Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Mjomba wake Zitto!!!
 
Watanzania ni viumbe wa ajabu sana.....hapa wanailaumu serikali kuchukua hatua juu ya uzalishaji holela wa bidhaa zinazotumiwa na wanadamu.....lakini ni watu hao hao ndio watakapo ilaumu serikali madhara yakitokea baada ya kutumia bidhaa ambayo haijathibitishwa kwa matumizi ya binadamu.......

Hii ni nchi na nchi ina utaratibu wa mambo yote yanavyokwenda hasa yanayogusa maisha au afya za binadamu moja kwa moja.........

Tunachotakiwa ni kupigania serikali kuondoa vikwazo vinavyoonekana kuwakwamisha wajasiliamali wadogo ili wapae kiuchumi na kuongeza ajira......

Lakini mambo yote hayo yafanyike kwa kuzingatia Hali na afya za binadamu......
 
Nakubaliana nawe 200%
 
ila bashe akitoa viboriti na vibanzi vidogo vidogo vya siasa chafu chafu, kwa kweli atakuwa kiongozi mzuri ndani ya li-chama chakavu la CCM!
CCM ndiyo wanyanyapaa wake,tatizo..
 
Kwani Polisi hawaruhusiwi kutoa hata maelekezo tu kwa watu kama huyo baada ya kumuhoji na kujiridhisha juu ya uelewa wake kwa kosa analotuhumiwa nalo??
 
police au ni TBS ndo wahusika
 
Vipi watengeneza kvant na konyagi fake
Umeisha sema fake . Kwanza ni kosa kutengeneza kitu fake, pili ni kosa kutumia trademarks za mtu/kampuni ya mtu pasipo kibari cha mhusika. Hao ni halali ya gereza.
 
Sijaandika Ili nionekane wa maana, nimeandika kwa mtazamo wangu, naheshimu pia mtazamo wako.
Tatizo lako umeandika kiushabiki sana na kulikandia jeshi la police kana kwamba walichofanya ni kinyume cha sheria. Tunapozungumzia rule of law simply means sheria ni msumeno!
 

Turudi kwa Kibatara ..Je Polisi hao wanajua PGO inssema nini kwa mjasirimia kama huyu?
 
sawa koplo matlda, tumekusikia.
 
Shida kwanini wasitoe ELIMU KWA WANANCHI.
Yaani baada ya kumkamata inatakiwa Sasa wampeleke akafuate hizo taratibu asichukuliwe Kama MUHALIFU.
Mimi hapa nimekuelewa zito na Bashe pia nimemuelewa
 
Jamani, hivi ni kweli tunatetea uhaqlifu? Hivi hiyo bidhaa ikiwadhuru wananchi mtamlaumu nani. Hivi kweli tumefikia mahali pa kuchagua sheria zipi zifuatwe na zipi zipuuzwe. Tutakuwa tunajenga taifa la namna gani? Ni afadhali mtu awe mkweli kuliko huyu aliekyuwa anatengeneza mafuta akiuza kutumia nembo za viwanda vingine. Huyo Zitto sasa hivi amekuwa irrelevant ndiyo maana anarukia vitu ambavyo yeye kama kiongozi wa kitaifa asingetakiwa. Anajikweza tu, but he is done.
 
Bashe akili kubwa sana. TBS waige mfano huu. Badala ya kuangamiza biashara yake kwa kutokuwa na makaratasi tu (usajili) ni vema TBS nao wakikuta watu wa namna hii wawarasimishe na kuwapa utaratibu hata bure ikibidi.
 

Kilatha🤣🤣🤣🤣
 


Anajikweza tu, but he is done.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…