Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

KUTOKA DODOMA 4U MOVEMENT
TANGAZO:
Tunawatangazia kwamba kufikia saa nne kamili asubuhi kwa wana 4U ambao si wa NEC wala wajumbe wa mkutano mkuu wawe wameshakabidhi vyumba katika hotel walizofikia, Pia wale wajumbe wa NEC na mkutano mkuu 4U hatutaendelea kugharamia uwepo wenu hapa dodoma!

Mwisho:
Hakutakuwa na usafiri wa mabasi yetu kuwarudisha wale wana 4U huko mikoani kila mtu atajigharamia.
asante
Mr Hemed Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
4U Movement | FRIENDS OF LOWASSA
 
Poleni sana 4U movement. Ilikuwa mshangilie ushindi lakini ndio basi tena!
 
Lowassa ameonewa kabisa,huyu bwana anafanya siasa za kimataifa kabisa kama marekani,tunaona wagombea wa urais marekani wanaanza harakati zao ndani ya chama muda mrefu sana na kujiandaa vyema...lakini kwa ccm siyo.yaani unamtaka yule ambaye atawafumbia macho....katika kundi hilo waote pale maamuzi yao yanatabirika....lowasa pekee ndiye alikuwa maamuzi magumu ambayo wakuu wa ccm hawapendi.....

Namshauri Lowassa.....nenda upinzani hasa Ukawa maana wana fremwork saffi.....ushinde urais...utapata kura za kumwaka ambazo watashindwa kuiba.

Sasa marekani ndio bongo?
 
Niletee zile pop corn za sukari..........halafu na candy floss..........hii movie ndefu sana........
Kwani itaisha saa ngapi ama lini ili na mimi niagize maji ya kandoro na mahindi ya kuchoma ya kutosha pamoja na ndimu na chumvi ya pilpili.
 
Walioimba ufisadi wa Lowassa ni CCM.
Mara kuvua gamba, n.k.

Sikumbuki popote Wapinzani walipomtaja Lowassa kuwa ni fisadi.
Ufisadi ndani ya Chama cha Mapinduzi ni MFUMO RASMI.
UKAWA wasipompokea Lowassa, maana yake ni kwamba hawataki kuuondoa madarakani mfumo wa ufisadi.
Tatizo letu ni mfumo, siyo watu au majina ya watu.
Kama kweli Ukawa wanaitakia mema nchi yetu, basi naamini wako kwenye kikao na Lowassa hivi sasa.
Mungu ibariki Tanzania.

Mwaka 2007 Mwembe Yanga Dk Will broad Slaa katika orodha alitoitaja ya mafisadi papa maarufu kama list of shame jina la Lowassa lilikuwemo,ulikuwa wapi mkuu?

Lowassa ni mmoja wa waliotishia kwenda kufungua mashtaka hadi Leo hajaenda
 
Wanabodi,
Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?!.
Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?!.
Pasco
Pasco wewe kweli ni mpiganaji unayeona mbali
ukiacha hii ya kumpigania Lowasa zaidi ya iaka 3 nyuma bado uliliona hilo ndilo Jiwe walilolikataa waashi.
fununu za sasa hivi ni kuwa jamaa yako Membe ndio Rais sasa sijui km ataibeba CCM yote?
Mchujo wa 3 Bora Makamba na Magufuli watakatwa (yaani bora hata wangemuachia Magufuli asonge angeweza pambana na Dr Slaa)
Watakaoingia 3 ni kina Mama na Membe
Mkutano utamalizika jioni hiii kwa Membe kupeperusha bendera
CCM kazi ipo, kumnadi mgombea mwenye Mawaa kz ipo
la sivyo tutegemee UTABIRI WAKO au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?!.
 
Hakuna cha Safari ya matumaini wala nini hapa, Lowassa ni fisadi na CCM wasingeweza kumpitisha fisadi. Kama CCM wenyewe wameliona hilo, unafikiri upinzani watampokea huyu jamaa? Sina hakika kama ukawa watampokea huyu fisadi na kumpa nafasi ya kuipeperusha bendera yao kwenye uchaguzi mkuu. Inawezekana kabisa huu ni mwisho wa safari za Lowassa kisiasa. Sana sana kitu mimi nafikiria Team Lowassa watafanya ni Sabotage. Watapiga kura Ukawa, ingawa watabakia CCM. Na wakifanya hivyo sisi ndio furaha yetu, kwani tunataka mabadiliko, Ukawa wachukue nchi, CCM ikae pembeni. Huu ndio mwanzo wa kifo cha CCM.
 
Huu ndio mwisho wa jina CCM (chama cha majambazi ) kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania
 
hatukubali

Pole sana kwani alikuahidi cheo gani? Uwaziri, ukuu wa mkoa au wilaya? Hata hivyo afadhali tu maana serikali yote ingejaa wapambe wake ambao pia wangeajiri wafanayakazi ndugu zao na hivyo tungekuwa na serikali aina ya " Oligarchy".
 
Pasco ungepumzika for now
sioni kama una make sense anymore
kila ulichotuambia huko nyuma kimeenda the opposite
labda sasa ungenyamaza kwanza.......ni kama vile nyinyi wapambe wa mgombea
mna kiu na urais kuliko mgombea mwenyewe
Mkuu naona leo unambana Pasco kila ikikatiza unaye tu.

Teh Teh teh
 
Last edited by a moderator:
kama lowassa anafikiri watanzania wengi wanampenda ahame chama ndipo atajua hasira za watanzania juu yake,aling'ang'ania ccm kwa sababu alijua ni chama chenye dola atashinda kwa mbinu zote hata kwa goli la mkono lakini nje ya ccm hana nguvu zozote na akitoka kamati ya maadili ya ccm itamfungia kazi mwisho wake ataishia gerezani au kufilisiwa kabisa pia nawapa pole wapambe wake ndio wajue rais hachaguliwi kihuni kama walivyofikiri
 
Ugonjwa wa mtu anaujua yeye mwenyewe na daktari wake. Yeye kesha sema kuwa yuko fit, na hakuna daktari aliyejitokeza kutamka kuwa Lowasa ni mgonjwa wewe na wenzako hiyo huruma yenu imetokea wapi?
Hapo ni mdumange tuu lazima muucheze.

Ukisoma huelewi basi hata picha huoni?
 
Wanabodi,

CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.

Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?

Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?

Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?

Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?

Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?

Pasco!


Pasco

I wrote with confidence! #lowassa hakatishi #teamlowassa mkafoka balaa Mr. President kaibuka au kakimbia Id?
 
Home > Member List
View Profile: Mr. President
User Name: Mr. President
User Title: Banned
Last Activity: Yesterday 12:03

Copyright JamiiForums.com
 
kama lowassa anafikiri watanzania wengi wanampenda ahame chama ndipo atajua hasira za watanzania juu yake,aling'ang'ania ccm kwa sababu alijua ni chama chenye dola atashinda kwa mbinu zote hata kwa goli la mkono lakini nje ya ccm hana nguvu zozote na akitoka kamati ya maadili ya ccm itamfungia kazi mwisho wake ataishia gerezani au kufilisiwa kabisa pia nawapa pole wapambe wake ndio wajue rais hachaguliwi kihuni kama walivyofikiri
Kwa bandiko hili ndipo utaona kuwa ccm ni chaka la wahalifu na wanalazimishwa daima wasikemee uhalifu kwa kigezo cha kufilisiwa.
Nyota njema kwa mara ya kwanza Tanzania kwamba uwezekano wa kuiondoa ccm madarakani umekuwa mkubwa sasa zaidi ya wakati wowote, ngoja tuendelee kuamini kuwa kweli JK ni chaguo la Mungu!

 
Nyerere aliwahi kusema ni heri mbuzi kuwa mgombea wa CCM kuliko mkristo kuwa raisi wa Tanzania, hii imetimia. Majina yote 5 yaliyo chaguliwa CCM ni uislam mtupu. Tumechoshwa ni team uislam ndani ya CCM, mahamuzi magumu yanaitajika sasa.
Hivi mnapata faida gani kupotosha uko shule mlikwenda kusoma nini ujinga?

Membe na Maghufuli ni Waislam?
 
Back
Top Bottom