SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kitendo cha kufikia hatua ya kutoa tuhuma nzito kwa kutumia kipengele cha "Upangaji Matokeo" kuhusiana na mechi ya Mamelodi Sundowns vs Yanga kunanikumbusha siasa zetu za vyama vingi na jinsi migogoro inavyotokeaga.
Kwa haraka nakumbuka migogoro ya kina Mrema ndani ya NCCR, Zito Kabwe ndani ya CHADEMA, na Lipumba ndani ya CUF, hawa wote ni watu waliokaribishwa katika vyama halafu baadae wakaota mapembe na kujaribu kuleta mapinduzi ndani ya vyama vyao.
Ni juzi tu ambapo Yanga ilikuwa inatamba kwamba Hersi ni bosi wa mabosi wote. Leo hii wamesahau yote hayo wanatoa tuhuma kali na nzito dhidi ya Rais wa CAF Patrice Motsepe huku hawajui kuwa ni yeye aliyempa hilo pande Hersi. Na pia jiulize walikuwa wanajisifu nini kwa hiko cheo cha Hersi, kumbe hana ushawishi wowote huko CAF au na yeye ameihujumu Yanga? Labda kweli anaihujumu timu yake maana alishaitabiria kufungwa na Mamelodi.
Yanga wakubali bado ni wachanga katika mashindano haya. Wataendelea kuonewa saaana mpaka kwanza akili ziwakae sawa. Mwaka jana Wydad vs. Simba, Baleke alifunga goli halali lakini refa alipoenda kwenye VAR alifanya maamuzi bila watazamaji kuonyeshwa replay ya VAR, watu tukalalamika kidogo maisha yakaendelea. Yanga kila siku wamekaa kupinga historia za mafanikio ya Simba wakati laiti wangezikubali wasingejiona wao ndiyo wa kwanza kufika huko wanapojisifia maana huko kuonewa Simba wameshakumbana napo sana ikiwemo nusu fainali ya 1974 ambayo Yanga wamekataa kuitambua. Nimewasikia mashabiki hadi viongozi wa Yanga siyo tu hawatambui Simba kufika fainali ya Shirikisho, lakini hawatambui pia Simba kufika nusu fainali ya CAFCL. Kwa maana nyingine hii klabu imeamua kuukumbatia ujinga.
Akili za Yanga zimekuwa corrupted. Juzi kwa ukaribu wao na wanasiasa, wameruhusiwa kuingiza mashabibi bure huku serikali ikijua maafa ambayo yamewahi kutokea walipofanya hivyo siku za nyuma. Maafa yakajirudia tena ila cha kushangaza zaidi, serikali imepoteza mapato kutokana na mechi kufanywa bure, klabu imepoteza mapato bila sababu halafu siku chache baadae serikali hiyo hiyo imeenda kuipatia msaada timu hiyo hiyo ili kupeleka mashabiki Afrika Kusini. Hizi ni akili za watu wanaoendeshwa kisiasa ndiyo wanaweza kufanya maamuzi ya namna hii. Siku zote nimekuwa nasema Yanga ni taasisi ya CCM kama ilivyo UVCCM, UWT-CCM na Baraza la Wazazi. Tofauti ni kuwa kutokana na makatazo ya FIFA, Yanga haijawahi kurasimishwa rasmi kama taasisi ya CCM.
Yanga ikumbuke kuna maisha baada ya robo fainali ya CAFCL 2023-2024. Mashabiki wa Yanga walikuwa wanaicheka Simba kwa kuishia robo fainali kwa misimu mfululizo kama vile wao wameyapatia maisha leo hii wanashangilia "wametoka kiume" katika hatua hiyo hiyo. Kuna AFL ambayo walisema waliahidiwa na Motsepe lakini wanaweza wasipewe hiyo nafasi tena maana anayeweza kuwabeba ndiyo kwanza wanamfanyia zengwe atoke CAF. Kuna kibarua cha Hersi kwenye kile kitaasisi cha mchongo ambacho Motsepe alikianzisha. Yote hayo yatapepea wakiendelea kuwatunishia vifua wenye nguvu na ushawishi.