Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

Lawana ziende kwa maboss hivi kwanini mnasomba pesa yote ya mauzo ya siku husika bila kuacha hata pesa ya chenchi walau elfu50 tu.
 
kwakwel kuna muda suala la chench inakuwaga taabu sana hasa maeneo ya kijijini kilimo kikishaanza ela kuanzia elf2 kushuka chini uwa zinapotea vibaya, unanunua kitu muuzaji atazurula kutafuta chench vibaya, ndio maana mataifa ya walioendelea hawapendagi taabu hii wanatumia malipo ya electronic.
 
mim kuna kipindi miaka ya nyuma nipo Arusha kwenye duka la fadha mdogo duka la vyakula, unakuta asubuhi saa12 mtu anakuja na 10k anataka sabuni ya jamaa ya shilling 400, kumbe anataka chench ya kuacha nyumban na ingine nauli ya daladala, uwa nawaambia sabuni sina na wanaziona
 
Unajua anaweza akawa anafikilia, na wewe umekuja kununua juisi ili tu upate chenchi.

Kuna muda chenchi ni hadimu sana aise, mtu akija na 10000 kununua kitu cha 500 sometime inakata sana maini. unaweza kosa chenchi ya kumpa mtu atakae kuja kununua bidhaa yenye faida zaid ya hio juisi.
Humu wengi waliokomenti huko juu hawana biashara,,Kuna maeneo mengine maduka machache ,,,lkn pia kumuacha mteja ndani ili uvute upande was pili kutafuta chenji Ni risk,,,utaibia soon maana sio maduka yote ndio yenye uzio....

Pia Kuna wateja wengine siwezi kuwauzia anakuja na buku 10 halafu anataka pipi za Mia au Mia 2.... Huyu anataka chenji kijanja TU...
 
Yaani uliambiwa utafute wewe mwenyewe? Duh mimi nilienda kwa mama mmoja anauza samaki, nikampa 10k eti akaanza kujisemesha na mama mwenzie kwa dharau hivi eti "hee mambo ya mwisho wa mwezi hayo hawana hela ndogo" afu wanacheka, i felt bad na sijarudi tena
Mimi ningemwambia nipe hiyo nikupe pesa ndogo akishanipa tuu huyo nasepa bora nikahesabu nyufa za nyumba kuliko dharau hiyo
 
si kila mwenye biashara ni mfanyabiashara mkuu,biashara kipaji ndomana wahindi wanatuacha mbali sana
 
Ni kawaida madogo wakiachiwa maduka. Liuze , lisiuze wao kwao hamna shida
 
Niliwahi kwenda kununua maji.na sh elf 5 nikamwambia muuzaji naomba maji ya 500 alivyoona nampa elf 5 akanijibu Kwa hasira Sina chenji nilishangaa
 
Niliwahi kwenda kununua maji.na sh elf 5 nikamwambia muuzaji naomba maji ya 500 alivyoona nampa elf 5 akanijibu Kwa hasira Sina chenji nilishangaa
Tena sio kwa lugha nzurii [emoji23][emoji23][emoji23] kama vile umeenda kuomba msaada
 
Habarini wana JF,

Juzi kuna jambo limenitafakarisha sana nmeenda dukani haya maduka ya bidhaa za rejareja ni barabaran kuna maduka kadhaa na kuna banda la chips na salon.

Nmefika kwanza nmemkuta muuzaji kijana hivi kwa kukadiria miaka 17 au 18 anachezea simu yupo bize sana ikabidi nimshtue kwa kugonga meza ndo akashtuka na kunisikiliza. Nkamwambia naomba juice ya embe ya elfu moja na maji ya mia tano, nkatoa noti ya Elfu Kumi, huwezi amini dogo alinirudishia pesa akasema sina chenchi broo kanunue kwa maduka mengine.

Nkawa kama sijamuelewa vizuri nikahisi anasema juice hamna wakati naziona kwenye shelfu, nakmuuliza unasema juisi hamna? Akasema broo chenchi sina ila juice ipo kanunue duka lingine tu.

Nlimuangalia sana yule dogo akarudi kukaa na kuendelea kuchezea simu yake. Aisee wenye maduka kuweni makin na hawa vijana wanaowauzia au kama ni ndugu yako umeweka akuuzie kuwa nae makini.

Imenishangaza sana kwa sababu alikua na uwezo wa kutoka kuomba kwa wafanyabiashara wenzake pale nje.
Unasema change..!? Wengine wakikuona umeanza kwa mshindani wake, then ukakosa bidhaa unayoitaka halafu uende kwake, anakutimua
 
Back
Top Bottom