Kuku kibudu aliyekufa akachinjwa ana shida gani?

HII NDO AYA MNATUMIA KUMTETEA KITIMOTO MBNA LEO UMEGEUKA TENA UNASEMA HAVUNGUMZII CHAKULA
 
Hamna shida mbona kwenye vilabu vya taputapu watu wanakunywa mpaka supu za mizoga
Makabila mengi tu hapo zamani walikuwa wananyonga. Hii kuchinja siyo jadi yetu waafrika. Kama baadhi ya wachaga walikuwa wanachukuwa ng'ombe mzima, wanamfunga kamba kwa kumlaza chini kama wanamchinja halafu wanaziba matundu ya pua kwa matope na mdomo wanaufunga kwa kamba. Mnyama anateseka kwa kukosa hewa mpaka anakufa.
 
Mwanadamu ni kiumbe pekee kwenye uso huu wa ardhi ambaye anayeweza kutumia akili aliyoumbiwa nayo ili kuweza kuyasarifu maisha yake, mwandamu huyu amepitia hatua mbalimbali katika maisha yake mpaka amefikia hapa alipo. Katika sifa za viumbe hai kula ni mojawapo, na hii ndiyo sifa iliyo muhimu sana ambayo ndiyo inayomuwezesha mwanadamu kuwa hai. Wengi wa wanadamu waliishi na wanaishi kutokana na miongozo inayosemekana imetoka kwa Mungu, lakini leo hii kutokana na hiyo akili aliyopewa binadamu na kuweza kujua mengi ambayo huko nyuma alikuwa hayajui, elimu imemuwezesha kutambua chakula gani ni kizuri kwa afya na chakula gani si kizuri kwa afya yake. Hata kama ukisoma vitabu vya imani viliweza kuainisha kipi kiliwe na kipi kisiliwe, hata Adamu alivyoumbwa aliambiwa asile tunda la mti fulani au asiukaribie kabisa huo mti, kwani kuna baadhi ya vyakula vinaathiri mwili na hata akili ya mwanadamu. Leo hii tunaona kuna tatizo la nguvu za kiume kupotea hata kwa vijana wetu ila ukiangalia tatizo hilo linasababishwa na vyakula tunavyokula, kwani "ufisadi umedhihiri nchi kavu na baharini kwa yale yanayofanywa na wanadamu kwa mikono yao."
 
🙆🤷🤷
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…