SoC02 Kujitegemea Vijana kiuchumi

SoC02 Kujitegemea Vijana kiuchumi

Stories of Change - 2022 Competition

Feivillahmwilafi10

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
1
Reaction score
7
KIJANA mwenye ndoto za kuwa na maisha bora huonekana kwa namna mbali mbali akijituma,kujishughulisha na kutumia mda wake mwingi kwa asilimia kubwa kuzalisha fedha ili aweze kutimiza malengo na mipango anayotamani kuwa nayo ili kuuoa moyo wake kile kitu unahitaji.(vijana wa namna hii huwa Ni msaada mkubwa katika jamii)

Hizi hapa Ni baadhi ya sifa za vijana wanaoukataa umaskini
  • Wanajali muda
  • Wanapenda kujifunza Mambo mapya
  • Huonekana bize muda mwingi
  • Hawaendekezi starehe muda mwingi
  • Muda mwingi huutumia katika Mambo ya KIUCHUMI.
1. Siyo watu wa makundi ya hivyo
2. Hupenda kusikiliz zaidi kuliko kuzungumza.
3. Hufanya kazi ya kuingiza pesa akiwa tayari matumizi ya hio pesa ameshayandaa.
4. Wana uwezo mkubwa wa kutatua changamoto katika utafutaji
5. HAWAKATI TAMAA wanaposhindwa..
6. Wanatoa sadaka .

MAMBO YANAYOWEZA KUMSAIDIA KIJANA KISAIKOLOJIA ILI AWEZE KUFANIKIWA KIUCHUMI
1. Kutokuchagua aina za kazi za kufanya​
2. Kujiamini na kuamini uwezo wake​
3. Kujipenda​
4. Kujituma​
5. Kujifunza kwa waliofanikiwa​
6. Kujiweka bize na Mambo ya msingi​
7. Kuepuka makundi mabaya​
8. Kuwa mtu wa ibada​
9. Kutafuta fursa za kiuchumi​

CHANGAMOTO ZA AJIRA TANZANIA
Kwa sasa katika nchi nyingi zinakabiliwa na uhaba wa ajira ikiwemo TANZANIA hivyo kijana wa kitanzania ambae amehitimu elimu yake ya kidato cha nne,sita,vyuo vya Kati na vyuo vikuu wanatakiwa watoe zana ya kuajiriwa na mbadala wake akili zao zipanuke zaidi na kufikilia kujiajiri ili waweze kuendesha na kuyamudu maisha yao ya kila siku.

Pia serikali na wadau wengine wa maendeleo waweke uwanda mpana zaidi kwa vijana ambao wana malengo ya kufanikiwa lakini wakwama mitaji kwa ajili ya kujiajiri wao wenyewe hivyo kuwawezeshesha vijana hawa mikopo yenye masharti nafuu . na pia serikali kuangalia namna ya kuwawekea mazingira nafuu kwa ajili ya kuwapa wepesi kuanza Safari ya kujiajiri Kama vile masuala ya Kodi na vibali serikali iwekee wepesi ili kuwarahisishia vijana hawa kujiajiri.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WENZANGU.
Mimi pia ni kijana nisie na ajira lakini nimejiajiri katika kilimo Cha nyanya nilianza Kama mfanyakazi wa mtu ili niweze kujipatia mtaji nilifanikiwa kwa misimu mitatu kufanya kazi huku nikijiwekea mwenyewe nachopata na sasa nimesimama mwenyewe.

USHAURI KWA VIJANA
Ushauri wangu kwa vijana wenzangu Ni kwamba tusiweke akilini mwetu Mambo ya vyeti tulivyonavyo tukaona hatupaswi kuwa vibarua na wafanyakazi kwa watu tuliowazidi elimu lakini KIUCHUMI wametutangulia tukumbuke mkono mtupu haulambwi .

Hivyo tujitoe kujiajiri ili tuweze kuajiri wengine na tutajenga nchi yenye vijana wenye uwezo mkubwa KIUCHUMI.
 
Upvote 8
Back
Top Bottom