Duuuh.
Nimekutwa na kadhia kama hiyo mitaa ya kwa Keko, juzi juzi tuu hapo.
Nimezama dukani, kununua maji ya 500. Nikawakuta madada wawili. Mmona nafahamiana naye, alishawahaw kuja ofisini ninapofanyia kazi(stationary).
Baada ya kuwasalimia, nikawapa 5000 wanipe maji ya 500. Yule mdada nisiyemfahamu, akanijibu CHENJI HAKUNA huku akiendelea kuperuz simu yake.
Mdada tunayefahamiana akamwambia yule mdada mwingine, huyo ni mkaka wa pale stationery.
Basi hapa ndo dada wa kwanza, tusiyefahamiana, akapokea ile 5000, akanipa maji ya 500 na kunirudshia chenji.
Nikajiuliza maswali kadhaa, nikasepa!!!
SO HIYO NI ZAIDI YA CHENJI KUTOKUWEPO MZEE.