Kukabiliana na upungufu wa Dollar nchini, napendekeza safari za nje kwa watumishi wa umma zifutwe

Kukabiliana na upungufu wa Dollar nchini, napendekeza safari za nje kwa watumishi wa umma zifutwe

Zile safari zinakausha hazina Kweli Kweli ndugu,

Mwigu anawaomba WB kutukopesha dollar Ili tuagize mafuta,

Wakati kungedhibiti safari za nje, tungebaki na hazina ya kutosha.

Dollar zipo, ila uzururaji nje ya nchi Kwa watumishi umezidi!!
Taifa lenye viongoz wapenda stareh unategemea nn hapo ndug!! Angalia bungen ni mwendo wa kuongezeana posho tu.
 
Suluhu zingine SHORT Term na Long-term ni:

1. Kuimarisha mahusiano na Russia Ili tuuziwe mafuta Kwa Tshs Badala ya Dollar.

2. Kandarasi kubwa wapewe wazawa, wao ndo waingie ubia na WA nje ktk KAZI wasioziweza, hii itasaidia kupunguza latizo.

3. Uhamasishaji ufanyike Ili watalii waje na dollar nchini tofauti na ilivyo sasa, makampuni ya nche yanalipwa juu Kwa juu.

4. Iwe MARUFUKU kusafirishwa wanyama nje ya nchi. Hii itasaidia kuimarisha utalii.

5. Wawekezaji Toka nje, wasipewe dhamana ya kukopa Benki zetu za ndani na nje. Tumeona hili likishamiri, wakishakopa wanatuachia madeni ambayo yanaongeza deni la Taifa.

6. Sera ya SIASA nchi iboreshwe.

Pawepo Utaratibu wa kubadili vyama vinavyoongoza Nchi. Viwepo vyama vikuu visivyozidi vitatu.

Viwe vinabadilishana uongozi, hii italeta changamoto na hamasa ktk kufikiri Kwa upanga kuleta solutions njema.

Mf Mitano Kwa CDM, akimaliza Mitano wanapewa wengine, bt DIRA ya Taifa iwe moja tu ya miaka 300 ijayo, vyama vishindane kuitekeleza.

7. Mazao ya KILIMO ya biashara yasiuzwe ghafi.

Serikali ivikopeshe vikundi vya wakulima kupitia bank ya KILIMO kuanzisha viwanda vidogo vidogo Ili wafanye package.

Wizara ya mambo ya nje ishiriki Kwa ufasaha kutangaza.

8. Viwanda vilivyouwawa vifufuliwe wapewe vyama vya wakulima.

Viwanda vya pamba Kanda ya ziwa vifufuliwe, vizalishe nguo kutosheleza soko la ndani kupunguza hazina ya dollar kuagiza nguo nje.

Pia vifanye export Kwa ziada katika mataifa ya nje.

9. Wawekezaji hewa wadhibitiwe. Mh Rais majuzi alidokeza juu ya mfanyabiashara aliyekopa mabenki kadhaa ya ndani Kwa kutumia dhamana ya sirikali aliyopewa na baada ya Kupata pesa hizo, alitokomea na kuiachia Serikali deni.

10. Mikataba mibovu iangaliwe.

Ni Ile inayoingiwa Kwa RUSHWA, na Serikali inapojaribu kuvunja, huibuka wazawa wanaotumia kuhakikisha tunashindwa case na kuingia HASARA ya kulipa.

11. Akiba ya Dhahabu iimarishwe.

Wachimbaji wazawa wadhaminiwe kuchukua mikopo kununua machine za kisasa za uchimbaji Ili kuzalisha Dhahabu yetu ya ndani.

Pia Benki kuu inunue Kwa wingi Dhahabu Kutoka Kwa wazawa na kutunza akiba.
 
Kudhibiti Pia Uhaba wa Dollar;

Bureau de change zidhibitiwe Ili kujua HAKIKA mzunguko wa dollar nchini, itasaidia pia kudhibiti wafanyabiashara wanaozitumia kutakatisha pesa haramu,chafu na za wizi!!
 
Kenya hapo Jirani wamechukua ushauri huu,

Kiongozi wetu ndo kwanza yupo Doha Qatar!!
 
Dollar hazipatikani, ila viongozi hawakosi dollar kufanya safari za nje
 
Malipo ya tozo,fees,ada,pango Kwa dola ni uhujumu uchumi..Fedha Za Tanzania zitumike..Hatuna sababu ya kutengeneza mahitaji (Demand) isiyo ya lazima..

Bandari/shipping lines/CFS/Transporters ..Apartments..Vyuo..Kwa nini walazimishe kulipwa USD?..Ikibidi hata mishahara ya watumishi kwenye baadhi ya Makampuni,taasisi na mashirika (NGO’s) ilipwe Kwa TZS.

Tumepoteza wafanyabiashara wengi waliohamia nchi jirani Kama Malawi,Zambia,DRC,Mozambique sababu ya ongezeko la kodi ktk bidhaa nyingi..Tuangalie upya..

Mwisho nchi ipunguze miradi ya miundombinu inayokula fedha nyingi ambazo kimsingi wanalipwa wakandarasi wa kigeni..

Zabuni kubwa Za mabilioni ya fedha ktk procurement (IFB/ICT/ICB/RT)ya nchi wapewe wazawa kimkakati ili malipo yake yabaki nchini badala ya sasa fedha nyingi kwenda nje..
 
Pia tukomeshe biashara ya kuuza wanyama hai nje, tembo, Twiga, Simba nk nk.

Jambo hili linapunguza Utalii nchini hivyo kupunguza mapato ya pesa za kigeni, dollar ikiwamo.
 
Itafika muda hata yeye atakosa nauli
Uzuri wa pesa ni kwamba ukishazisunda nyingi kabisa huwa mwenyewe anakuwa hapati furaha kabisa ya maisha !
Maana kila siku anazifikiria hizo pesa zake !
Na kila siku anawaza ni nini kinaweza kutokea kuhusu hizo pesa zake 😅😅🙏
Mwisho wa siku watakaokuja kuzitumbua ni wengine kabisa sio yeye aliyezisunda !
Maisha iko vile ! To bear in mind maisha ni mafupi sana !!
Dunia ni rangilangire !! 🙏🙏😅
 
Back
Top Bottom