Kukatika kwa umeme nchi nzima ni mbinu ya kupooza maandamano ya July 7

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
825
Reaction score
1,519
Ikiwa unadhani kwamba kukatika kwa umeme nchi nzima kulikotokea lao tarehe 27 June saa 1 kamili usiku ni hitilafu ya kawaida ya mitambo ya kufua umeme utakuwa umekubali kudanganyika kirahisi mno. Kuzima umeme nchi nzima kamwe hakuwezi kuwa ni tukio la bahati mbaya wala kuhusianishwa na tangazo lililotolewa na shirika la Tanesco kwamba kuna hitilafu katika gridi ya taifa.

Kwa sasa taifa la Tanzania limekumbwa na mtanzuko mkubwa na serikali iliyopo madarakani ikihaha kuzuia upepo wa maandamano ya tarehe 7 mwezi wa 7. Zipo mbinu kadhaa za kijasusi zitakazotumika na zinazoendelea kutumika ikiwemo kukatwa kwa umeme nchi nzima.

Kwanza, umeme ukikatwa utalegeza nguvu ya mitandao ya mawasiliano kwa simu kuisha chaji na mitandao ya simu kushindwa kurusha matangazo. Ni njia ya uhujumu isiyo wazi. Kwakuwa minara baada ya kukatwa kwa umeme itatutumia nguvu ya jenereta za mafuta ambayo ni ghali na adimu kwa sasa, kukatwa umeme kwa muda mrefu kutazuia kusambazwa kwa ufanisi kwa mtandao wa intanenti.

Pili, ikiwa wana usalama watahitaji kusambazwa vifaa ikiwemo silaha na magari ya kuzuia maandamano pamoja na askari basi wangependa kufanya jambo hilo kwa siri bila kutambulika, njia ya kukata umeme nchi nzima itawanufaisha wao kuweza kutekeleza mipango yao miovu.

Tutu, ikiwa wanausalama wapo katika msako mkali wa kuwakamata wale wanaoitwa vinara wa maandamano na kuwapoteza kisha kusingizia watu wasiojulikana, basi wangependa kufanya operesheni zao kimya kimya na kwa usiri mkubwa. Uwepo wa kiza totoro nchi nzima utarahisisha mambo yao, hivyo usijekushangaa kwamba baada ya umeme kurudishwa ukasikia visa kadhaa vya watu waliopotea na wasijulikane walipo.
 
Kama ndio lengo hilo basi hatuna viongozi huko Malawi....

Hivi hao viongozi wenu ni kwanini wasiwasikilize na kutatua wanachodai? Hivi ukiwajibika au kujiondoa unapata hasara gani? Tukumbuke hakuna kiumbe chenye pumzi kitakacho ishi milele hata kama watadhulumu uhai wa wengine ipo siku isiyo na jina Kila mmoja ataondoka kwa namna yake....

Embu viongozi wenu wa Malawi wajitafakari, kaeni nao wasikilizeni kwa manufaa ya mioyo ya wengi
 
Unazani rahisi kuzima Grid ya Taifa ya umeme, siasa uchwara ndiyo hizo sasa.

Hizo tuhuma zako zote zinakosa mashiko jifunze kuwa serious kwa vitu nyeti.

Siasa siyo uadui bali kwa mustakabali mpana wa Tanzania iliyo bora leo na kesho pia.
 
Walizima internet nchi nzima, chawa endelea kujitoa akili
 
Unazani rahisi kuzima Grid ya Taifa ya umeme, siasa uchwara ndiyo hizo sasa.

Hizo tuhuma zako zote zinakosa mashiko jifunze kuwa serious kwa vitu nyeti.

Siasa siyo uadui bali kwa mustakabali mpana wa Tanzania iliyo bora leo na kesho pia.
Wewe unadhani ugumu uko wapi ili watu wajifunze kuwa siriazi na vitu nyeti na wajue kwamba siasa siyo uadui?
NB:Unabishana hata na TANESCO waliotoa tangazo lao kwamba umeme ulikatika kutokana na hitilafu waliziziainisha unataka uaminike wewe?
 
Umeme ulipokatwa zilee coaster nyeupe SU na Yutong za kijani zimepga kazi sana sio nawatia uoga sasa jichanganye hakuna simile
Shaba zitalia sanaa
 
Wewe na Samia mtaishi milele hamtakufa.
 
Unazani rahisi kuzima Grid ya Taifa ya umeme, siasa uchwara ndiyo hizo sasa.

Hizo tuhuma zako zote zinakosa mashiko jifunze kuwa serious kwa vitu nyeti.

Siasa siyo uadui bali kwa mustakabali mpana wa Tanzania iliyo bora leo na kesho pia.
Walizima internet ambayo ni engine ya maisha ya watu Kwa sasa sembuse umeme Kuna backup ya generators na solar? Punguza ujinga think big!
 
Siasa sio uadui? Ccm wanaziweza Siasa za hoja?
 
Ikiwa unadhani kwamba kukatika kwa umeme nchi nzima kulikotokea lao tarehe 27 June saa 1 kamili usiku ni hitilafu ya kawaida ya mitambo ya kufua umeme utakuwa umekubali kudanganyika kirahisi mno. Kuzima umeme nchi nzima kamwe hakuwezi kuwa ni tukio la bahati mbaya wala kuhusianishwa na tangazo lililotolewa na shirika la Tanesco kwamba kuna hitilafu katika gridi ya taifa.

Kwa sasa taifa la Tanzania limekumbwa na mtanzuko mkubwa na serikali iliyopo madarakani ikihaha kuzuia upepo wa maandamano ya tarehe 7 mwezi wa 7. Zipo mbinu kadhaa za kijasusi zitakazotumika na zinazoendelea kutumika ikiwemo kukatwa kwa umeme nchi nzima.

Kwanza, umeme ukikatwa utalegeza nguvu ya mitandao ya mawasiliano kwa simu kuisha chaji na mitandao ya simu kushindwa kurusha matangazo. Ni njia ya uhujumu isiyo wazi. Kwakuwa minara baada ya kukatwa kwa umeme itatutumia nguvu ya jenereta za mafuta ambayo ni ghali na adimu kwa sasa, kukatwa umeme kwa muda mrefu kutazuia kusambazwa kwa ufanisi kwa mtandao wa intanenti.

Pili, ikiwa wana usalama watahitaji kusambazwa vifaa ikiwemo silaha na magari ya kuzuia maandamano pamoja na askari basi wangependa kufanya jambo hilo kwa siri bila kutambulika, njia ya kukata umeme nchi nzima itawanufaisha wao kuweza kutekeleza mipango yao miovu.

Tutu, ikiwa wanausalama wapo katika msako mkali wa kuwakamata wale wanaoitwa vinara wa maandamano na kuwapoteza kisha kusingizia watu wasiojulikana, basi wangependa kufanya operesheni zao kimya kimya na kwa usiri mkubwa. Uwepo wa kiza totoro nchi nzima utarahisisha mambo yao, hivyo usijekushangaa kwamba baada ya umeme kurudishwa ukasikia visa kadhaa vya watu waliopotea na wasijulikane walipo.
pure nonsense 🐒
 
Wewe unadhani ugumu uko wapi ili watu wajifunze kuwa siriazi na vitu nyeti na wajue kwamba siasa siyo uadui?
NB:Unabishana hata na TANESCO waliotoa tangazo lao kwamba umeme ulikatika kutokana na hitilafu waliziziainisha unataka uaminike wewe?
Watu wakifanya mambo kulingana na miongozo na si kukurupuka kwa siasa za matukio na kuona hata jambo la Grid ya Taifa kuanguka imekuwa jukwaa lenu la siasa.

Sijabishana na TANESCO bali aliyetoa hoja ya vitendo vinavyoendelea kwa ukosefu wa umeme ndiyo amepinga ukweli kwa siasa uchwara zake.
 
Walizima internet ambayo ni engine ya maisha ya watu Kwa sasa sembuse umeme Kuna backup ya generators na solar? Punguza ujinga think big!
Ukiacha fikiria kila tukio ni hujuma utakuwa na fikra nzuri za kupiga hatua.

Shughulisha fuvu hilo siyo kuingiza siasa hadi kwenye taaluma nyeti.

N.k
Hayo matukio ya awali yalikuwa na sababu za kufanya hivyo kulingana na wakati uliokuwepo.

Nchi haijengwi kwa blah blah bali mikakati thabiti.
 
Siasa sio uadui? Ccm wanaziweza Siasa za hoja?
CCM wanaziweza vizuri shida ipo kwenye maslahi mbele kwa wengi wao ndiyo maana unaona leo kwenye korido zao ni kulilia vyeo tu na si kukipigania chama.

Uzalendo wa kuigiza huku wenzio wananeemeka ndiyo wanashindwa wanaCCM kwa sasa lakini ndani yake kuna wenye hoja nzuri tena zenye mashiko.
 
Jana usiku mida ya saa 4 kwenda saa 5 maeneo y ufundi mpaka bandari ya mizigo nilikutana na gari nyingi sana za polisi zile za maji kuwasha n za kubeba polisi ni kama zilikuwa zinaweka wese pale sheli ya puma ufundi kishazinaondoka.. kiufupi mambo sio shwari.. ova
 
Back
Top Bottom