Kosa la Ndugai ni lipi? kuhoji kukopa hovyo kila siku kama ndio sifa hii? nawe kama unaamini Ndugai amekosa una mtindio wa ubongo.Ona sasa kumbe unaishi kwa assumptions? Ndio niliona nia yako ovu toka awali wewe utakuwa ja ubia na ndugai yaani muda wote unalialia kumbe una lako jambo, mwenywe aliyefanya kosa kajua kosa kaomba radhi wewe unasema kafuna kombe ili iweje afunike kombe?
Haki ni nini?Ndugai si wangu mjomba. Nina hangaika na haki.
Haki ni haki tu. Iwe yako, yangu, ya Ndugai, ya Polepole au ya awaye yote.
Hatuwezi kuwa na different standards towards human rights.
Ni hayo tu mheshimiwa Jaji.
CHADEMA walishaweka wazi kuwa wanatetea haki ya mtu yeyote yule, iwe ni wa ccm, cuf, act wazalendo au iwe aliwaytesa au kuwanyanyasa ili mradi tu ni mwanadamu na haki yake inavunjwa
Haki ni nini?
Jambo kubwa ilikuwa kumtoa Ndugai kuwa Spika mengine tutarekebisha
Wewe una chuki na mama huna cha haki wala nini ndio maana hata gwajima alihoji iweje kila kitu kipite kwako alafu utoke hadharani uanze kukosoa wewe si kama una agenda ingine ni ipi? Ndugai kafanya mambo ya ovyo mengi sana kuanzia term ya kwanza ya magu hadi ya pili mwanzoni yote haya hujayaona eti lissu sijui nini, sisi tunachosema ndugui kwanza yeye mwenywe kaomba radhi kwa maana kajua kosa lake ma ndio maana baada ya msamaha wake kukatalia kaamua kujiuzulu leo unasema haki yake imesiginwa, ni haki ipi hiyo? Utoke kwenye sahani ya chakula ndani uje nje ulalamike chakula kina chumvi. Bro nakushauri fanya shughuli zako achana na ushabiki maandazi huo hautakusaidia
CAG Musa Assad
BUNGE NI DHAIFU
kipi kilichomkuta?
Tuna simama na mwenyekiti wetu[emoji1787].
Ila upinzani uwa hawaeleweki wanataka nini
Kuna kipindi walipiga Sana kelele ndugai ajiuzulu ndugai ajiuzulu.
Leo kafukuzwa mnalalamika
"Ndugai mnyongeni ila kutoa maoni ilikuwa haki yake."
Yeye alipowaita wenzake kuwaji walipo toa maoni yao yanayolindwa kikatiba haikuwa shida? alipotumia madaraka yake vibaya kuwavua wabunge waliochagulowa kihalali na wananchi haikuwa nongwa, yeye alipoleta polisi kuwadhalilisha wabunge wengine ndani ya bunge haikuwa tatizo ,alipowasimamisha baadhi ya wabunge bila sababu za msingi hapakuwa na mawaa.Ila yeye njia zile zile alizotumia kuwasurubu wengine zilipotumiwa dhidi yake kilio kimekuwa kingi!!!.
Kifupi anatakiwa kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka.Ila basi alijitengenezea kinga ya kutoshitakiwa bila hivyo alitakiwa kuwajibika kisheria.
Tena umenikumbusha wale wabunge wa CUF mahakama ilisema warudi bungeni Jamaa yako AKAKAIDI AMRI YA MAHAKAMA.
Yeye alidharau mhimili mwingine malipo ni hapa hapa duniani na yeye leo kadharauliwa na mhimili mwingine,ngoma droo.
Halfu nikukumbushe Jamaa yako alijaa kiburi kuliko maelezo mtu kuuliza swali tu anaitwa kamati ya maadili "it was fair?"
katiba imevunjwa mara ngapi na mbona hamkuchukua hatua zozote?Una maana penati tumepewa kipa hamna golini sisi tumesusa? Kwamba tutafunga kwa nguvu zetu na hiyo ni fainali kombe la dunia dak ya majeruhi?
Seriously?
Bado huoni kuwa tuna matatizo makubwa mno?
Mussa Asad yeye haikuwa haki yake kutoa maoni?
Upinzani sijui mmerogwa na Nani?huyo jamaa kawatesa Sana bungeni leo mnamuonea huruma
katiba imevunjwa mara ngapi na mbona hamkuchukua hatua zozote?
Atoke kwanza Ndugai mengine yatafuata sababu Ndugai ndiyo alikuwa anaongoza kwa kuvunja katibaNdiyo maana tunalalamika na kutoridhishwa na status quo:
CHADEMA: Kujipanga kwa Ukombozi hakuna Ukomo
Sisi ni wanachama kwenye vyama hivi. Kama wanachama tukajikuta tumefungwa kamba mikononi na miguuni.
Au ulitaka tukachukulie hatua wapi?
Uliyerogwa utakuwa ni wewe. Wakukusikiliza kwenye huu utopolo waki labda Chatto na Makunduchi huko:
1. Tulipokuwa tukimpigia kelele Ndugai kwenye ukiukaji wake mkubwa wa katiba dhidi, ya kina Assad, pascal, na yake mengi bungeni - mlikuwa upande wa udhwalimu.
2. Leo tukipigia kelele haki za Ndugai kukiukwa - mko upande wa upande wa udhwalimu.
Tofauti yetu na nyinyi ni kuwa sisi hatuna simile na ubaradhuli.
Bila shaka utakuwakuwa ni mmoja katika washirika muhimu sana kwenye ubaradhuli.
Atoke kwanza Ndugai mengine yatafuata sababu Ndugai ndiyo alikuwa anaongoza kwa kuvunja katiba
Shida hamjui mnataka nini.
Na mna mchanganya Mungu.
au mnadhani ndugai akiwa spika wa bunge ndo atawapa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi?
Ndugai awepo asiwepo hawasaidii chochote katika harakati zenu ni kazi bure NI sawa na mumtetee au msimtetee HAMUWEZI KUBADILISHA MAAMUZI.
Mbowe kapewa kesi ya ugaidi umemuona ndugai akimtetea?
Ila nyie wazee wa kuruka na beat kimbele mbele.
JIFUNZENI KUBALANCE SHOBO
Una mawazo mgando na huelewi unachoongea.
"Ndugai kama Ndugai ni adui yetu mkubwa kama ulivyo wewe."
Hata hivyo haki hata za adui yetu ukiwamo wewe ukipenda ni haki zetu pia.
"JIFUNZENI KUBALANCE SHOBO"
Kosa la Ndugai ni lipi? kuhoji kukopa hovyo kila siku kama ndio sifa hii? nawe kama unaamini Ndugai amekosa una mtindio wa ubongo.