ya hivi vitu ni dalili ya ubwege

Kujiita wa mjini halafu huna vitu hivi au moja ya hivi vitu ni dalili ya ubwege

Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Ni fahari kuzaliwa mjini na kuwa mtu wa mjini kama una yale yanayopatikana mjini.

Mfano, mjini kuna karibu huduma zote za kijamii mathalani shule, vyuo, na miundombinu yote muhimu ya wewe kuipata elimu.

Sasa itashangaza umezaliwa mjini, umekulia mjini, halafu ati usiwe na elimu. Halafu kutwa kuchwa kutambia wajinga wenzako kuwa wewe ni mtu wa mjini. Unajichoresha kwa Watu lakini wewe hilo hulijui.

Umezaliwa mjini kwenye fursa nyingi sana lakini huna kazi wanakuja wale wa vijijini wanakupiku wanakuajiri wewe unakalia mimi born town, unajichoresha. Ni kwamba upeo wako mdogo.

Umezaliwa mjini, kuna vyombo vya habari na upatikanaji wa elimu ya kijamii na kiraia lakini unaúlizwa mambo madogo ya nchi au kijamii unajiumauma. Huna unalojua la maana zaidi ya vitu vya kitoto toto. Upeo mdogo, unatambia Watu kuzaliwa mjini Watu wanakuchora tuu.

Wewe ni mtoto wa mjini lakini unamawazo ya kichawi na kishirkina. Yaani unaamini hakuna linalowezekana bila uchawi au ushirikina. Kitu kidogo unaenda kwa waganga. Hivi uliona Watu wa mjini wakawa na mawazo ya namna hiyo. Vijijini huko ndio Watu huwaza kwa namna hiyo.
Watu wanakuchora tuu.

Mwili wa mjini akili ya shamba. Sasa umezaliwa mjini alafu unaamini katika uwezo wa uganga na ushirikina. Hivi ungezaliwa kijijini si ndio ungekuwa mchawi au mganga mwenyewe. Watu wanakuchora.

Sifa moja ya wapo ya Watu wa mjini hasa majiji makubwa kimataifa ni kutoamini mambo ya kishirikina na kichawi. Ukiona bado upo kwenye jamii inayoamini mambo hayo kwa wingi ujue hicho ni kijiji tuu.

Umezaliwa mjini lakini unamawazo ya ukabila. Wewe kila kitu kuulizia ukabila. Watu wanakuchora tuu.

Unatamba wewe ni Born town lakini unatumia Jiko la mkaa na kuni. Hauna mashine na majiko ya kurahisisha maisha bado unatamba wewe ni WAMJINI. Unajichoresha. Kama upo mjini na bado unatumia Jiko la kuni vipi ungekuwa kijijini

Wewe ni Born town lakini hata kutumia kompyuta au kutumia mitandao ya kijamii, sijui mambo ya email hujui. Bado unajiita mtu wa mjini. Watu wanakuchora. Kazi kupiga piga kelele.

Unajiita born town lakini hujui hata lugha moja nyingi ya kimataifa ili kuwasiliana na dunia. Hivi unajua maana ya mjini. Born town ni lazima ajue lugha hata moja ya kimataifa kuachana na ile ya taifa lake. Watu wanakuchora.

Unatamba wewe ni Born town alafu hata huna mpango wa kwenda hata nchi jirani, huna hata passport. Ajabu hata kitambulisho cha taifa hauna. Hivi neno mjini unalichukuliaje? Watu wanakuchora tuu.

Kifupi wewe ni Bwege tuu. Upeo mdogo unakufanya usumbue mabwege wenzako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
mkuu wa mjini tumekukosea nini
 
Ni kama Machadema yaani wanaemtegemea kwenye propaganda hajua kwamba TRA ni ya Muungano anaanza kushangaa Kamishna wa ZRA kuteuliwa Kamishna wa TRA 😃😃

Mabwege ni wengi sana upande ule.
TRA ni Ya Muungano Kwani Kuna Mtu hajui Huko??
Basi wnahitaji shule ya Katiba..

Swala namba 10..Kodi ya Mapato...
Screenshot_20240703_120858_Adobe Acrobat.jpg

Screenshot_20240703_120922_Adobe Acrobat.jpg
 
Wakuja mnahangaika kweli na watoto wa mjini. Tumejikuta tu jamani hatukupenda kuzaliwa mjini.
 
Na kwa nini watu ambao hawana standards za mjini ndio hupendelea kutamba nd kujigamba wao ni Born hiahia.
Je ni kutokujiamini?
Ipo hivyo kila sehemu kwa watu wanaotokea miji mikubwa. Kwetu ni Dar, kwa wakenya ni Nairobi, Nigeria ni Lagos, South Africa ina miji mingi ila watu wanaotokea Johannesburg ndio hujiona superior

Kuna namna mtu akitokea miji hiyo anaona anaishi kwenye sehemu kubwa na imeendelea kuliko wa sehemu nyingine ndio maana kuna ego wanakuwa nayo
 
Back
Top Bottom