GE2025 Kujiuzulu kwa Polepole na maswali 7 yanayofikirisha

GE2025 Kujiuzulu kwa Polepole na maswali 7 yanayofikirisha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Na. Manase Visulo

Nikiri kwamba taarifa za kujiuzulu kwa Balozi wetu nchini Cuba, Balozi Polepole sio jambo lililotarajiwa wala kufikiriwa na tulio wengi.

Nikwasababu hiyo naomba kuteta nanyi kwa kusema mambo Saba (7 ) ikiwa sita ni ya kufikirisha kwa kuzingatia historia ya Balozi Polepole kabla,Wakati na baada ya kuingia kwenye mfumo wa chama na Serikali na zaidi sababu alizotoa kama msingi wa yeye kujiuzulu;

# Kwanza, Pongezi.

Kwamba uamuzi wake wa kujiengua kwenye Serikali asiyoridhika na utendaji wake ni ustaarabu! Wote waliofanya hivi duniani kote walipongezwa. Hivyo napenda kumpongeza.

#Pili, Maoni yangu kwamba PolePole wa Bunge la Katiba sio Polepole wa baada ya uteuzi wa chama kama Mwenezi

Nakumbuka kauli yake ya " Unajua V8?" Akinasibisha CCM ya wakati wake na utajiri , akisahau dhana ya chama cha wakulima na wafanyakazi!

# Tatu ni dhana ya Demokrasia ndani na nje ya chama

Sitaki kuamini kama ni PolePole huyu wa CCM chini ya awamu ya 5 anaehoji Demokrasia ya CCM awamu ya sita au Demokrasia ya nchi awamu ya sita. Hili ninaliacha kama swali kwa wasomaji , nikweli kwamba kuna mjadala kuhusu demokrasia miongoni mwa wadau. Lakini nadhan Polepole anaeweza kuzungumzia hilo ni yule wa Tume ya Katiba sio huyu baada ya kuwa mwenezi CCM.

Mtakumbuka akiwa Mwenezi CCM , Polepole alitamani kuwa binadamu ambae ni kila kitu hata kudhihaki wakosoaji kwa kejeli na vitisho!

# Nne, Ninawaza ni misingi gani ya chama ambayo alitaka Rais Samia atekeleze zaidi ya alichokifanya kwenye kukabili adui watatu wa Taifa; Ujinga, Maradhi na Umasikini?

#Tano, Leo hii, Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza Bajeti ya afya kutoka TZS900bn mpaka TZS1.62Trilioni.

RAIS Samia ameongeza huduma za dharula kutoka hospital 7 mpaka Hospitali125, vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 8,783 mpaka 12, 846 sawa na ongezeko la Vituo vipya 4,063 na matokeo yake ni kushuka kwa idadi ya vifo vya watoto kutoka 67 mpaka 43 katika kila watoto 1000.

# Afya ni pamoja na maji, ndio maana tafiti zinaonesha kwamba katika kila dola moja ($1) inayowekezwa kwenye uzalishaji wa maji, inaokoa dola nne ($4) ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama. Awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa sekta ya maji kwa kutekeleza miradi ya maji 2,331.

#Sita ni uwekezaji mkubwa kwenye elimu,

Mikopo ya elimu juu kutoka wanafunzi 142,170 sawa na TZS464bn Hadi wanafunzi 248,332 sawa na TZS787.4 Vyuo vya kati kutoka 662 hadi 860 sawa na kujenga VETA mpya 198 na hii ni miaka minne tu.

# Saba, vita dhidi ya umasikini imepiganwa awamu ya sita.

Uwekezaji mkubwa kilimo kutoka Bajeti ya TZ294bn hadi TZS1.24Trilioni yenye matokeo kwenye ongezeko la eneo la umwagiliaji kutoka hekta 561,383 mpaka hekta 983,466.06.

# Upatikanaji wa mboleo umeongezeka kutoka tani za Mbolea 678.017 mpaka tani milioni 1.21 Katika miaka minne (4) zaidi ya 700bn zimetumika kuagiza mbolea na kusababisha matumizi ya mbolea kuongezeka kutoka kilo 19 mpaka 24 kwa hekta, hii inatafsiri kubwa kwenye tija. Ndio sababu Tanzania imeongoza afrika kwa Uzalishaji wa chakula na Hifadhi.

# Sekta zote zinazopunguza umasikini zimeguswa kuanzia wachimbaji wadogo mpaka utalii. Sekta ya barabara amejenga kilometa mpya la lami 4,721 amesambaza umeme kwenye jumla ya vijiji vipya 3,731 na kufanya vijiji vyote 12,318 kuwa na umeme hata hivyo hajaishia hapo ameufikisha kwenye Vitongoji 33,657 kati ya 64,359 sawa na 52.3% hii ni miaka minne tu.


# Nane,Nihitimishe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amefanya pakubwa kugusa wanyonge.

Tumesahau wafanyakazi waliokwama mafao yao tangu miaka ya 1990, wakidai serikali zaidi ya TZS2.18Trilioni ,Watu Hawa wameidai Serikali kwa zaidi ya Miaka 35 leo deni hili limelipwa kupitia hati fungani maalumu ya Trilioni 2.67,

Ndio maana najiuliza tuhuma zote alizozitaja Hamprey Polepole zinahusu maendeleo ya wananchi wa nchi hii au nchi nyingine?
Umeacha mambo muhimu and it's obvious umeyaacha kwa makusudi kabisa.
Two wrongs don't make anything right, vipi haujazungumzia bibie kuendelea utekaji, utesaji na uuaji? Vipi kuhusu Wamasai kuhamishwa kama ng'ombe wanaoswagwa kutoka katika makazi yao na hayo makazi kupewa Waarabu kwa makubaliano ambayo hayako wazi? Kuna usiri wa nini? Vipi bandari za Tanganyika kugeuzwa shamba la bibi huku za Zanzibar zikibakia kuwa untouched?
 
Ubarikiwe umetimiza wajibu wako, mwenye macho anaona, mwenye masikio anasikia, mwenye kujua kusoma anasoma. Huyu mama Rais wetu amefanya mambo makubwa sana kwa muda mfupi, matumaini yangu miaka 5 ijayo atafanya mambo makubwa zaidi. Polepole kwanza ni wale binadamu very arrogant, wanajiona wanajua kuliko binadamu wengine, pili ni mtu mbinafsi mwenye maslahi yake binafsi, vilevile ni mtu mlalamishi asiyeweza ku-appreciate anachofanya binadamu mwenzake ht km ni nzuri kiasi gani. Kumbuka Magu alimwokoteza kwenye vile vitaasisi vya kuikosoa serikali na walalamishi ktk kila kt ili wafurahishe mabwana zao kule Ulaya wapate mkate wao. Ndg nyoka ni nyoka tu, Rais Samia alikosea kuhangaika na kiumbe km Polepole alitakiwa kum-dump basi. Km ni vile vipindi vya mtandaoni serikali ingemtuliza tu kwa utaratibu unaoeleweka. Kingine Polepole yuko kwenye lile genge la kisukuma hawakutaka kabisa Samia awe Rais, baada ya kushindwa kuzuia hilo nafikiri walijipanga amalizie tu kipindi cha Magu na asigombee au akigombea asifanikiwe, sasa ameudhika sana kuona CCM kumpitisha Samia kuwa mgombea pekee wa CCM, na hiyo kujiuzulu ni uvumilivu ulimshinda. Kosa lilikuwa la Magufuli kuokoteza magarasha, Polepole hakuwa mwanaCCM km alivyo Dr. Bashiru Ally, Bashiru alikuwa CUF hiyo inajulikana. Chama kiongozi wake kimlee tangia akiwa mtoto huyo anajua misingi ya chama na hatatetereshwa na wimbi lolote. Huyu mwenezi wa sahivi Amos Makalla aliongoza kura maoni CCM mwaka 2020 jimbo la Mvomero Magu akamchukua mshindi wa 3 ila Makalla hatukumsikia akitetereka, maana makala alikuwa tangia chipukizi wa CCM, baadaye UVCCM. Viongozi wa CCM wawe na wivu na chama siyo kila mtu ni wa kumpa uongozi.
Nepotism at it's peak.
 
Polepole ni masalia ya Mwendazake, hawezi kuona hiyo picha kubwa (big picture) uliyoiweka kwa vile Samia AMENG'ARA katika performance tofauti na matarajio ya Sukuma Gang waliotaka kumpora madaraka.
Ameng'ara? Labda kama ameng'ara kwenye kalio lako.
 
Na. Manase Visulo

Nikiri kwamba taarifa za kujiuzulu kwa Balozi wetu nchini Cuba, Balozi Polepole sio jambo lililotarajiwa wala kufikiriwa na tulio wengi.

Nikwasababu hiyo naomba kuteta nanyi kwa kusema mambo Saba (7 ) ikiwa sita ni ya kufikirisha kwa kuzingatia historia ya Balozi Polepole kabla,Wakati na baada ya kuingia kwenye mfumo wa chama na Serikali na zaidi sababu alizotoa kama msingi wa yeye kujiuzulu;

  1. Pongezi.
Kwamba uamuzi wake wa kujiengua kwenye Serikali asiyoridhika na utendaji wake ni ustaarabu! Wote waliofanya hivi duniani kote walipongezwa. Hivyo napenda kumpongeza.

2. Maoni yangu kwamba PolePole wa Bunge la Katiba sio Polepole wa baada ya uteuzi wa chama kama Mwenezi

Nakumbuka kauli yake ya " Unajua V8?" Akinasibisha CCM ya wakati wake na utajiri , akisahau dhana ya chama cha wakulima na wafanyakazi!

3. Ni dhana ya Demokrasia ndani na nje ya chama

Sitaki kuamini kama ni PolePole huyu wa CCM chini ya awamu ya 5 anaehoji Demokrasia ya CCM awamu ya sita au Demokrasia ya nchi awamu ya sita. Hili ninaliacha kama swali kwa wasomaji , nikweli kwamba kuna mjadala kuhusu demokrasia miongoni mwa wadau. Lakini nadhan Polepole anaeweza kuzungumzia hilo ni yule wa Tume ya Katiba sio huyu baada ya kuwa mwenezi CCM

Mtakumbuka akiwa Mwenezi CCM , Polepole alitamani kuwa binadamu ambae ni kila kitu hata kudhihaki wakosoaji kwa kejeli na vitisho!

4. Ni misingi gani ya chama ambayo alitaka Rais Samia atekeleze zaidi ya alichokifanya kwenye kukabili adui watatu wa Taifa; Ujinga, Maradhi na Umasikini?

5. Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza Bajeti ya afya kutoka TZS900bn mpaka TZS1.62Trilioni.

RAIS Samia ameongeza huduma za dharula kutoka hospital 7 mpaka Hospitali125, vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 8,783 mpaka 12, 846 sawa na ongezeko la Vituo vipya 4,063 na matokeo yake ni kushuka kwa idadi ya vifo vya watoto kutoka 67 mpaka 43 katika kila watoto 1000.

Afya ni pamoja na maji, ndio maana tafiti zinaonesha kwamba katika kila dola moja ($1) inayowekezwa kwenye uzalishaji wa maji, inaokoa dola nne ($4) ambazo zingetumika kutibu magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama. Awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa sekta ya maji kwa kutekeleza miradi ya maji 2,331.

6. Ni uwekezaji mkubwa kwenye elimu

Mikopo ya elimu juu kutoka wanafunzi 142,170 sawa na TZS464bn Hadi wanafunzi 248,332 sawa na TZS787.4 Vyuo vya kati kutoka 662 hadi 860 sawa na kujenga VETA mpya 198 na hii ni miaka minne tu.

7. Vita dhidi ya umasikini imepiganwa awamu ya sita

Uwekezaji mkubwa kilimo kutoka Bajeti ya TZ294bn hadi TZS1.24Trilioni yenye matokeo kwenye ongezeko la eneo la umwagiliaji kutoka hekta 561,383 mpaka hekta 983,466.06.

Upatikanaji wa mboleo umeongezeka kutoka tani za Mbolea 678.017 mpaka tani milioni 1.21 Katika miaka minne (4) zaidi ya 700bn zimetumika kuagiza mbolea na kusababisha matumizi ya mbolea kuongezeka kutoka kilo 19 mpaka 24 kwa hekta, hii inatafsiri kubwa kwenye tija. Ndio sababu Tanzania imeongoza afrika kwa Uzalishaji wa chakula na Hifadhi

Sekta zote zinazopunguza umasikini zimeguswa kuanzia wachimbaji wadogo mpaka utalii. Sekta ya barabara amejenga kilometa mpya la lami 4,721 amesambaza umeme kwenye jumla ya vijiji vipya 3,731 na kufanya vijiji vyote 12,318 kuwa na umeme hata hivyo hajaishia hapo ameufikisha kwenye Vitongoji 33,657 kati ya 64,359 sawa na 52.3% hii ni miaka minne tu


8. Nihitimishe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amefanya pakubwa kugusa wanyonge.

Tumesahau wafanyakazi waliokwama mafao yao tangu miaka ya 1990, wakidai serikali zaidi ya TZS2.18Trilioni ,Watu Hawa wameidai Serikali kwa zaidi ya Miaka 35 leo deni hili limelipwa kupitia hati fungani maalumu ya Trilioni 2.67,

Ndio maana najiuliza tuhuma zote alizozitaja Hamprey Polepole zinahusu maendeleo ya wananchi wa nchi hii au nchi nyingine?
Umekuja kumsifu Bi Kizimkazi na kumwimbia mapambio tu kamakawaida yenu lakini hujajibu hoja wala kubadilisha fikra za yeyote kusema tuna Rais hapo

Tanzania mpaka hapa tulipo hatuna kuongozi wa nchi, bali tuna kundi/genge la wahuni na washenzi fulani tu ndo wanaiburuza nchi hii watakavyo huku mama yenu akiwa kama kinyago au picha tu isiyo na maana yeyote

Sisi hatuna shida na historia ya nyuma ya mtu. Lakini anayetoka na kukiri kwa kinywa chake na kuamini moyoni mwake kuwa, nchi hii kwa sasa inahitaji mabadiliko ya kimfumo na kiutawala na kuungana na wanaodai mabadiliko hayo na tukamwangalia na kuona kuwa amebadilika, huyo ni mwenzetu

Kwa ujasiri wa Polepole kutema marupumarupu ya ubalozi na kukosoa serikali na boss wake hadharani, anastahili kuungwa mkono

Lakini, we are very carefully. We are still scrutinizing his honesty yet
 
Ubarikiwe umetimiza wajibu wako, mwenye macho anaona, mwenye masikio anasikia, mwenye kujua kusoma anasoma. Huyu mama Rais wetu amefanya mambo makubwa sana kwa muda mfupi, matumaini yangu miaka 5 ijayo atafanya mambo makubwa zaidi. Polepole kwanza ni wale binadamu very arrogant, wanajiona wanajua kuliko binadamu wengine, pili ni mtu mbinafsi mwenye maslahi yake binafsi, vilevile ni mtu mlalamishi asiyeweza ku-appreciate anachofanya binadamu mwenzake ht km ni nzuri kiasi gani. Kumbuka Magu alimwokoteza kwenye vile vitaasisi vya kuikosoa serikali na walalamishi ktk kila kt ili wafurahishe mabwana zao kule Ulaya wapate mkate wao. Ndg nyoka ni nyoka tu, Rais Samia alikosea kuhangaika na kiumbe km Polepole alitakiwa kum-dump basi. Km ni vile vipindi vya mtandaoni serikali ingemtuliza tu kwa utaratibu unaoeleweka. Kingine Polepole yuko kwenye lile genge la kisukuma hawakutaka kabisa Samia awe Rais, baada ya kushindwa kuzuia hilo nafikiri walijipanga amalizie tu kipindi cha Magu na asigombee au akigombea asifanikiwe, sasa ameudhika sana kuona CCM kumpitisha Samia kuwa mgombea pekee wa CCM, na hiyo kujiuzulu ni uvumilivu ulimshinda. Kosa lilikuwa la Magufuli kuokoteza magarasha, Polepole hakuwa mwanaCCM km alivyo Dr. Bashiru Ally, Bashiru alikuwa CUF hiyo inajulikana. Chama kiongozi wake kimlee tangia akiwa mtoto huyo anajua misingi ya chama na hatatetereshwa na wimbi lolote. Huyu mwenezi wa sahivi Amos Makalla aliongoza kura maoni CCM mwaka 2020 jimbo la Mvomero Magu akamchukua mshindi wa 3 ila Makalla hatukumsikia akitetereka, maana makala alikuwa tangia chipukizi wa CCM, baadaye UVCCM. Viongozi wa CCM wawe na wivu na chama siyo kila mtu ni wa kumpa uongozi.
Porojo ndefuu pumba tupu
 
Tunamsaidia kufanya nini?
Magu alipendwa na wengi mno huku mtaani hata kifo chake watu 45 walipoteza maisha wakimuomboleza.. ila huyu hapendwi hadi na wanawake wenzie ni Rubbish President
 
Mleta mada katumia nafasi ya kumshushua mwenzao wakati akipiga Kampeni kwa Samia kwa kuweka takwimu ambazo ni wajibu wa serikali kutimiza hayo; lakini anasahau kuwa mizani (kwa bahati mbaya siku hizi siyo analog tena, imekuwa digital) ya upande wa ili ni nzito zaidi ya hayo aliyoyapigia chapuo yeye.

Nikikaa hapa na kutazama huo upande wa pili, nitajaza kurasa; na muda huo kwa sasa sina. Itoshe tu kusema kuwa la msingi zaidi ni HAKI ya mTanzania kuwa HURU kumchagua kiongozi yeyote anayemtaka yeye, bila ya kusumbuliwa, wala kuwa na mashaka ya kura yake kuhesabiwa. Samia hili kwake ni sumu, na hili ndilo linamwondolea heshima yoyote ya kuwa kiongozi wa nchi. Sasa tunasubiri auwe waTanzania ili aendelee madarakani kwa nguvu.

Utajenga mashule ya kueneza ujinga huo uendelee; utajenga mahospitali ya watu wajinga wasiokuwa na haki yoyote ya kuwachaguwa viongozi wao?
Unajenga mahospitali kujaza wagonjwa wenye msongo wa akili? Tena mahospitali ambayo huduma zake wananchi hawana uwezo nazo?

Sijasema chochote katika uharibifu unaofanywa na Samia juu ya raslimali za taifa hili; na zaidi sizungumzii kuwatengeneza waTanzania kuwa watwana ndani ya nchi yao wenyewe! Kiongozi asiye amini wananchi wake kuwa na uwezo.

Hizo shule zinajengwa zifanye kazi gani, ya kutengeneza watwana; badala ya watu wanaojiamini na kuamini uwezo wao wa kujiletea maendeleo yao wenyewe?

Hili ni jibu la haraka haraka, bila ya mpangilio maalum, kuonyesha ubovu wa uongozi wa Samia Suluhu Hassa; mtu asiyekuwa na dira yoyote juu ya nchi hii! Mtu aliye okotwa tu; na kuewa uongozi wa nchi ambayo hana uchungu wowote juu yake!.

Mwisho: Sasa kaishika CCM, yeye na GENGE lake, siyo CCM Chama cha wananchi tena. Hili nalo tumpongeze; wakati akichochea mifarakanyo kati yetu wenyewe, kwa kujenga makundi kwenye jamii zetu, ili tufarakane zaidi?
 
Wewe ndugu mwandishi uko ndani ya serikali au nje?

Unateuzi yoyote kutoka kwa Rais?

Umewahi kushika wadhifa wowote wa juu kwenye chama au serikali

Kama hayo yote ujawahi pitia then kaa kimya tu

Yeye anajua zaidi yako,

Hizi namba za takwim za ela ziko kwenye makaratasi tu umeenda site ukaona hizo ela zimetumika?

Kila mwaka wa bajet wizara zinalalamika zimepata pesa pungufu ya ombi lao

So achana na namba za makaratasi twende kwenye reality
Ndio ulaghai wenyewe huo. Hawa watu wanapenda sana kutumia hadaa nyingi na ulaghai kujionyesha kuwa wamefanya kazi kubwa, wakati ni hewa tupu!
Haajawahi kuwa na serikali yenye uongo mwingi kama hii ya Samia Suluhu Hassan.
 
POLE FISADI NA NUSU WALIOTAKA UBUNGE 2020 WANAMJUA VIZURI SANA
OCTOBA NI TIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

MAMA ANAFANYA KILA SEKTA YEYE TU
 
Back
Top Bottom