Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Wakati Tundu Lissu akikamatwa na kuswekwa Gerezani kwa tuhuma za hila dhidi yake na Chadema.
Wakati viongozi na Makada wa Chadema wakitekwa, kuuwawa na kupotezwa.
Wakati Maofisa wa System wakienda kumwaga vitu vya kemikali kwenye Ofisi za Chadema Mbeya kuwatisha Wanachadema na Wanambeya kuacha kumdai Mdude Nyangali
Wakati Chadema ikinyimwa viwanja vya kufanya mikutano na Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Mikoa.
Wakati watetezi wa haki na Wakosoaji wa Serikali akiwemo Padre Kitima na wengineo wengi wakijeruhiwa na kuumizwa huku waliofanya matukio hayo wakiwa wanatesa mitaani.
Wakati Watumishi wa Mungu na Wananchi wanaoteteza na kuhubiri haki kama Askofu Bagonza na Boniface Mwabukusi wakitishiwa maisha na kuuwawa,
Bado Serikali ya CCM na System yao kwa Kumtumia Msajili wa Vyama vya Siasa na Mapandikizi waliyoyatengeneza Chadema Wametengua uteuzi wa Wajumbe 8 wa Kamati Kuu ya Chadema.
Kila siku huwa nasema inawezekana CCM na wajinga wao waloowajaza kwenye System hawajui kitu wanachokitengeneza. Wanadhani mambo wanayoyafanya ni mapya sana duniani ila ukweli ni kwamba haya mambo yalishafanywa sana na Serikali na kidhalimu huko nyuma ambazo zilikuja kuanguka kwa namna ya kutisha na kusikitisha sana.
Kinachonifurahisha zaidi ni kwamba haya yote yanayofanywa na CCM na System ya Serikali yanazidi kuwaelewesha Watanzania ambao hata hawakuwahi kufuatilia siasa za Tanzania kuwa hakuna usawa katika kufanya siasa nchini Tanzania.
Kinachonifurahisha ni kwamba hizi ghiriba wanazofanyiwa Chadema na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa pamoja na Polisi na Vyombo vingine vya dola zinawafanya Watanzania kuelewa zaidi mantiki iliyopo kuhusu No Reforms No Election.
Watapigana lakini Hawatashinda.
Chadema itasimama kwa nguvu na uweza wa Mungu.
Lord denning,
Mwanza