Kukatika kwa kiungo: Nani anamshauri nani Tanganyika!

Kukatika kwa kiungo: Nani anamshauri nani Tanganyika!

1769868277107.jpg
 
‪Umewahi kusikili habari za Mnara wa Babeli? ‬

‪“Tunataka tuendelee na jambo hili la kununua dhahabu hata iwe nyingi, nyingi, nyingi, na nyingi hadi tulingane na mataifa mengine ambayo yalishanunua dhahabu. Ni kawaida dhahabu kuuzwa ili Serikali kugharamia miradi yake mikubwa” – MADURO‬

‪ “Misaada ya nje imepungua, nchi nyingi hazitoi tena misaada, tunahitaji njia mbadala za kupata fedha. Serikali imepanga kuuza sehemu ya akiba yake ya dhahabu ili kupata fedha za kusaidia kufadhili miradi mbalimbali ya miundombinu.” — KITILA. ‬

‪“Benki Kuu ina akiba ya dhahabu ya $3.24 bilioni imevuka lengo la bodi na imeamua kuuza dhahabu ya $1.2 bilioni ili kuweka mizania sawa ya $2 bilioni. Ni utaratibu wa kawaida wa Benki Kuu kuweka mizania sawa ya vihatarishi” – Benki Kuu ya Tanzania.‬

‪Anyways, tuachane na mbogamboga, tujadili hoja za BoT.‬

‪Benki kuu nyingi hutumia dhahabu kama mali ya kimkakati ya akiba kwa sababu ina thamani inayokubalika kimataifa na haiathiriwi moja kwa moja na sera za nchi nyingine. Ndiyo maana wanatunza akiba.‬

‪UZBEKISTAN wana akiba ya dhahabu $67 bilioni. TAIWAN $75 bilioni. KAZAKHSTAN $59 bilioni. BoT wanasema limit yao ni $2 bilioni na wameshavuka malengo na wako $3.24 bilioni, hivyo hawaoni shida kuuza ziada. TAMAA.‬

‪BoT, akiba ya dhahabu iliyopo haijaiweka nchi yetu katika orodha ya nchi 20 zenye akiba ya dhahabu, hilo lengo la kuwa na akiba ya $2 bilioni mnajipima na nani? Maana Tanzania hatupo hata katika orodha ya nchi 10 Afrika.‬

‪Akiba ya dhahabu LIBYA $92.9 bilioni. ALGERIA ($83.0 billion). SOUTH AFRICA ($65.4 billion). EGYPT ($44.9 billion). NIGERIA ($38.6 billion). MOROCCO ($371 billion). ANGOLA ($14.2 billion). Hawauzi akiba ya dhahabu.‬

‪Unavukaje malengo katika akiba? Unavuka malengo katika mapato. Una akiba $3.24 bilioni na unauza ⅓ ya akiba yako? KENYA, akiba yao ya dhahabu ni $10.1 billion. Je, hawajui kuweka mizania sawa ya vihatarishi?‬

‪Tanzania ina akiba ya ya $3.24 bilioni na wanaona kwamba watashindwa kujishikilia na akiba ya tani 6 ya dhahabu, wameamua kuuza dhahabu ya $1.2 bilioni kubaki na akiba $2 bilioni. MADURO anasema ni SERA‬

‪Hizo tani 6 za akiba ndiyo mmeingia tamaa mnaanza kuuza wakati ALGERIA wanazo tani 173 katika akiba ya dhahabu na hawajauza? Badala ya kuweka akiba ya kutosha, ninyi mnaanza kuingia tamaa. Acheni tamaa‬

‪Benki kuu nchi zote timamu zina akiba ya fedha za kigeni kwa ajili ya kulinda uchumi wao na sarafu zao. Dhahabu ni sehemu ya akiba hiyo kwa sababu za kimkakati. BoT wao wanasema wanauza dhahabu ili kununua DOLA. ‬

‪Dhahabu ni “safe haven” – yaani kwamba, ni mali ambayo hukimbiliwa wakati kuna hofu ya uchumi, mfumuko wa bei (inflation), au Wakati kuna migogoro au wasiwasi kuhusu nguvu ya sarafu kama dola ya Marekani‬

‪Mahitaji ya dhahabu huongezeka na mara nyingi bei yake hupanda. Dhahabu inaongezeka thamani. Ninyi mnauza akiba ya dhahabu kwa kuwa tu mmefikia lengo la bodi ya BoT. Nyieee! Labda mtueleze jikoni mmekaukiwa..‬

‪Dhahabu ni store of value. Kitu kinachoweza kuhifadhi thamani kwa muda mrefu bila kupoteza uwezo wake wa kununua bidhaa au huduma. Imetumika hivyo kwa maelfu ya miaka. Badala ya kuhifadhi, mmeamua kuuza akiba‬

‪Ushauri timamu ungelikuwa…‬

‪Madini ya dhahabu yasitokewe nje kwa magendo. Masoko ya uhakika. Serikali inunue madini kwa wachimbaji wadogo na wakubwa na kuuza nje. Mifumo iwe rafiki bila ukiritimba wa soko (state monopoly)‬

‪Masoko yatasaidia wachimbaji wadogo kupata wanunuzi wa uhakika, bei iliyo wazi, na malipo salama. Masoko yatasaidia serikali kufuatilia uzalishaji halisi. Hii itapunguza uharamia na kuongeza ukusanyaji wa kodi.‬

‪Nchi timamu zote zinaweka masoko ya wazi na yenye ushindani, kuwezesha wachimbaji kupata bei inayolingana na soko la dunia. Masoko shindani hupunguza walanguzi/wanunuzi wachache kudhibiti bei. ‬

‪Rahisisha leseni na kodi kwa wachimbaji wadogo, ongezeni usimamizi wa mipaka ili kupunguza magendo, na kutumia sehemu ya dhahabu kuongeza akiba badala ya kuuza. Hizo nyingine mnatupiga porojo tu. ‬

‪But What Do I Think I Know?‬
Credit: Martin Maranja Masese FB
1769903507988.jpg
1769903504612.jpg
 
Back
Top Bottom