Amefurushwa Mh. Ndugai kiongozi wa mhimili kinyume cha katiba.
Katika hali ya kusikitika, ni Chadema na NCCR pekee ndiyo angalau wamefahamika wanasimama wapi kwenye kadhia hii:
View attachment 2073184
Bado hakuna matamko yoyote rasmi ya kupinga au hata kukemea vikali kabisa ukiukwaji mkubwa huu wa haki za Mh. Ndugai.
Pamoja na makosa yake mengine yoyote, kufurushwa kwa kutoa maoni yake tu:
"kumbe angeweza kufurushwa hata kwa kwenda kujisaidia tu?"
Wako wapi CUF, ACT, CHAUSTA, UMD, CHAUMA, DP, nk?
Nani alipaswa kuwaongoza wananchi kuukataa ukiukwaji mkubwa huu wa haki za msingi za watu?
Nchi zinaongozwa kwa mujibu wa katiba si kwa kununa, hasira, chuki, visasi nk.
Ndugai mnyongeni ila kutoa maoni ilikuwa haki yake.
___________
Angalizo: DP ya Mtikila isingeufumbia macho ukiukwaji huu wa haki za mtu.
Nini kimebadilika? DP si ingalipo?
Apumzike kwa amani Rev. Mtikila.