Ngoja tuone Jeshi la Police litawapa kesi gani ..... Kesi za uchochezi zote zimebua. Waje na kesi za madai kama wanakifua...!!
Tufanye Malisa GJ na Boniface Jacob wamepotosha jamii, tufanye hivyo yaani kirahisi.....
Kauli ya SACP Muliro, ina utata sana ukimsikiliza kwa sikio la ndani, baada ya kupotea Robert Mashuhuda walidai alichukuliwa Kariakoo na Watu waliojitambulisha kuwa Polisi .........
Taarifa ya Muliro kwa vyombo vya habari ni kwamba Robert aligongwa na gari , akaenda mbali zaidi na kusema baada ya kuokota mwili wa Robert waliupeleka hospital ya Amana wakaambiwa majokofu yamejaa hvyo wakapeka mwili walipotaka wao....,Mkurugenzi wa hospital ya amana alipoulizwa akasema haijawahi kutokea Mochwari kujaa pale ,unajiuliza ni nani anaye potosha jamii mpaka sasa hivi??
Nani Mpotoshaji kati ya hawa watu watatu?
Kwa hii SAGA Maswali ni mengi sana......
1.Muliro alijuaje ni gari lilimgonga Robert na si mbwa alimrarua?
2.Mpaka sasa mwili haujazikwa ,nwili una majeraha ya kupigwa au ni majeraha ya kugongwa gari?
Kama hukuwahi kutokewa na matukio kama haya ni bora unyamaze kimya watu wanaumizwa nyie watu.....
Una neno gani juu ya SAGA hii??
Hivi Wananchi tunapokuwa na mashaka na hawa Police nani mwenye dhamana ya kuwachunguza hawa Police!??
Katiba Mpya
Katiba Mpya
Katiba Mpya inahitajika haraka sanaa thamani ya Watanzania haipo!!