mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Wanaolaumu uongozi wa TPA au mwekezaji wa awali (Ticts) ataje Shirika lolote la Umma lililofanya kwa ufanisi na tija. Ukweli ni kwamba mfumo wa uteuzi na uwajibishaji wa Wakuu wa mashirika ya umma ndiyo mbovu, au usimamizi wake ni dhaifu.Tuache kuwasingizia uongo wazalendo wetu walioitunza bandari yetu miaka yote pamoja na kwamba wamekuwa wakishibisha matumbo yao hapo hapo, na kingine kingi kilichobakia wakatupatia na sisi walalahoi tusife njaa.
Hili la kuwapa DP world bandari zetu zote bure na milele ni uhuni tu wa watawala na wala halina uhusiano wowote na ufanisi duni wa pale bandarini. Kwanini? Watawala wamedhamiria zaidi kuwapa waarabu wa Dubai umiliki wa milele wa bandari zetu zote na sio kuboresha bandari yetu.
Hivyo, basi tutegemea bandari kugeuzwa shamba la bibi, DPW itakapoanza kazi, kwa jinsi ile ile madini na maliasili zingine zinavyochotwa.
Nasimamia kumpongeza Mwendazake kwa jinsi alivyosimamia rasimali za Taifa.