Kujiuzulu kwa Ndugai: Hongereni CHADEMA na NCCR japo haikutosha

Kujiuzulu kwa Ndugai: Hongereni CHADEMA na NCCR japo haikutosha

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Amefurushwa Mh. Ndugai kiongozi wa mhimili kinyume cha katiba.

Katika hali ya kusikitisha, ni Chadema na NCCR pekee ndiyo angalau wamefahamika wanasimama wapi kwenye kadhia hii:

Bado hakuna matamko yoyote rasmi ya kupinga au hata kukemea vikali kabisa ukiukwaji mkubwa huu wa haki za Mh. Ndugai.

Pamoja na makosa yake mengine yoyote, kufurushwa kwa kutoa maoni yake:

"kumbe angeweza kufurushwa hata kwa kwenda kujisaidia tu?"

Wako wapi CUF, ACT, CHAUSTA, UMD, CHAUMA, DP, nk?

Nani alipaswa kuwaongoza wananchi kuukataa ukiukwaji mkubwa huu wa haki za msingi za watu?

Nchi zinaongozwa kwa mujibu wa katiba si kwa kununa, hasira, chuki, visasi nk.

Ndugai mnyongeni ila kutoa maoni ilikuwa haki yake.
___________

Angalizo: DP ya Mtikila isingeufumbia macho ukiukwaji huu wa haki za mtu.

Nini kimebadilika? DP si ingalipo?

Apumzike kwa amani Rev. Mtikila.
 
Katiba ya JMT imeeleza wazi uhuru wa muhimili wa bunge na madaraka ya spika ila tatizo Ndugai alishashiriki kuvunja nguvu ya bunge analoliongoza kwa kugeuka kibaraka wa muhimili mwingine ndio maana hata katiba imeshindwa kumlinda.
 
Makosa mawili hayafanyi moja kuwa halali.

"Yaliyomkuta kiongozi huyu wa mhimili kwa sababu ya kutoa maoni yake tu ni batili."

Ni hayo tu.
 
ACT Tanganyika ni wanufaika wa Maccm,
ACT Zanzibar wameshaahituka 2025 wanamwachia kiongozi mkuu wa chama ACT yake.
 
Km alivyomfurusha mh Lissu?
KARMA is always on time.

"Ndugai mnyongeni ila kutoa maoni ilikuwa haki yake."

Lissu shares these sentiments.

Wewe utaiongelea KARMA kumhusu Lissu kuliko Lissu mwenyewe?

Hii si ndiyo ya kumpenda mtoto wa mtu kuliko mama yake?

Hapo ukiitwa "fataki" itakuwa kukusingizia?
 
ACT Tanganyika ni wanufaika wa Maccm,
ACT Zanzibar wameshaahituka 2025 wanamwachia kiongozi mkuu wa chama ACT yake.

ACT na ZZK ni shida. Hata wahanga wa 2025 Pemba hawawakumbuki tena.

Kuna habari ZZK yuko kwenye mkeka mpya wa mama. Hivyo yuko kimkao wa kula zaidi.
 
"Ndugai mnyongeni ila kutoa maoni ilikuwa haki yake."

Lissu shares these sentiments.

Wewe utaiongelea KARMA kumhusu Lissu kuliko Lissu mwenyewe?

Hii si ndiyo ya kumpenda mtoto wa mtu kuliko mama yake?

Hapo ukiitwa "fataki" itakuwa kukusingizia?
Ndungai & the gang ndio muasisi/waasisi wa uminywaji wa uhuru wa kutoa maoni ....rooster are coming home to roost.
 
We brazaj mbona unahangaika sana na huyo ndugai wako? Huo uhuru wa kutoa maoni umeona kwenye tril 1.3? Tena zimekopwa zinatumika ndani, lakini zile tril 1.5 alizokwapua mwendazake ambapo ndugai alikuwa anazikingia kifua kwa kila aliyejaribu kuhoji kumuita kamati ya bunge? Mbona huo uhuru wake hakuutumia kwenye kamati ya bajeti wakati pendekezo limepekwa bungeni kwake? Pole sana ndugai kashaliwa kichwa
 
Ndungai & the gang ndio muasisi/waasisi wa uminywaji wa uhuru wa kutoa maoni ....rooster are coming home to roost.

"Let them go home constitutionally. Not at the expense of their right to utilize a washroom."

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
We brazaj mbona unahangaika sana na huyo ndugai wako? Huo uhuru wa kutoa maoni umeona kwenye tril 1.3? Tena zimekopwa zinatumika ndani, lakini zile tril 1.5 alizokwapua mwendazake ambapo ndugai alikuwa anazikingia kifua kwa kila aliyejaribu kuhoji kumuita kamati ya bunge? Mbona huo uhuru wake hakuutumia kwenye kamati ya bajeti wakati pendekezo limepekwa bungeni kwake? Pole sana ndugai kashaliwa kichwa

Ndugai si wangu mjomba. Nina hangaika na haki.

Haki ni haki tu. Iwe yako, yangu, ya Ndugai, ya Polepole au ya awaye yote.

Hatuwezi kuwa na different standards towards human rights.

Ni hayo tu mheshimiwa Jaji.
 
Huwezi kulilia haki hivyo kwa mtu aliyeshiriki kwa namna kubwa kuua haki za watu hivyo hapo wewe unalako jambo ni zaidi ya hiyo unayodai bi haki pole sana
 
Katiba ya JMT imeeleza wazi uhuru wa muhimili wa bunge na madaraka ya spika ila tatizo Ndugai alishashiriki kuvunja nguvu ya bunge analoliongoza kwa kugeuka kibaraka wa muhimili mwingine ndio maana hata katiba imeshindwa kumlinda.

Acha kuingiza uchama na uhisia kwenye content. Mapambano haya ni ya katiba ya CCM. Chama kikiamua kinakudhalilisha. Kumbuka wabunge wa CCM ndo wengi.

Ndo hao watakaa na kupiga kura kukuondoa kwa kukosa imani nawe. Ukiingia siasa jua Hii ndo michezo yake. Hatari Lakini salama.
 
Wengine sio rahisi uwaone hapo, kuna kiongozi mmoja wa chama mshirika anakuja na kauli "Tume Huru ilete Katiba Mpya" huyu ameshajua rafiki yake alisema Katiba Mpya isubiri sasa anaenda na matakwa yake, sio mpinzani tena.
 
Back
Top Bottom