#COVID19 Kujikinga na Maambukizi zaidi: Serikali walazimishe 'level seat'

#COVID19 Kujikinga na Maambukizi zaidi: Serikali walazimishe 'level seat'

Nyie nyote mnaoshabikia huu us.enge wa Corona ni watu mnaoishi kwa shemeji zenu na hamlipi hata Kodi ya nyumba/chumba. Hivi hiyo Corona unahitaji kumwambia mtu usibanane,vaa barakoa etc!??... Jibu ni kwamba Corona ipo zaidi mitandaoni, siku ikifika mtaani kila nyumba ikawa na msiba hutaona mtu akipanda daladala iliyojaa. Ila Corona mnaikuza kuliko uhalisia wake. Mlivyo WAPUMBAVU mpo mnasisitiza tu Mambo msiyojua athari zake. Petrol imetoka 2050 hadi 2400 na nauli ya Tegeta - Kariakoo bado ni 600 tu, je wakikaa level seat itakuwaje!??.. ndo maana nimesema mtoa mada ni mtu anayekaa kwa shemeji yake.
Mkuu,kama una daladala hebu wapunguzie hesabu walau kipindi hiki
 
Sasa level seat waliokaa jirani si bado wako jirani?

level seat haisaidii, ni kutengeneza mazingira magumu ya usafiri kwa wananchi.

Hizo nguvu za kuenforce level seat wazitumie kuenforce barakoa kwenye vyombo vya usafiri
 
Mkuu,kama una daladala hebu wapunguzie hesabu walau kipindi hiki
Kwasababu ya Corona!?.. Hivi umewahi kujiuliza kwanini hakuna kondakta anayechukua nauli katika basi la Mbagala Kariakoo linalojaa masaa yote bila barakoa wala sanitizer,anayekutana na abiria zaidi ya 1000 kwa siku.. Aliyefariki kwa Corona!?.. hii Corona ipo kwenye mitandao zaidi ya uhalisia. Umejiuliza kwanini baada ya video ya jeneza lenye manguo huko Uganda kushtukiwa kabla ya kuzika hakuna tena matangazo ya hatari kuhusu Corona Uganda!???... Mnaangamia kwa kukosa maarifa. Corona ipo lakini kwa kiwango cha chini sana, sio kama mnavyotuaminisha.
 
Maisha haya ni shida,jana mlikua mnapigania mruhusiwe mikutano ya hadhara mara mtaandaa maandamano ya kudai katiba. Leo hii mnataka level siti kisa kuna corona aiseee
 
Wala hakuna haja ya levo siti, watu wa daladala watapata hasara,
Inachotakiwa abiria wote wavae barakoa
Duuuh, mkuu unaelewaje juu ya afya kinga dhidi ya COVID-19? Kuvaa barakoa ni sehem ndogo Sana ya njia za kuzuia Ugonjwa huo. Social and individual distancing ndo kila kitu. Suala la level seat lina maana kubwa. Mikusanyiko mikubwa Kama Ziara za Mwenge na viongozi wa kiserikali, Bar , kumbi za sherehe na sehem zote zenye mikusanyiko mikubwa ya watu zinatakiwa kufungwa.

N.B Binafsi bado naunga mkono approach ya JPM aliyoitumia kukabiliana na Ugonjwa huo. Walau maisha yaliendelea. Juzi nimepita Kariakoo mtaa wa Kongo, aisee wale watu ukiwapiga Lockdown utazalisha kundi kubwa la vibaka. Otherwise walete Chanjo tule perdiems za semina na activities za Chanjo.
 
Back
Top Bottom