GE2025 Kujiuzulu kwa Polepole na maswali 7 yanayofikirisha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Na. Manase Visulo

Nikiri kwamba taarifa za kujiuzulu kwa Balozi wetu nchini Cuba, Balozi Polepole sio jambo lililotarajiwa wala kufikiriwa na tulio wengi.

Nikwasababu hiyo naomba kuteta nanyi kwa kusema mambo Saba (7 ) ikiwa sita ni ya kufikirisha kwa kuzingatia historia ya Balozi Polepole kabla,Wakati na baada ya kuingia kwenye mfumo wa chama na Serikali na zaidi sababu alizotoa kama msingi wa yeye kujiuzulu;

  1. Pongezi.
Kwamba uamuzi wake wa kujiengua kwenye Serikali asiyoridhika na utendaji wake ni ustaarabu! Wote waliofanya hivi duniani kote walipongezwa. Hivyo napenda kumpongeza.

2. Maoni yangu kwamba PolePole wa Bunge la Katiba sio Polepole wa baada ya uteuzi wa chama kama Mwenezi

Nakumbuka kauli yake ya " Unajua V8?" Akinasibisha CCM ya wakati wake na utajiri , akisahau dhana ya chama cha wakulima na wafanyakazi!

3. Ni dhana ya Demokrasia ndani na nje ya chama

Sitaki kuamini kama ni PolePole huyu wa CCM chini ya awamu ya 5 anaehoji Demokrasia ya CCM awamu ya sita au Demokrasia ya nchi awamu ya sita. Hili ninaliacha kama swali kwa wasomaji , nikweli kwamba kuna mjadala kuhusu demokrasia miongoni mwa wadau. Lakini nadhan Polepole anaeweza kuzungumzia hilo ni yule wa Tume ya Katiba sio huyu baada ya kuwa mwenezi CCM

Mtakumbuka akiwa Mwenezi CCM , Polepole alitamani kuwa binadamu ambae ni kila kitu hata kudhihaki wakosoaji kwa kejeli na vitisho!

4. Ni misingi gani ya chama ambayo alitaka Rais Samia atekeleze zaidi ya alichokifanya kwenye kukabili adui watatu wa Taifa; Ujinga, Maradhi na Umasikini?

5. Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza Bajeti ya afya kutoka TZS900bn mpaka TZS1.62Trilioni.

RAIS Samia ameongeza huduma za dharula kutoka hospital 7 mpaka Hospitali125, vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 8,783 mpaka 12, 846 sawa na ongezeko la Vituo vipya 4,063 na matokeo yake ni kushuka kwa idadi ya vifo vya watoto kutoka 67 mpaka 43 katika kila watoto 1000.

Afya ni pamoja na maji, ndio maana tafiti zinaonesha kwamba katika kila dola moja ($1) inayowekezwa kwenye uzalishaji wa maji, inaokoa dola nne ($4) ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama. Awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa sekta ya maji kwa kutekeleza miradi ya maji 2,331.

6. Ni uwekezaji mkubwa kwenye elimu

Mikopo ya elimu juu kutoka wanafunzi 142,170 sawa na TZS464bn Hadi wanafunzi 248,332 sawa na TZS787.4 Vyuo vya kati kutoka 662 hadi 860 sawa na kujenga VETA mpya 198 na hii ni miaka minne tu.

7. Vita dhidi ya umasikini imepiganwa awamu ya sita

Uwekezaji mkubwa kilimo kutoka Bajeti ya TZ294bn hadi TZS1.24Trilioni yenye matokeo kwenye ongezeko la eneo la umwagiliaji kutoka hekta 561,383 mpaka hekta 983,466.06.

Upatikanaji wa mboleo umeongezeka kutoka tani za Mbolea 678.017 mpaka tani milioni 1.21 Katika miaka minne (4) zaidi ya 700bn zimetumika kuagiza mbolea na kusababisha matumizi ya mbolea kuongezeka kutoka kilo 19 mpaka 24 kwa hekta, hii inatafsiri kubwa kwenye tija. Ndio sababu Tanzania imeongoza afrika kwa Uzalishaji wa chakula na Hifadhi

Sekta zote zinazopunguza umasikini zimeguswa kuanzia wachimbaji wadogo mpaka utalii. Sekta ya barabara amejenga kilometa mpya la lami 4,721 amesambaza umeme kwenye jumla ya vijiji vipya 3,731 na kufanya vijiji vyote 12,318 kuwa na umeme hata hivyo hajaishia hapo ameufikisha kwenye Vitongoji 33,657 kati ya 64,359 sawa na 52.3% hii ni miaka minne tu

8. Nihitimishe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amefanya pakubwa kugusa wanyonge.

Tumesahau wafanyakazi waliokwama mafao yao tangu miaka ya 1990, wakidai serikali zaidi ya TZS2.18Trilioni ,Watu Hawa wameidai Serikali kwa zaidi ya Miaka 35 leo deni hili limelipwa kupitia hati fungani maalumu ya Trilioni 2.67,

Ndio maana najiuliza tuhuma zote alizozitaja Hamprey Polepole zinahusu maendeleo ya wananchi wa nchi hii au nchi nyingine?
buyo polepole kuna kitu kibaya kafanya kule kwenye ubalozi cuba ndio maana kajiuzulu kwa kuogopa kukamatwa kwa wizi
 
Ukifanikiwa kuusoma barua ya pole pole ?

Ulifanikiwa kuusoma na kuusikiliza ufafanuzi wa Polepole?

Ulishawahi kuwa Balozi na ukaionja radha yake ?

Unadhani Polepole angeliamua tu kupiga kimya na kuendelea tu kula mema ya inji unadhani angelipunguliwa wapi?

Unadhani huo unafiki wa Polepole unamaslahi gani kwake kiuchumi na kijamii?

Tuache kujibu hoja tusizo na uwezo wazo mkuu.

Ninachojua kelele zake zinaweza zisiwe na tija saana kwa vyama vya upinzani lakini kwa upande mwingine zipo , anaetusaidia kumpiga adui tunaepigana nae ni mwenzetu .
 
Back
Top Bottom