Kukataa kumuuzia mteja bidhaa kisa chenji

Lawana ziende kwa maboss hivi kwanini mnasomba pesa yote ya mauzo ya siku husika bila kuacha hata pesa ya chenchi walau elfu50 tu.
 
kwakwel kuna muda suala la chench inakuwaga taabu sana hasa maeneo ya kijijini kilimo kikishaanza ela kuanzia elf2 kushuka chini uwa zinapotea vibaya, unanunua kitu muuzaji atazurula kutafuta chench vibaya, ndio maana mataifa ya walioendelea hawapendagi taabu hii wanatumia malipo ya electronic.
 
mim kuna kipindi miaka ya nyuma nipo Arusha kwenye duka la fadha mdogo duka la vyakula, unakuta asubuhi saa12 mtu anakuja na 10k anataka sabuni ya jamaa ya shilling 400, kumbe anataka chench ya kuacha nyumban na ingine nauli ya daladala, uwa nawaambia sabuni sina na wanaziona
 
Humu wengi waliokomenti huko juu hawana biashara,,Kuna maeneo mengine maduka machache ,,,lkn pia kumuacha mteja ndani ili uvute upande was pili kutafuta chenji Ni risk,,,utaibia soon maana sio maduka yote ndio yenye uzio....

Pia Kuna wateja wengine siwezi kuwauzia anakuja na buku 10 halafu anataka pipi za Mia au Mia 2.... Huyu anataka chenji kijanja TU...
 
Mimi ningemwambia nipe hiyo nikupe pesa ndogo akishanipa tuu huyo nasepa bora nikahesabu nyufa za nyumba kuliko dharau hiyo
 
si kila mwenye biashara ni mfanyabiashara mkuu,biashara kipaji ndomana wahindi wanatuacha mbali sana
 
Ni kawaida madogo wakiachiwa maduka. Liuze , lisiuze wao kwao hamna shida
 
Niliwahi kwenda kununua maji.na sh elf 5 nikamwambia muuzaji naomba maji ya 500 alivyoona nampa elf 5 akanijibu Kwa hasira Sina chenji nilishangaa
 
Niliwahi kwenda kununua maji.na sh elf 5 nikamwambia muuzaji naomba maji ya 500 alivyoona nampa elf 5 akanijibu Kwa hasira Sina chenji nilishangaa
Tena sio kwa lugha nzurii [emoji23][emoji23][emoji23] kama vile umeenda kuomba msaada
 
Unasema change..!? Wengine wakikuona umeanza kwa mshindani wake, then ukakosa bidhaa unayoitaka halafu uende kwake, anakutimua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…