Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
TAARIFA YA JESHI LA POLISI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawashikilia wanachama wa CHADEMA ambao ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Aikael Mbowe, Joseph Osmud Mbilinyi Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Pascal Yohana Haonga, Mbunge mstaafu CHADEMA Mbozi Mlowo, Mdude Mpaluka Nyagali, Apolinary Boniface Margwe, Afisa habari CHADEMA na Adam Hassan Kasekwa, mlinzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Pia, Soma: Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi akielekea Mbozi mkoani Songwe
Wengine waliokamatwa ni Paul Joseph Paul, Afisa wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mbeya, Kelvin Keneth Ndabila, Afisa habari Kanda ya Nyasa, mkazi wa Mbeya, Michael Laison Msongole, Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Mbozi, Mlowo, Mohamed Abdilah Ling'wanya, Mlinzi wa Mbowe Mkazi wa Dar es salaam, Alfan Hassan Mbire, mlinzi wa Mbowe na Ezekia Elia Zambi, Mwenyekiti ACT Wazalendo Mkoa wa Songwe.
Tukio hilo limetokea eneo la stendi ya zamani ya Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe Novemba 22,2024 majira ya 10:30 asubuhi baada ya Chama cha CHADEMA kwenda kufanya mkutano wa kampeni eneo ambalo hawakupangiwa na ndipo askari waliwapa amri ya kutawanyika lakini walikaidi ndipo askari waliamua kuwatawanya kwa nguvu na ndipo walipoanza kurusha mawe na kuwajeruhi askari wawili maeneo ya kichwani, usoni na puani na kwa sasa wanaendelea na matibabu hospitali ya Wilaya ya Mbozi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito na kusisitiza kwa Viongozi wa Vyama vyote kutii na kufuata ratiba za kampeni zilizotolewa na Wasimamizi wa Uchaguzi ili kuepusha vurugu ambazo zinaepukika kwa kufuata utaratibu, ili Jeshi la Polisi tuweze kutoa ulinzi stahiki kwa mujibu wa ratiba.
Nitoe tahadhari kwa wananchi pamoja na vyama vya siasa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi na mtu yeyote ambaye atakiuka Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwani vitendo kama hivyo ni kuvunja sheria ili kuvuruga amani, utulivu na usalama katika kampeni zinazoendelea katika Mkoa wetu wa Songwe.