Kuku kibudu aliyekufa akachinjwa ana shida gani?

Kuku kibudu aliyekufa akachinjwa ana shida gani?

Ni sawa na kupiga risasi maiti
Utasema umemuua?
Kuku kafa sasa kuna maana gani kupitisha tena kisu shingoni?

Ili utuonyeshe waalikwa kuwa umechinja eti 😄 🤣
Huyo mheshimiwa ametafsiri kuchinja kuwa ni ile kazi ya kumnyonyoa huyo kuku mfu, kumpasua, kuondoa utumbo na kumkatakata vipande ili aweze kupikwa au kuandaliwa kama chakula. Hatua hizo ni mchakato yan anamchakata (Process) kuku mfu.
Nadhani nimemsaidia kwa nia njema tuu kufafanua alichomaanisha. Kama sivyo; basi naomba aje akanushe hapa.
 
Mnyama yoyote akifa mwenyewe bila kuchijwa hana Radha yoyote labda mahotelin kwa sababu utakuwa amewekewa vitu vingivingi
 
Sina utaalamu lkn naona kuna haja ya mnyama kumwaga damu yake kabla kumuandaa kwa mapishi.
Sina uhakika lkn nawaza tu, bila kumwagika damu mnyama jee huwa hana madhara? Nahisi kuna umuhimu kwa mwili wa mnyama kuupunguza damu kabla ya kumuandaa kwa mapishi
sawa na wataalamu wa afya wanasema mnyama/ndege kuchinjwa kunasaidia kuondoa bacteria mbalimbali ambao wanaweza kusababisha madhara kwa binadamu.Fikiria mnyama/amekufa kwa kula sumu akifa kibudu bila ya kunjinjwa maana yake ni kwamba sumu isalia mwilini mwa mnyama na kumletea madhara mlaji
 
Hakuna madhara yoyote kiafya kumla mnyama ambaye damu yake haijamwagika kama chakula. Wale Jamaa wengine hula "kisusio".
Ni kweli inafaa kuupunguza mwili wa mnyama damu kama atatumika kama chakula kwa sababu damu ikivia ndani ya mwili; mwili huo(Nyama) huharibika mapema sana, muonekano wa nyama hauvutii walaji inakuwa nyekundu mno na ladha yaweza kubadilika kwa kiasi fulani kwani virutubisho(Nutrients) na takamwili (metabolic Waste products)vilivyokwenye mzunguko wa damu hubaki kwenye nyama. Ila usiogope we twanga/kula kama huna kinyaa.
 
Ni sahihi kabisa na wapo watu waliowahi kuathirika (hata kufa) kwa ulaji huo.
 
Eti wakuu kwa mfano kuku kafa na na ndani ya nusu saa akachinjwa ana shido gani kuliwa?mimi sielewi mantiki ya kuku kutoliwa baada ya kufa nachojua ili mfugo aliwe lazima AFE kwanza..
Kama amekufa kwa maradhi hatari ukimla unamsindikiza chap
 
"Kuku kibudu aliyekufa akachinjwa " hiyo heading tu imemaliza kila kitu,utachinjaje kuku aliyekufa? Maana hata mwaga damu
 
Hakuna madhara yoyote kiafya kumla mnyama ambaye damu yake haijamwagika kama chakula. Wale Jamaa wengine hula "kisusio".
Ni kweli inafaa kuupunguza mwili wa mnyama damu kama atatumika kama chakula kwa sababu damu ikivia ndani ya mwili; mwili huo(Nyama) huharibika mapema sana, muonekano wa nyama hauvutii walaji inakuwa nyekundu mno na ladha yaweza kubadilika kwa kiasi fulani kwani virutubisho(Nutrients) na takamwili (metabolic Waste products)vilivyokwenye mzunguko wa damu hubaki kwenye nyama. Ila usiogope we twanga/kula kama huna kinyaa.
sio kweli kula nyama ambayo haijachinjwa kuna madhara makubwa kiafya, Nimetoa mfano mnyama ambaye amekula sumu Kama asiponjinjwq ile sumu itaenea mwili mzima wa mnyama na hii itapelekea mlaji kupata madhara makubwa
 
Kwa mtizamo wako huo; basi elewa fika kwamba kuchinja sio kigezo cha kuondoa sumu mwilini. Kwa mfano mnyama aliyekufa kutokana na kula sumu ya panya (zinc sulphide) hata ukimchinja halafu ukajichanganya eti umemchinja na ukala hiyo nyama; basi na wewe ni bye bye. Ndo mana wadau hapo juu walisema kama ukijua kisababishi cha kifo na ukaridhika hakuna madhara, waweza kula. Mnyama aliyekufa kwa kugongwa na nyoka ukila hata bila kumchinja huyo mnyama hakuna madhara. Umeona hizo tofauti? Pote kisababishi cha kifo ni sumu na pote mnyama hakuchinjwa i.e. damu haikumwagwa.
 
Mmmmh. Ukienda kwa mtizamo huo; basi hutokaa ule chochote kwani hakuna kitu chochote (sio vyakula tuu bali hata hewa unayovuta wamejaa tele) kisichokuwa na vimelea (microbes) i.e. Fungi, Protozoa, Bacteria na Viruses.
Hoja mtambuka ni Je, ni wenye kuleta madhara kwa mtumiaji??? Kumbuka wengine ni muhimu sana wawepo ili maisha yako na yangu yaendelee i.e. wanafaida/manufaa makubwa katika mustakabali wa Uhai wetu wanadamu na viumbe vingine hapa duniani. Mungu muumbaji ni fundi sana. Tunamshangaa na hatumwelewi na hatutakaa tumwelewe.
Na ndio maana kuna namna ya kuandaa nyama na sisi waislam tumeelekezwa kabla ya kula tuseme Bismillah.
 
Kuchinjwa ni Kabla ya kufa,. Sio afe ndo achinjwe. Ni vile ninavyoamini Mimi. Kama kashakufa ni haramu na mwenyezimungu anajua zaidi.
Upo porin unawinda na mishale
Ukamchoma swala mshale swala akakimbia ukamfuatilia ukakuta amekufa
Je huyu swala nae hafai kuliwa?? Coz umekuta ameshakufa?
 
Kikubwa awe kifo chake hakikutokana na sumu au magonjwa ya kuambukiza, kama amekufa kifo cha kawaida hiyo ni nyama halali kwa imani ya kidunia, ila ukiamua kuishi kidini basi fata masharti ya dini yako kadri utakavyokua umedanganywa.
 
Back
Top Bottom