Suluhu zingine SHORT Term na Long-term ni:
1. Kuimarisha mahusiano na Russia Ili tuuziwe mafuta Kwa Tshs Badala ya Dollar.
2. Kandarasi kubwa wapewe wazawa, wao ndo waingie ubia na WA nje ktk KAZI wasioziweza, hii itasaidia kupunguza latizo.
3. Uhamasishaji ufanyike Ili watalii waje na dollar nchini tofauti na ilivyo sasa, makampuni ya nche yanalipwa juu Kwa juu.
4. Iwe MARUFUKU kusafirishwa wanyama nje ya nchi. Hii itasaidia kuimarisha utalii.
5. Wawekezaji Toka nje, wasipewe dhamana ya kukopa Benki zetu za ndani na nje. Tumeona hili likishamiri, wakishakopa wanatuachia madeni ambayo yanaongeza deni la Taifa.
6. Sera ya SIASA nchi iboreshwe.
Pawepo Utaratibu wa kubadili vyama vinavyoongoza Nchi. Viwepo vyama vikuu visivyozidi vitatu.
Viwe vinabadilishana uongozi, hii italeta changamoto na hamasa ktk kufikiri Kwa upanga kuleta solutions njema.
Mf Mitano Kwa CDM, akimaliza Mitano wanapewa wengine, bt DIRA ya Taifa iwe moja tu ya miaka 300 ijayo, vyama vishindane kuitekeleza.
7. Mazao ya KILIMO ya biashara yasiuzwe ghafi.
Serikali ivikopeshe vikundi vya wakulima kupitia bank ya KILIMO kuanzisha viwanda vidogo vidogo Ili wafanye package.
Wizara ya mambo ya nje ishiriki Kwa ufasaha kutangaza.
8. Viwanda vilivyouwawa vifufuliwe wapewe vyama vya wakulima.
Viwanda vya pamba Kanda ya ziwa vifufuliwe, vizalishe nguo kutosheleza soko la ndani kupunguza hazina ya dollar kuagiza nguo nje.
Pia vifanye export Kwa ziada katika mataifa ya nje.
9. Wawekezaji hewa wadhibitiwe. Mh Rais majuzi alidokeza juu ya mfanyabiashara aliyekopa mabenki kadhaa ya ndani Kwa kutumia dhamana ya sirikali aliyopewa na baada ya Kupata pesa hizo, alitokomea na kuiachia Serikali deni.
10. Mikataba mibovu iangaliwe.
Ni Ile inayoingiwa Kwa RUSHWA, na Serikali inapojaribu kuvunja, huibuka wazawa wanaotumia kuhakikisha tunashindwa case na kuingia HASARA ya kulipa.
11. Akiba ya Dhahabu iimarishwe.
Wachimbaji wazawa wadhaminiwe kuchukua mikopo kununua machine za kisasa za uchimbaji Ili kuzalisha Dhahabu yetu ya ndani.
Pia Benki kuu inunue Kwa wingi Dhahabu Kutoka Kwa wazawa na kutunza akiba.