gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 825
- 1,519
Ikiwa unadhani kwamba kukatika kwa umeme nchi nzima kulikotokea lao tarehe 27 June saa 1 kamili usiku ni hitilafu ya kawaida ya mitambo ya kufua umeme utakuwa umekubali kudanganyika kirahisi mno. Kuzima umeme nchi nzima kamwe hakuwezi kuwa ni tukio la bahati mbaya wala kuhusianishwa na tangazo lililotolewa na shirika la Tanesco kwamba kuna hitilafu katika gridi ya taifa.
Kwa sasa taifa la Tanzania limekumbwa na mtanzuko mkubwa na serikali iliyopo madarakani ikihaha kuzuia upepo wa maandamano ya tarehe 7 mwezi wa 7. Zipo mbinu kadhaa za kijasusi zitakazotumika na zinazoendelea kutumika ikiwemo kukatwa kwa umeme nchi nzima.
Kwanza, umeme ukikatwa utalegeza nguvu ya mitandao ya mawasiliano kwa simu kuisha chaji na mitandao ya simu kushindwa kurusha matangazo. Ni njia ya uhujumu isiyo wazi. Kwakuwa minara baada ya kukatwa kwa umeme itatutumia nguvu ya jenereta za mafuta ambayo ni ghali na adimu kwa sasa, kukatwa umeme kwa muda mrefu kutazuia kusambazwa kwa ufanisi kwa mtandao wa intanenti.
Pili, ikiwa wana usalama watahitaji kusambazwa vifaa ikiwemo silaha na magari ya kuzuia maandamano pamoja na askari basi wangependa kufanya jambo hilo kwa siri bila kutambulika, njia ya kukata umeme nchi nzima itawanufaisha wao kuweza kutekeleza mipango yao miovu.
Tutu, ikiwa wanausalama wapo katika msako mkali wa kuwakamata wale wanaoitwa vinara wa maandamano na kuwapoteza kisha kusingizia watu wasiojulikana, basi wangependa kufanya operesheni zao kimya kimya na kwa usiri mkubwa. Uwepo wa kiza totoro nchi nzima utarahisisha mambo yao, hivyo usijekushangaa kwamba baada ya umeme kurudishwa ukasikia visa kadhaa vya watu waliopotea na wasijulikane walipo.