Kukata kodi ya jengo kwenye LUKU, watakaokuwa walipaji wakuu ni wapangaji na si wamiliki tena

Kukata kodi ya jengo kwenye LUKU, watakaokuwa walipaji wakuu ni wapangaji na si wamiliki tena

Ni nyumba ya kiwango gani inapaswa kulipa kodi? Maana kutokana na mradi wa REA hadi mabanda ya nyasi na mbao yana umeme!
Ukiwa na mita ya luku tayari unayo adhi ya kulipa kodi hata ziwe mbavu za mbwa
 
Mbona ni rahisi tu hilo,ukishalipa umeme wako kama kuna kodi ya nyumba inakatwa,ni kumuonyesha tu risiti yako mwenye nyumba mnakuja kukatana kwenye kodi.

mwenye nyumba yupi, hawa wazaramu pasua kichwa wa hapa Dar?
 
Mkuu kuna watu wanakaa nyumba za serikali na zina LUKU, inamaana mtumia luku ndo atalipa hiyo kodi au?
Mkuu kodi itakatwa kupitia mita za Luku- hivi mbona huelewi na vitu ni rahisi-hivi wakiitwa watu wa jinsia ya kiume unashangaa nini wavulana wakienda?
 
Nimegundua udhaifu katika wale walioleta wazo hili lakini zaidi wale wapangaji kwenye nyumba. Ni juzi tu hapa wengi walishangalia kushuka kwa bei za kuwekewa umeme wa single phase kuwa shilingi 27,000, ambazo mwanzoni zilikuwa ni vijijini tu!

Serikali kupitia Tanesco imeamua kufidia upotevu wa mapato kutokana na kuweka usawa katika uwekaji wa single phase mijini! Haikuwa na maana uwekaji wa single phase mjini kuwa aghali kuliko wa vijijini ambapo gharama za uwekaji vijijini zilikuwa kubwa. Single phase installations kwa mijini ilikuwa ni wizi!!!

Sasa imekuwa kila mwenye mita alipe!! Mwisho wa siku wanapata pesa nyingi kwa kusambaza mapato kwa watu wengi!!

Hii haikupaswa hata kuitwa kodi ya nyumba. Ni kodi ya kutumia mita ambacho ni kufaa cha Tanesco!! Na atalipa anayekitumia au anayekilipia.
 
Mita ya LUKU ina jina la mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji, hata kama mpangaji atalipia bado itakuwa ni sehemu ya kodi
Kwa lugha nyingine, kodi yako itapungua kwa kiasi ulicholipia. Pia kodi hii inalipwa mara moja tuu kwa mwaka.
Wenye nyumba hawatapunguza kodi ya pango na mpangaji atalipia kodi ya nyumba kupitia kununua luku.
 
Vitu kama hivi Mwendazake alikua anjichukuliaga credit kwa wananchi kiulainiiii.

Mwigulu muda wa kufikiria vitu vidogo namna hii hana, always anawaza kuendelea kua ndani ya teuzi za Rais tu
Mwigulu hajawahi kuwa na manufaa kwa nchi hii zaidi ya familia yake tu.
 
Mimi sijaelewa kitu,
Naomba mtu mwenye akili timamu anieleweshe kwa upole na kwa hatua,

Kodi ya ardhi analipa mpangaji kupitia LUKU?

Ufafanuzi please.
 
Mimi sijaelewa kitu,
Naomba mtu mwenye akili timamu anieleweshe kwa upole na kwa hatua,

Kodi ya ardhi analipa mpangaji kupitia LUKU?

Ufafanuzi please.
Utamlipa shi ngapi kwa kazi hiyo kubwa uliyoomba? Maana inahitajika mtu mwenye shahada ya uchumi na awe amebobea kwenye diplomasia ya uchumi ili uweze kuelewa.
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.
Sijui yaani mwenye fremu nimlipie Kodi ya jengo MWIGULU anachekesha,sawa
 
Hivi ile hoja ya Luku imepita au kuna mbunge alikuwa na stress za kugombezwa na mkewe sasa akazimalizia kwa kutapika matango pori bungeni?
 
Mwisho wa yote, KODI zote huwa zinalipwa na WALAJI.... wazalishaji ni MABOMBA ya SERIKALI kufyonza KODI kutoka kwa MLAJI.... BADO na BIMA KWA WOTE iingizwe kwenye MABANDO YA SIMU 😀😀 ili kaya zote MILIONI 12 ZIPATE MATIBABU BURE...
 
Uwezo wa viongozi wetu wa kufikiri una walakini. Wananchi masikini wanakwenda kubebeshwa mzigo wa malipo ya kodi ya majengo tena. Nasema hivi kwa kuwa nyumba nyingi wapangaji ndiyo wanaonunua umeme na wala si wamiliki.

Sasa kitendo cha kukata kodi ya pango la jengo kutoka kwenye umeme ni kuwaumiza wananchi masikini wa nchi hii huku wamiliki wa majengo hayo wakiendelea kuchukua kodi zao kama kawaida.

Bajeti mbaya kuwahi kutokea tangu Uhuru.

Kodi kwa maendeleo ya nchi yetu
 
Hii safi Sana, mpaka vijijini tutalipa kodi

Tanzania tax base yetu ni nyembamba sana. Wanaolipa kodi wachache na wanodai huduma za serikali ni karibu watu wote.
Simu nazo zinatupeleka kule kule. Tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu
 
Back
Top Bottom