Alafu utalisikia jitu linalalama et biashara ngumu hakuna wateja, kumbe tabia yake ya uvivu na ulegevu kazin ndio inaliponza,
Hii ipo kwa waTanzania wafanyabiashara wengi sana, na sio chenji tu bali hata wepesi wa kumuhudumia mteja watu wengi hii hawana, unamkuta mfanyabiashara anajishauwa anataka umbembeleze wakati pesa yako mwenyewe, nayeye ndie muhitaji wa pesa yako,
mi huwa nikifika madukani nataka muuzaji aoneshe uhitaji na unyenyekevu ama sivyo nitamporomoshea maneno hayo mpaka ajute kufanya biashara,
Na ndio hawa hawa hawakawii kuita wenzao wachawi wakiona wamefanikiwa, kumbe siri iko kwenye namna ya kudili na wateja, unihudumie hovyo na kwa uzembe utegemee nirudi kukuungisha? Sitorudi kamwe, na sitoishia kukupita tu bali nitawashawishi na watu wengine wakukimbie ili ukose wateja akili ikukae sawa ndipo ujuwe wapi unakosea.
Tunahitaji sana Elimu ya biashara haswa kwa hawa wakurupukaji wasiojali wateja.