Kukosea kupiga simu kwanini iwe kwa watu wa kabila moja?

Kukosea kupiga simu kwanini iwe kwa watu wa kabila moja?

Nilishapata wrong calls nyingi za aina hii, ila kuna mama mmoja sijui ndio wa usukumani huko mpaka nilimzoea ikabidi nisevu namba yake "mama wa kisukuma" maana alikuwa kama mama angu hazipiti siku tatu bila kunipigia
 
Sijui kwanini aisee..wasukuma na Waha sijui kuna tatizo gani huko,halafu kingine hata zile namba ambazo zinabadilishwa na kupewa mtumiaji mwingine baada ya mwenye nayo kuitelekeza nazo pia wanazielekezea huko si mara moja nakutana na kesi hiz

Tunapoteza Sana line. Matokeo yake anapewa mtu mwingine.
Jingine idadi yetu ni kubwa mnoo
 
Mimi sio mfuasi wa kuponda makabila, nawapenda wote, hata mwenzi wangu sio wa kabila langu. Lakini najiuliza kwanini kila ninapopigiwa simu ya kukosewa huyo mtu anakuwa msukuma, kama sio mwanaume atakuwa mwanamke.

Nawajuaje? Mara nyingi husalimia kikwao, ama kuita majina yao, tunaposhindwa kuelewana huwa nawaambia wamekosea kupiga.

Wengine watarudia mara mbili au tatu na wakati umemwambia amekosea.
Hoja yangu ni kwamba kwanini wawe wasukuma tu? Ina maana nchi hii ina idadi kubwa ya Wasukuma? Au nini ndugu zangu?
Nikusaidie Tu.

1. Mwanza
2. Shinyanga
3. Simiyu
4. Geita
5. Tabora
6. Katavi
7. Bunda.
8. Ifakara.
9. manyoni.
10. Chunya
11. Kibiti
12. Sumbawanga
13. Pemba.
14. Wilaya ya kigamboni
15. Na wilaya zote za Tanzania ukitoa mikoa ya Kilimanjaro. Arusha na Manyara the rest of the area wamejaa na kuzaana saana.

So the main point is they are many.
 
Wasukuma oyeeeeeeee


Kazi na iendelee[emoji7]
Unachukua namba yako au ya mtu ye yote kwenye contact list yako halafu unabadilisha namba moja ya mwisho, mwanzoni au katikati halafu unapiga. Lazima utakutana na mtu tu hata iweje.

Ila leo nimepiga nikakutana na Msukuma mwenzangu halafu wagūkaya kabisa tumeishia kupiga stori tu. Nimepiga nyingine nimekutana na Mpemba sijui maana Kiswahili chake kikali mpaka siyo poa yaani. Hapa nataka nipige ya mwisho kwa leo. Usije ukashangaa inakuangukia wewe mjukuu. Ajenda ya leo kila ninayempigia namuuliza kama ni memba wa JF 😁
 
Unachukua namba yako au ya mtu ye yote kwenye contact list yako halafu unabadilisha namba moja ya mwisho, mwanzoni au katikati halafu unapiga. Lazima utakutana na mtu tu hata iweje.

Ila leo nimepiga nikakutana na Msukuma mwenzangu halafu wagūkaya kabisa tumeishia kupiga stori tu. Nimepiga nyingine nimekutana na Mpemba sijui maana Kiswahili chake kikali mpaka siyo poa yaani. Hapa nataka nipige ya mwisho kwa leo. Usije ukashangaa inakuangukia wewe mjukuu. Ajenda ya leo kila ninayempigia namuuliza kama ni memba wa JF [emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]


Kama yule was geita alivyowapigia zima moto kwa kujifrahisha[emoji16][emoji16][emoji16]

Wasukuma bana
 
Ila daah!mnajitahidi kuongeza binadamu duniani.mwingine alinambia ni Nehema yupo kwimba!
Mimi hapa nina watoto tisa na bado naongeza wengine. Ni kufyatua tu yaani.

Huyo Nehema ulimwacha hivi hivi tu? 😁😁😁
 
Nikajua ni tatizo langu alone kumbe ni mtambuka, yani kuna line ya voda nilisajili ikabidi nitupe.
Maana kila siku simu zaidi ya tano Halafu ukiwaambia sio Wewe wanamaindi kinoma.
Akipiga tu utasikia we shija, we magadula
Mmoja alinipigia akasema shiiiiiiino nikamuambia shiino mama ako
 
Wasukuma hongereni sana👏👏👏👏
 
Back
Top Bottom