Wewe mpuuzi tu ina maana unataka kusema waliomuua Mushi ni watu wa awamu ya tano? Vipi waliomuua mwanahabari Mwangosi, Dr Mvungi wa katiba mpya na Chacha Wangwe wa CHADEMA kipindi cha awamu ya nne ya Kikwete nao ni watu wa awamu ya tano?Uharibifu uliofanywa kwenye awamu hiyo madhara yake usitegemee yaishe haraka hivyo.
Hizi tabia za kusifusifu viongozi mpaka kufikia kusema Rais katoa hela za kujenga daraja au barabara yameanzia awamu ya tano zaidi, Sasa umeona yalivyonoga Sasa?
Kauli za kutishia kupoteza watu zilipandwa awamu hiyo rejea kauli za kina Musiba, na juzi umemsikia vizuri kiongozi wa uvccm Kagera, alichokisema,umesikia ameitwa kuhojiwa popote?
Kwa hiyo kusema kwa kuwa JPM hayupo asilaumiwe kwa matukio yanayotokea Sasa ambayo yanayafanana na ya kipindi chake, siyo kweli, laana ya uuaji huwa haiondoki kirahisi hivyo.
Wewe hujiulizi umewahi kusikikia vyombo vyetu vya Dola vikisema lolote kuhusu waliomshambulia Lisu angalau kuonyesha wako tofauti na utawala ule?
Ama wamewahi kusema lolote kuhusu walipo akina Azory Ngwanda au Ben Sanane?, Sasa kama watendaji wa serikali waliokuwa awamu hiyo wapo na kwenye awamu hii unategemea mambo yabadilike haraka hivyo!!
Unafikiri kina Mandera walikuwa wajinga kuunda Tume za maridhiano za kuondoa visasi kama kipaumbele cha kwanza,walionao ilikuwa ni lazima kuondoa uchungu kwenye mioyo ya watu walioumizwa kwanza ndio mambo mengine yafuate.
Pia nikukumbushe vipi kuhusu kutekwa kwa Dr Ulimboka kiongozi wa chama cha Madaktari nao walio mteka kipindi cha Kikwete walitumwa na hao wa awamu ya tano?
Acheni ujinga na upumbavu wenu wa kumwongelea mabaya JPM kila kukicha lakini hutasikia mnaongea haya yanayofanyika saizi kwenye utawala wa Samia kama Rais Samia anahusika lakini kipindi cha JPM kila tukio mlisema kawatuma yeye kuua na kuteka watu!
,