benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Wakati uzinduzi wa Ofisi za Rais Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, ukitarajiwa kufanyika Mei 20 Mwaka huu Serikali imesema serikali imesema inajivunia mchango wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika ujenzi huo, ambao utaandika historia nyingine.
Rais Samia ataingia katika Historia ya Tanzania kwa kuwa Rais wa Kwanza kuhamia na kuanza kutumia Ikulu ya Chamwino Dodoma baada ya kukamilika tangu wimbo wa Serikali kuhamia Dodoma uanze kuimbwa enzi za Hayati Mwalimu Nyerere
Akizungumza jana baada ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, kutoa video fupi kuelekea uzinduzi wa Ikulu mpya, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema kukamilika kwa ujenzi huo, Rais Dk. Samia ameonesha ushujaa.
Msigwa alisema ujenzi wa Ikulu hiyo umekuwa wa kihistoria kutokana na kutumia fedha za ndani, huku vijana wazalendo wa jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakitumika kuufanikisha.
"Ofisi ya Ikulu Dodoma imekamilika...ofisi hii ndiyo ambayo Rais Dk. Samia ataitumia kwa kazi zake za kila siku, tunafahamu Ikulu ya Dar es Salaam ilijengwa wakati wa ukoloni, hivyo hatua ya ujenzi huu kujengwa kwa fedha za ndani kwa kutumia vijana wetu wa JKT na kukamilika hadi kufikia kuzinduliwa mapema mwezi huu, serikali tutaendelea kutambua mchango wa Rais Samia kama shujaa katika kuandika historia hii muhimu," alisema.
Alisema ujenzi huo unakwenda pamoja na ujenzi wa mji wa serikali jijini Dodoma, ambao umefikia asilimia 60 hadi 70, ukiwa ni utekelezaji wa llani ya Uchaguzi ya CCM na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1973 kuhusu serikali kuhamia mkoani humo.