Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

tufanye ni duka lako hilo, na huyo dogo umemtoa shamba umemweka hapo auze!
We unazani ule muda kutoka dukan na kwenda kutafuta chenchi angeweza kupoteza wateja wangapi ambao wangeitaji huduma yake Kwa muda huo ambao ametoka kutafuta chenchi? Usalama wa bidhaa zake pale dukn angemwachia nani? Kumbuka wateja wasio waaminifu wanaweza vuta baadhi ya vitu vilivyopo dirishani wakavificha wakati muuzaji ameenda kutafuta chenchi
 
Sababu dhaifu sana ukiwa muuza duka kwa mindset hii utakula hasara mapema tuu. Kwahyo siku ambayo wateja wengi wana hela kubwa hautauza
 
Kawaida duka linatakiwa liwe na chenchi muda wote.
Mteja akija apewe chenchi baada ya kununua bidhaa.

Usitoe chenchi kwa wanaokuja nunua vocha za 500 kwa 5000/10000
 
Duka sio lake na mshahara uko pale pale
 
Hawa madogo wanawaharibia sana wenye maduka hii kitu niliwahi kuifikilia sana, hasahasa kwenye maduka ya nguo dogo anakomaa ili apate cha juu matokeo yake watu wanaulizia bei na kuondoka🤔
 
Baba samahani, nimezunguka sana kutafuta change, labda uache hiyo pesa uje baadae, Sina change kabisa. Angalau hii kauli ingemridhisha.
 
Sababu dhaifu sana ukiwa muuza duka kwa mindset hii utakula hasara mapema tuu. Kwahyo siku ambayo wateja wengi wana hela kubwa hautauza
Hata huo uwezo wa kumiliki duka anao basi😂😂😂😂 mtu Mwenyewe kula na kulala anawategemea watu
 
Duuuh.

Nimekutwa na kadhia kama hiyo mitaa ya kwa Keko, juzi juzi tuu hapo.

Nimezama dukani, kununua maji ya 500. Nikawakuta madada wawili. Mmona nafahamiana naye, alishawahaw kuja ofisini ninapofanyia kazi(stationary).

Baada ya kuwasalimia, nikawapa 5000 wanipe maji ya 500. Yule mdada nisiyemfahamu, akanijibu CHENJI HAKUNA huku akiendelea kuperuz simu yake.

Mdada tunayefahamiana akamwambia yule mdada mwingine, huyo ni mkaka wa pale stationery.

Basi hapa ndo dada wa kwanza, tusiyefahamiana, akapokea ile 5000, akanipa maji ya 500 na kunirudshia chenji.

Nikajiuliza maswali kadhaa, nikasepa!!!


SO HIYO NI ZAIDI YA CHENJI KUTOKUWEPO MZEE.
 
Ndio huko kwenu mna mawazo hayo? Kwani unakuwa huuzi?
 
Ni sawa lakin kibiashara inakubomoa, unadhan naweza kuja siku nyingine kununua dukan kwako, kuna watu unampa elf kumi unahitaj bidhaa ya mia tatu anapambana mpka anapata chenchi, anafanya hivo kwa sabab ya kujenga ukarbu na mteja.
Au mpaka mwenyewe unajistukia unamwambia ntaifata badae
 
1. Aliona unamaliza chenji zake.

2. Vile hakujui alikudharau,iweje chenji zitolewe kwa kujuana.
 
wakati wa kufungua duka miongoni mwa vitu vya kuzingatia ni chenchi mkuu!!, fikiria konda akuruhusu ushuke kisha hana chenchi!, natoa mfano wa konda kwa sababu matokeo ya kupoteza wateja kizembe yanaonekana moja kwa moja sasa kwenye duka unaweza usione kama ni mistake lakini ndio mtu naona kama huuzi, kumbe hizi ndogo ndogo unakubali kirahisi ziondoke
 
kuna wateja wakuwakimbia kama ukoma pia. unamaliziwa chenji zote kwa bidhaa za hovyooo. akija mtu na bidhaa ya maana unashindwa kumpa chenchi unaangaika mpka anaondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…