Kukatika kwa kiungo: Nani anamshauri nani Tanganyika!

Kukatika kwa kiungo: Nani anamshauri nani Tanganyika!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kwenye kabumbu kiungo mchezeshaji akiyumba timu lazima ichezee kichapo ama ifanye vibaya
Maziwa ya ng'ombe yako ya aina mbili, fresh na mtindi.. Ukisikia maziwa yamekatika maana yake sio fresh na sio mtindi

Mbege pia inakatika
Pombe pia inakatika
Hata soda pia.. Ukiifungua haifanyi psii..!
Umeshawahi kuona gari iliyokata center bolt? Inaenda tenge!

Mamlaka, falme na serikali za kibinadamu nazo hukatika.. Yaani kunakosekana muunganiko ndani ya mamlaka kati ya walio juu wao kwa wao ama wao walioko juu na walioko chini

Chemistry ikikataa kwenye formula yoyote lazima mkatiko utokee.. Hata kwenye kufanya ngono lazina movement zi blend! Akienda juu unaendachini, akienda kushoto unaenda kulia simultaneously😀

Sasa haws ndugu zetu naona chemistry yao imegoma kabisa.. Hesabu zimekataa ku tally! Matokeo yake kiungo kimekatika

Wakati hawa wa juu wakiteketeza mamilioni kutafuta picha za "Ku show off" kwamba mambo ni sawa kabisa hawa wachini wanazidi kuharibu kwa kutengeneza muvi za kijinga mno zinazozidi kuwaharibia
Sasa ni wazi kiungo kimekatika.. Kila mmoja ananeng'eneka kivyake! 😀
downloadfile-1.jpg
 
Nani anamdanganya nani hapa? Maji yamelowana.. Mvua imenyeshewa

Hii ni sura ya ulabu ila haijatoa lock bado
 
Hii ni sura ileile ila angalia hilo jicho
 
"Tujitafakari kwa msaada wa SOCRATES wa Tanzania kwa kumsoma na kumsikiliza.
ANAANDIKA ASKOFU BAGONZA

NADHANI TUNAJICHANGANYA?! Au ni Mimi Najichanganya?!

1. SAFARI YA VATICAN

Tungepatana nyumbani kwanza na wawakilishi wa Papa kabla ya kwenda kwa Papa. Tumempiga Padre wake; Tumetengeneza Wakatoliki Vijora; Tunamdhalilisha Kitima, halafu tunaenda kwa Papa. Hatari ipo ya kuambiwa, “Kama hamkumsikiliza Musa na Manabii, hamtaweza kushawishika hata mtu akifufuka”(Luka 16:31). Patana na mshtaki wako kabla ya kwenda kwa Kadhi.

2. MABEBERU:

Tumezoea kuzizodoa nchi za Ulaya kuwa ni mabeberu. Vatican iko Ulaya. Je, Hata Papa ni Beberu? Naye anataka kuchimba Uranium yetu?

3. AMANI YA NCHI

Wizara ya Mambo ya Nje inamuomba Papa aiombee nchi yetu iwe na Amani na Utulivu. Wizara ya Mambo ya Ndani inasema nchi iko salama imetulia. Hawawasiliani? Nani msemaji wa nchi?

4.MARIDHIANO

Wazee wa Chama wanataka Maridhiano. Bunge linasema nchi iko sawa. Tume iko kazini kuchunguza. Nani mkweli? Je kuna ukweli tusioujua hadi tuumulike kwa tochi ya Tume? Je tunataka maridhiano kabla ya ukweli?

5. CHADEMA na CCM

Wapo wanaosema Chadema Imekufa lakini wanaisema kila siku. Huyu ni marehemu mwenye nguvu. Makada wa CCM wanasema CCM tunatamba nayo. Ukiiangalia unaiona ni mfungwa asiye na pingu. Nani zaidi kati ya marehemu anayeishi na aliye hai lakini amekufa?

6. YALIYOTOKEA OKTOBA 29

Siku hii inatusumbua mpaka tunaenda Vatican. Bado kwenda Mecca. Kama waliokufa hawajulikani; waliowaua wanajijua. Dunia inajua makundi yote mawili. Hekima ya WAJALUO inasema, “kuchelewa kwenda kujisaidia, hakuzuii njaa kuuma”. Tukubali: Tuliua, Walikufa; tuombe radhi, tuwajibishane na kusonga mbele.

7. TUNDU LISU

Waliompiga risasi hawajapatikana lakini walioiba michango yake wamekamatwa. Yeye yuko rumande. Mahakama imeenda likizo na haki yake iko likizo. Fikiria daktari akienda kupumzika katikati ya operesheni mgonjwa?!

8. WIZARA YA MAMBO YA NJE

Hii Wizara inaonyesha tuko vitani. Kimsingi ina mawaziri 4: Kombo, Kabudi, Nyalandu na JK. Msiniulize JK ni nani maana mtamuona anatumwa katika masuala magumu nje. Waliobaki 3 na manaibu 2, wanaunda kikosi kazi cha mawaziri wa wizara. Msiniulize nani ni Boss maana Kabudi anaweza kujikuta ni Naibu Waziri. TUNAJIKANYAGA MNO.

9. Taifa likiwa katika mtifuano kama tulio nao, linakuwa kama mgonjwa. Hawezi kwenda kwa daktari akagoma kuvua nguo. Tuvue zote na madaktari watuingizie vidole kila mahali ili kubaini ugonjwa ulipo ndipo tutibiwe.

Wajaluo wakibanwa TEZI DUME husingizia wanaumwa kichwa.
Sasa Wajaluo wa TEZI JIKE hao usiseme"

Maneno ya professor Anna Tabaijuka
1769696603842.jpg
 
Kwenye kabumbu kiungo mchezeshaji akiyumba timu lazima ichezee kichapo ama ifanye vibaya
Maziwa ya ng'ombe yako ya aina mbili, fresh na mtindi.. Ukisikia maziwa yamekatika maana yake sio fresh na sio mtindi

Mbege pia inakatika
Pombe pia inakatika
Hata soda pia.. Ukiifungua haifanyi psii..!
Umeshawahi kuona gari iliyokata center bolt? Inaenda tenge!

Mamlaka, falme na serikali za kibinadamu nazo hukatika.. Yaani kunakosekana muunganiko ndani ya mamlaka kati ya walio juu wao kwa wao ama wao walioko juu na walioko chini

Chemistry ikikataa kwenye formula yoyote lazima mkatiko utokee.. Hata kwenye kufanya ngono lazina movement zi blend! Akienda juu unaendachini, akienda kushoto unaenda kulia simultaneously😀

Sasa haws ndugu zetu naona chemistry yao imegoma kabisa.. Hesabu zimekataa ku tally! Matokeo yake kiungo kimekatika

Wakati hawa wa juu wakiteketeza mamilioni kutafuta picha za "Ku show off" kwamba mambo ni sawa kabisa hawa wachini wanazidi kuharibu kwa kutengeneza muvi za kijinga mno zinazozidi kuwaharibia
Sasa ni wazi kiungo kimekatika.. Kila mmoja ananeng'eneka kivyake! 😀View attachment 3535687View attachment 3535688
Unaamua kwa dhamira yako kuua watu ambao unatakiwa uwaongoze wewe; halau ukishamaliza hiyo kazi ya kuua unahangaika saaana kiasi hiki cha kufanya ulaghai na utapeli.
Wewe ni kiongozi mwenye akili kichwani mwako kweli?
 
Huo ujumbe toka kwa Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Papa ; naona bahasha ya kaki hapo mezani yenye ujumbe huo.
Sasa najiuliza, kama ndani yake kuna maelezo yoyote kuhusu yule Padre Kitima waliyetaka kumaliza maisha yake, hao hao wanaopeleka ujumbe.

Samia Suluhu Hassan anazo tabia zile zile zinazojulikana kuwa watu wauaji (serial killers) huwa wanazo.

Samia ni 'serial killer'. asiyeshtushwa na uovu wowote.
 
Huo ujumbe toka kwa Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Papa ; naona bahasha ya kaki hapo mezani yenye ujumbe huo.
Sasa najiuliza, kama ndani yake kuna maelezo yoyote kuhusu yule Padre Kitima waliyetaka kumaliza maisha yake, hao hao wanaopeleka ujumbe.

Samia Suluhu Hassan anazo tabia zile zile zinazojulikana kuwa watu wauaji (serial killers) huwa wanazo.

Samia ni 'serial killer'. asiyeshtushwa na uovu wowote.

View: https://www.facebook.com/share/v/1FCTmDg2rz/
 
KWI KWI KWI
Kanisa Katoliki si jukwaa la maigizo ya kisiasa wala taasisi inayoweza kushughulikiwa kwa mbinu za mkato. Ni taasisi ya kale yenye sheria zake (Canon Law), nidhamu ya juu, na muundo wa ki-hierarchical unaoheshimika duniani kote.

Maamuzi, mawasiliano na mahusiano yake hufuata taratibu zilizoainishwa wazi na zinazotambulika kimataifa.
 
KWI KWI KWI
Mkulima kala mbegu anataka kutuua njaa

Hawa wanasema wameuza kubalance mizania eti labda itashuka bei...sijawahi kuona Gold ikishuka thamani

Serikali na Wabuge huko Dodoma wanabwajaja wanasema wameuza kufadhili miradi ya maendeleo ya kimkakati.

Which is which? ..
Tumuamini nani?..
Who is who...? May be who are you!
 
Baba aendelea kuuliza NI Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD
DHAHABU: Wasemaji Wengi Wanasababisha Wakosoaji Wengi.

Tabia ya kufichaficha mambo, inasababisha serikali kujikanyaga na kutoa matamko yanayokinzana. “Matamko-mgongano” yakiwa mengi, yanasababisha wasemaji na wazushi wengi kama ilivyo sasa. Ebu ona hili la kuuza RIZEVU/NYANTAKOLWAKOLWA yetu ya dhahabu ;

1. Mara Benki Kuu iseme “Reserve Haiuzwi” na kwamba watu wanazusha.

2. Baadaye inasema itauzwa kidogo tu iliyozidi. Na baadaye tena inasema itauzwa sehemu lakini si kulipia miundombinu.

3. Mtumishi mwingine wa Benki Kuu analiambia kundi la Whats up kwamba zitauzwa kulipia miradi ya Miundombinu lakini watanunua nyingine kwa sababu zipo!

4. Wizara ya Uwekezaji inanukuliwa na vyombo vya habari vya nje kuwa “Rais ameamua dhahabu ziuzwe kwa sababu bei ni nzuri kwa sasa”,

5. “Machawa wetu” huko bungeni wanasema dhahabu zitauzwa na muuzaji asisikilize maoni ya wananchi wanaoitwa wanaharakati.

6. Yote haya, hayakanushi ukweli kuwa AKIBA YA DHAHABU ITAUZWA. Dhahabu ni mali ya BOT; na BOT ni mali ya serikali; na serikali ni mali ya wananchi (hili sina uhakika sawasawa).

SASA

7. Mwaka jana liliibuka timbwili. Serikali ikauza “shares” zake za makaa ya mawe. Kampuni iliyonunua ikaziweka sokoni Australia. Mtanzania mmoja akaenda akazinunua. Sisi wenye fitna tukamrukia na kumwita majina yote mabaya. Alikosea wapi? Yaani unamwacha mke halafu hutaki aolewe tena?! Roho mbaya, Shingo feni.

8. Je, tukiuza akiba ya Dhahabu. Akatokea Mjaluo anayefanya kazi BOT. Akauza wake zake na kamongo wote ziwani, akazinunua; tukimjua tumsalie Novena au Albadir? Na huyo mtu akijikuta ana hazina ya dhahabu kubwa kuliko BOT, hatatuchagulia tulale na kuamka saa ngapi?

9. Uuzwaji huu wa RIZEVU ya dhahabu uliokuja ghafla kama hekima ya Wajaluo, ukija kugeuka kuwa KAGODA, IPTL, na Escrow nyingine, tuanze kuitana tumbili tena?

USHAURI WANGU:

a) Nenda pole pole. Haraka ya Bandari imetufikisha wapi?

b) Kuwe na Msemaji mmoja wa serikali. Kuwatumia wasanii kwa mambo nyeti ni kuidhalilisha serikali yetu hata kama inajifanya siyo yetu.

c) Bunge lijikite kuisimamia serikali siyo kuwasema wana harakati. Mishahara yao hailipwi kutoka mifuko binafsi ya wana harakati.

d) Ongeza uwazi. Dhahabu si madawa ya kulevya. Mambo ya siri na ya gizani, yalimsababisha Mjaluo amuoe kibogoyo aliyemposa gizani.

e) Kubali ukweli: Kwamba, kutikisa RISEVU yetu kutatikisa shilingi yetu. Msiposema na ikatikisika, tusianze kutekana tutakapoanza kuwazodoa. Tajiri asiye na RISEVU ni maskini kuliko maskini wa kipato mwenye RISEVU.

Wajaluo mmenielewa?
1769868322883.jpg
 
Back
Top Bottom