Ni mtazamo wako tu huu.
Kuna watu wanaishi kijijini washatoboa maisha. Yupo jamaa mmoja anamiliki magari kwa ajili ya biashara ya usafiri kutoka kijijini hadi mjini. Ameanza tangu 2002, ambapo alianzia kwenye uuzaji wa kuku miaka ya late 1990, then akafungua Duka, ikafuatia gari aina ya Landrover kwa wakati huo mwaka 2002, Biashara ikawa inakua. Kila ikifika msimu wa kilimo anaingia shambani kulima vitunguu kwa kutumia faida kutoka kwenye biashara ya Duka na usafiri.
Hadi sasa biashara zake zimeinuka na zinaendelea kupiga hatua, ni tegemeo kwenye usafiri kijijini. Wengi waliowahi kufanya biashara ya usafishaji hawakudumu kama yeye, wengine wanaanza na kumuacha yeye hatetereki.
Binafsi naona ni ile commitment ha mtu kufanya anachokiamini kwa usahihi na kutokata tamaa