Five55
JF-Expert Member
- Jun 14, 2024
- 325
- 331
Na. Manase Visulo
Nikiri kwamba taarifa za kujiuzulu kwa Balozi wetu nchini Cuba, Balozi Polepole sio jambo lililotarajiwa wala kufikiriwa na tulio wengi.
Nikwasababu hiyo naomba kuteta nanyi kwa kusema mambo Saba (7 ) ikiwa sita ni ya kufikirisha kwa kuzingatia historia ya Balozi Polepole kabla,Wakati na baada ya kuingia kwenye mfumo wa chama na Serikali na zaidi sababu alizotoa kama msingi wa yeye kujiuzulu;
2. Maoni yangu kwamba PolePole wa Bunge la Katiba sio Polepole wa baada ya uteuzi wa chama kama Mwenezi
Nakumbuka kauli yake ya " Unajua V8?" Akinasibisha CCM ya wakati wake na utajiri , akisahau dhana ya chama cha wakulima na wafanyakazi!
3. Ni dhana ya Demokrasia ndani na nje ya chama
Sitaki kuamini kama ni PolePole huyu wa CCM chini ya awamu ya 5 anaehoji Demokrasia ya CCM awamu ya sita au Demokrasia ya nchi awamu ya sita. Hili ninaliacha kama swali kwa wasomaji , nikweli kwamba kuna mjadala kuhusu demokrasia miongoni mwa wadau. Lakini nadhan Polepole anaeweza kuzungumzia hilo ni yule wa Tume ya Katiba sio huyu baada ya kuwa mwenezi CCM
Mtakumbuka akiwa Mwenezi CCM , Polepole alitamani kuwa binadamu ambae ni kila kitu hata kudhihaki wakosoaji kwa kejeli na vitisho!
4. Ni misingi gani ya chama ambayo alitaka Rais Samia atekeleze zaidi ya alichokifanya kwenye kukabili adui watatu wa Taifa; Ujinga, Maradhi na Umasikini?
5. Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza Bajeti ya afya kutoka TZS900bn mpaka TZS1.62Trilioni.
RAIS Samia ameongeza huduma za dharula kutoka hospital 7 mpaka Hospitali125, vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 8,783 mpaka 12, 846 sawa na ongezeko la Vituo vipya 4,063 na matokeo yake ni kushuka kwa idadi ya vifo vya watoto kutoka 67 mpaka 43 katika kila watoto 1000.
Afya ni pamoja na maji, ndio maana tafiti zinaonesha kwamba katika kila dola moja ($1) inayowekezwa kwenye uzalishaji wa maji, inaokoa dola nne ($4) ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama. Awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa sekta ya maji kwa kutekeleza miradi ya maji 2,331.
6. Ni uwekezaji mkubwa kwenye elimu
Mikopo ya elimu juu kutoka wanafunzi 142,170 sawa na TZS464bn Hadi wanafunzi 248,332 sawa na TZS787.4 Vyuo vya kati kutoka 662 hadi 860 sawa na kujenga VETA mpya 198 na hii ni miaka minne tu.
7. Vita dhidi ya umasikini imepiganwa awamu ya sita
Uwekezaji mkubwa kilimo kutoka Bajeti ya TZ294bn hadi TZS1.24Trilioni yenye matokeo kwenye ongezeko la eneo la umwagiliaji kutoka hekta 561,383 mpaka hekta 983,466.06.
Upatikanaji wa mboleo umeongezeka kutoka tani za Mbolea 678.017 mpaka tani milioni 1.21 Katika miaka minne (4) zaidi ya 700bn zimetumika kuagiza mbolea na kusababisha matumizi ya mbolea kuongezeka kutoka kilo 19 mpaka 24 kwa hekta, hii inatafsiri kubwa kwenye tija. Ndio sababu Tanzania imeongoza afrika kwa Uzalishaji wa chakula na Hifadhi
Sekta zote zinazopunguza umasikini zimeguswa kuanzia wachimbaji wadogo mpaka utalii. Sekta ya barabara amejenga kilometa mpya la lami 4,721 amesambaza umeme kwenye jumla ya vijiji vipya 3,731 na kufanya vijiji vyote 12,318 kuwa na umeme hata hivyo hajaishia hapo ameufikisha kwenye Vitongoji 33,657 kati ya 64,359 sawa na 52.3% hii ni miaka minne tu
8. Nihitimishe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amefanya pakubwa kugusa wanyonge.
Tumesahau wafanyakazi waliokwama mafao yao tangu miaka ya 1990, wakidai serikali zaidi ya TZS2.18Trilioni ,Watu Hawa wameidai Serikali kwa zaidi ya Miaka 35 leo deni hili limelipwa kupitia hati fungani maalumu ya Trilioni 2.67,
Ndio maana najiuliza tuhuma zote alizozitaja Hamprey Polepole zinahusu maendeleo ya wananchi wa nchi hii au nchi nyingine?

- Pongezi.