hatukubali
Lowassa ameonewa kabisa,huyu bwana anafanya siasa za kimataifa kabisa kama marekani,tunaona wagombea wa urais marekani wanaanza harakati zao ndani ya chama muda mrefu sana na kujiandaa vyema...lakini kwa ccm siyo.yaani unamtaka yule ambaye atawafumbia macho....katika kundi hilo waote pale maamuzi yao yanatabirika....lowasa pekee ndiye alikuwa maamuzi magumu ambayo wakuu wa ccm hawapendi.....
Namshauri Lowassa.....nenda upinzani hasa Ukawa maana wana fremwork saffi.....ushinde urais...utapata kura za kumwaka ambazo watashindwa kuiba.
Kwani itaisha saa ngapi ama lini ili na mimi niagize maji ya kandoro na mahindi ya kuchoma ya kutosha pamoja na ndimu na chumvi ya pilpili.Niletee zile pop corn za sukari..........halafu na candy floss..........hii movie ndefu sana........
Walioimba ufisadi wa Lowassa ni CCM.
Mara kuvua gamba, n.k.
Sikumbuki popote Wapinzani walipomtaja Lowassa kuwa ni fisadi.
Ufisadi ndani ya Chama cha Mapinduzi ni MFUMO RASMI.
UKAWA wasipompokea Lowassa, maana yake ni kwamba hawataki kuuondoa madarakani mfumo wa ufisadi.
Tatizo letu ni mfumo, siyo watu au majina ya watu.
Kama kweli Ukawa wanaitakia mema nchi yetu, basi naamini wako kwenye kikao na Lowassa hivi sasa.
Mungu ibariki Tanzania.
Pasco wewe kweli ni mpiganaji unayeona mbaliWanabodi,
Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?!.
Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?!.
Pasco
membe ni muislam, magufuli ni muislam?
hatukubali
Ugonjwa wa mtu anaujua yeye mwenyewe na daktari wake. Yeye kesha sema kuwa yuko fit, na hakuna daktari aliyejitokeza kutamka kuwa Lowasa ni mgonjwa wewe na wenzako hiyo huruma yenu imetokea wapi?
Hapo ni mdumange tuu lazima muucheze.
Wanabodi,
CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.
Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?
Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?
Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?
Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?
Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?
Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?
Pasco!
Kwa bandiko hili ndipo utaona kuwa ccm ni chaka la wahalifu na wanalazimishwa daima wasikemee uhalifu kwa kigezo cha kufilisiwa.kama lowassa anafikiri watanzania wengi wanampenda ahame chama ndipo atajua hasira za watanzania juu yake,aling'ang'ania ccm kwa sababu alijua ni chama chenye dola atashinda kwa mbinu zote hata kwa goli la mkono lakini nje ya ccm hana nguvu zozote na akitoka kamati ya maadili ya ccm itamfungia kazi mwisho wake ataishia gerezani au kufilisiwa kabisa pia nawapa pole wapambe wake ndio wajue rais hachaguliwi kihuni kama walivyofikiri
Hivi mnapata faida gani kupotosha uko shule mlikwenda kusoma nini ujinga?Nyerere aliwahi kusema ni heri mbuzi kuwa mgombea wa CCM kuliko mkristo kuwa raisi wa Tanzania, hii imetimia. Majina yote 5 yaliyo chaguliwa CCM ni uislam mtupu. Tumechoshwa ni team uislam ndani ya CCM, mahamuzi magumu yanaitajika sasa.